Posts

MAJUKWAA YA MAZUNGUMZO KUIMARISHA SEKTA YA MADINI

Image
Makongamano na majukwaa yanayojadili mwenendo, changamoto na maendeleo ya sekta ya madini ni nguzo muhimu katika kuimarisha sekta hiyo na kuhakikisha inatoa mchango mkubwa zaidi katika maendeleo ya Taifa. Hayo yamebainishwa na Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Moses Kongola, kwa niaba ya Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, wakati akifunga kongamano la siku mbili lililoandaliwa na HakiRasilimali, lililojadili tafiti mbalimbali, maendeleo na nafasi ya Tanzania katika sekta ya madini mkakati. Mhandisi Kongola amesema majukwaa hayo ni muhimu kwa kuwa yanatoa fursa kwa Serikali, wadau wa sekta ya madini, watafiti, wachimbaji na jamii kujadili kwa pamoja namna ya kukabiliana na changamoto zilizopo na kutumia ipasavyo fursa zinazotokana na utajiri wa madini nchini. Amesema Serikali inaendelea kuweka mkazo katika uongezaji thamani madini nchini kabla ya kusafirishwa nje ya nchi, hatua ambayo itasaidia kuongeza mapato ya Serikali, ajira na fursa za kiuchumi kwa Watanzania. “Ni wajibu wa ki...

CHANDA CHEMA HUVIKWA PETE

Image
Maafisa na askari  wa jeshi la Uhifadhi wa Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro waliopoteza maisha, kujeruhiwa na kufanya kazi kwa uhodari wametunukiwa vyeti na fedha kutokana na kujitoa kwao kwa hali na mali kulinda rasilimali za wanyamapori na misitu. Tuzo hizo zimetolewa tarehe 31 Julai 2026 kwenye maadhimisho ya  siku ya  askari wanyamapori duniani ambayo huadhimishwa kwa lengo la kuutambua mchango wa  askari hao katika kulinda rasilimali za nchi na kuenzi mchango wa Askari 10 waliopoteza maisha yao na kujeruhiwa wakiwa kazini katika hifadhi ya Ngorongoro. Naibu kamishna wa Uhifadhi huduma za shirika Aidan Makala  amewapongeza askari wote wa jeshi la uhifadhi kutokana na  kujitoa kwa hali na mali katika kazi hiyo huku akiwasisitiza kufanya kazi kwa kushirikiana na wananchi ili kulinda matakwa ya haki jinai. Naibu Kamishna Makala ameleza kuwa,  askari  wa  uhifadhi ni nguzo ya ulinzi wa rasilimali za wanyamapori  na misitu ambapo ...

SERIKALI,WAWEKEZAJI NA WATOA HUDUMA MIGODINI WAJADILI CHANGAMOTO NA MAFANIKIO SEKTA YA MADINI

Image
Dar es salaam Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau wa sekta ya madini kupitia majukwaa ya majadiliano kwa lengo la kujenga sekta yenye ushindani, inayovutia uwekezaji na kutoa mchango mkubwa katika ukuaji wa uchumi wa Taifa. Mhe. Mavunde ameyasema hayo katika kikao cha Mining Breakfast Briefing (*MBB*), kilichoandaliwa kwa ushirikiano wa Chemba ya Migodi Tanzania(TCM) na Wizara ya Madini, ambapo ametoa wito kwa wadau kuendelea kutumia majukwaa hayo kujadili fursa na changamoto zinazohusu sekta ya madini. Amewashukuru viongozi na wanachama wa Chemba ya Migodi Tanzania kwa kuendelea kutoa nafasi ya Serikali na wadau kukutana na kujadiliana kuhusu masuala mbalimbali ya sekta hiyo, huku akilipongeza Mantra Tanzania Limited kwa kudhamini kikao hicho. Amesema ushiriki wa wadau katika majukwaa hayo unaonesha dhamira ya pamoja ya kujenga sekta ya madini yenye ushindani, inayovutia mitaji na teknolojia, pamoja na kuhakikisha rasilimali za mad...

HABARI KUBWA KATIKA MAGAZETI YA JULAI 30,2026

Image

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO

Image