Posts

MAMA FATMA KARUME AFARIKI DUNIA

Image
  Mama Fatma Karume, aliyekuwa mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, amefariki dunia leo, Septemba 21, 2026. Taarifa za kifo chake zimefika wakati akiwa nyumbani kwa mmoja wa watoto wake huko Zanzibar. Mama Fatma Karume alikuwa mjane wa Hayati Sheikh Abeid Amani Karume, Rais wa Kwanza wa Zanzibar, ambaye aliiongoza Zanzibar baada ya Mapinduzi ya Januari 12, 1964. Kifo chake ni msiba mkubwa kwa familia, ndugu, jamaa na wananchi wa Zanzibar. Taarifa zaidi kuhusu mazishi na ratiba nyingine za msiba zinatarajiwa kutolewa na Serikali. Mama Fatma Karume amefariki akiwa na umri wa miaka 97.

WAZIRI MKUU KUMWAKILISHA RAIS DKT. SAMIA KATIKA MKUTANO WA AFYA MOJA NCHINI ITALIA

Image
Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba ameondoka nchini leo (Jumamosi, Septemba 19, 2026) kwenda Roma, Italia kumwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika Mkutano wa siku tatu wa Kimataifa wa Kujadili Afya Moja na Mifumo ya Chakula na Kilimo.   Mkutano huo utakaofanyika katika Makao Makuu ya Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), jijini Roma, Italia kuanzia Septemba 21–23, 2026 unalenga kuimarisha utekelezaji wa dhana ya Afya Moja (One Health) inayotambua uhusiano kati ya afya ya binadamu, wanyama, mimea na mazingira, kwa lengo la kuhakikisha mifumo endelevu ya chakula na kilimo   Mkutano huo utahusisha viongozi wa nchi na Serikali, wakiwemo Marais kati ya watano hadi saba, Mawaziri kati ya 30 hadi 50, pamoja na wawakilishi wa taasisi za kikanda na kimataifa, wadau wa maendeleo, sekta binafsi, taasisi za utafiti na mashirika ya kimataifa.   Mambo muhimu yatakayojadiliwa katika mkutano huo ni Ujumuishaji wa dhana ya Afya Moja (One Health) katika sera na uw...

MAKAMU WA RAIS AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA MTO NG’OMBE, AAGIZA TAKA ZIONDOLEWE HARAKA

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, amefanya ziara ya kushtukiza katika eneo la Mto Ng’ombe, Tandale jijini Dar es Salaam, kukagua hali ya usafi wa mazingira na maandalizi ya kukabiliana na athari zinazoweza kujitokeza katika kipindi cha mvua.   Akiwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Waziri wa TAMISEMI pamoja na viongozi wa Wilaya ya Kinondoni, Mhe. Ndejembi ameelekeza Mkoa wa Dar es Salaam kuhakikisha mto huo unasafishwa na taka zilizorundikana kandokando ya Mto Ng’ombe zinaondolewa haraka na mazingira yanaendelea kuwekwa katika hali ya usafi.   Amewaagiza Viongozi wa Halmshauri, kupitia maafisa mazingira na maafisa maendeleo, kuendelea kutoa elimu kwa wananchi namna ya kuzingatia usafi na ukusanyaji wa taka. Amesema ni muhimu kwa Halmashauri kuweka miundombinu mizuri ya kukusanya taka na kuzichukua kwa wakati ili wananchi wasitupe taka hizo katika maeneo yas...

LOWASSA: MSHIKAMANO TANZANIA, MAREKANI UONGEZE FURSA ZA UWEKEZAJI

Image
  Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Tan Communication Media Ltd, inayomiliki na kuendesha kituo cha redio cha Redio 5 cha jijini Arusha, Robert Lowassa, amesema mshikamano baina ya Marekani na Tanzania yaongeze fursa zaidi za uwekezaji nchini. Lowassa ameyasema hayo leo wakati alipokutana na kufanya mazungumzo na Msemaji na Afisa Habari wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, Nice Cole ofisini kwake Arusha.   Amesema Marekani imekuwa mshirika muhimu kwa Tanzania katika maeneo mbalimbali, ikiwemo utalii, biashara, uwekezaji na miradi ya maendeleo.   Lowassa amesema ni matumaini yake kuwa mshikamano huo utaendelea kuwa imara zaidi ili kufungua fursa nyingi zaidi za uwekezaji na maendeleo kwa manufaa ya pande zote mbili.   Naye Mkurugenzi Mtendaji wa TanMedia, Angela Maina, amekaribisha ushirikiano huo, akisema Arusha na Tanzania kwa ujumla vina nafasi kubwa ya kunufaika zaidi kupitia mafunzo kwa vijana na waandishi wa habari, pamoja na programu za kubadilishana uzoefu (excha...

TANZANIA YAZIDI KUIMARISHA NAFASI YAKE KATIKA BIASHARA YA UMEME KIKANDA

Image
  Na Mwandishi Wetu, Zanzibar Tanzania imeendelea kuimarisha nafasi yake katika biashara ya umeme kikanda, huku Mradi wa Kuunganisha Gridi za Umeme Tanzania na Zambia ukifikia asilimia 90 ya utekelezaji na kutarajiwa kukamilika Februari 2027, hatua itakayoiunganisha Tanzania na soko la umeme la Kusini mwa Afrika na kuongeza fursa za biashara ya umeme kuvuka mipaka. Akizungumza, Septemba 11, 2026, katika ufunguzi wa Mkutano wa 67 wa Kamati ya Usimamizi ya Jumuiya ya Umeme ya Kusini mwa Afrika (SAPP), Naibu Waziri wa Maji, Nishati na Madini wa Zanzibar, Mhe. Seif Kombo, amesema kuimarisha biashara ya umeme kuvuka mipaka ni muhimu katika kuongeza upatikanaji wa nishati, kuimarisha usalama wa gridi na kupunguza gharama za umeme katika ukanda huo. Ameeleza kuwa Tanzania, kupitia Serikali na TANESCO, inaendelea kuwekeza katika kuimarisha miunganisho ya gridi, ikiwemo Mradi wa Tanzania-Zambia wa msongo wa kilovoti 400 ambao, utakapokamilika, utaongeza uwezo wa Tanzania kushiriki katika bi...

MAKAMU WA RAIS AAGWA RASMI NA WIZARA YA NISHATI

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Deogratius Ndejembi, ameagwa rasmi na Menejimenti ya Wizara ya Nishati pamoja na Taasisi zilizo chini yake katika hafla iliyofanyika katika Ukumbi wa Kambarage Treasury Square, Dodoma. Jumatano Septemba 09, 2026.   Hafla hiyo imehudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughukia Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Felchesmi Mramba, Menejimenti ya Wizara na Wakurugenzi wa Taasisi zilizopo chini ya Wizara hiyo.   Akizungumza katika hafla hiyo, Makamu wa Rais amewaasa Viongozi na Watendaji hao kuendelea kumwombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, pamoja na Wasaidizi wake ili waendelee kutekeleza majukumu yao ya kuwahudumia Watanzania.   Aidha, Makamu wa Rais amewataka Viongozi na Watendaji hao kuendelea kufanya kazi kwa bidii, weledi, uaminifu na uzalendo ili kutimiza matarajio ya wananchi kwa Serikali.

SAPP KUFUNGUA FURSA KWA TANZANIA KUWA KITOVU BIASHARA YA UMEME KUSINI MWA AFRIKA

Image
MIKUTANO ya 67 ya Jumuiya ya Umeme ya Kusini mwa Afrika (SAPP) inayofanyika Zanzibar imefungua fursa mpya kwa Tanzania kuimarisha nafasi yake kama kitovu cha biashara ya umeme katika ukanda wa Kusini mwa Afrika, huku ikitarajiwa kuongeza mapato ya taifa kupitia mauzo ya umeme na kuimarisha usalama wa nishati katika ukanda huo. Mikutano hiyo imewakutanisha wajumbe kutoka nchi wanachama 18 wa SAPP kwa lengo la kujadili masuala ya biashara ya umeme, uendeshaji wa mifumo ya umeme, uwekezaji katika miundombinu ya nishati na usalama wa nishati katika nchi zilizoko ukanda wa Kusini mwa Afrika. Akifungua mikutano hiyo Septemba 8, 2026 katika Hoteli ya Golden Tulip, Zanzibar, Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO), Bw. Haji Mohamed Haji, amesema kuimarishwa kwa uunganishaji wa gridi za umeme kati ya nchi wanachama kutarahisisha biashara ya umeme kuvuka mipaka na kuwezesha nchi zenye ziada ya umeme kuziuzia nchi zinazokabiliwa na upungufu wa nishati. Amesema ushirikiano huo utaongeza uf...