Posts

Showing posts from November, 2025

MRADI WA UMEME KISHAPU KIELELEZO CHA ONGEZEKO LA UZALISHAJI UMEME NCHINI – DC KISHAPU

Image
Mkuu wa Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga, Mhe. Peter Masindi, amesema mradi wa umeme unaozalishwa kwa nguvu ya jua ni kielelezo cha ongezeko la uzalishaji wa umeme nchini  ikiwa ni dhamira ya Serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ya kutaka kuongeza uzalishaji umeme hadi kufikia jumla ya megawati 8000 ifikapo mwaka 2030. Mhe. Masindi aliyasema hayo Novemba 28, 2025, alipoambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Bw. Lazaro Twange, kukagua maendeleo ya Mradi wa kuzalisha umeme wa jua unaotekelezwa wilayani humo. Amesema mradi huo sio tu utakuwa na faida kwa wananchi wa Mkoa wa Sinyanga pekee bali hadi katika mikoa ya Jirani ambapo pia amesema zaidi ya wananchi 1,200 waliokuwa wakiendesha shughuli zao katika eneo la Mradi tayari  wamelipwa fidia na kwamba jamii imeupokea mradi kwa mtazamo chanya na imekuwa mstari wa mbele kulinda miundombinu. “Mradi huu ni tegemeo kwa wananchi  wa Kishapu wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha miundombinu inalindwa. Wameuelewa Mradi na ...

MIONGOZO ITAKUWA RAFIKI KWENYE UPATIKANAJI WA MIKOPO KWA WANAWAKE DODOMA: NAIBU WAZIRI MARYPRISCA

Image
Na Jackline Minja WMJJWM-  Dodoma. Wizara kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkoa wa Dodoma itaendelea kushirikiana kwa karibu na jukwaa la viongozi la uwezeshaji wanawake kiuchumi jijini Dodoma, kwa kuhakikisha mazingira wezeshi ya biashara yanaimarishwa, Sera na Miongozo rafiki inatekelezwa na fursa zaidi za maendeleo zinapatikana kwa wanawake wote bila ubaguzi. Akizungumza na viongozi pamoja na wajumbe wa Jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Jiji la Dodoma Novemba 28,2025 Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mhandisi. MaryPrisca Mahundi amesema Majukwaa hayo yamekuwa chachu ya mabadiliko katika maisha ya wanawake wa jiji la Dodoma ambapo yameongeza uelewa wa masuala ya fedha, yamewajengea uwezo wa kiuongozi na yamewapa ujasiri wa kuanzisha na kuendeleza shughuli mbalimbali za kiuchumi. “Majukwaa haya ya wanawake yana umuhimu mkubwa katika ustawi na maendeleo ya wanawake na yameanzishwa ili kutoa fursa kwa wanawake kuweza kukutana, kuchochea ubu...

TBN YATOA UFAFANUZI KUHUSU MKUTANO WA IKULU DAR ES SALAAM

Image
Mtandao wa Wanablogu Tanzania (TBN) unapenda kutoa ufafanuzi rasmi na kuweka mambo wazi kufuatia taarifa zisizo sahihi na zinazoleta utata zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu mkutano uliofanyika hivi karibuni Ikulu. TBN inakanusha vikali madai yanayosambazwa na baadhi ya watu wanaojiita wanaharakati, wakidai—bila uthibitisho wowote—kuwa wanahabari wa maudhui ya mtandaoni waliitwa Ikulu jijini Dar es Salaam kwa lengo la "kupewa maelekezo" kuhusu maandamano yanayodaiwa kupangwa kufanyika tarehe 9 Desemba. Kusudi Halisi la Mkutano TBN inathibitisha kuwa madai haya si sahihi na yamekuwa yakipotoshwa. Kusudi la kweli na la moja kwa moja la wito wa Ikulu lilikuwa hili: Mkurugenzi mpya wa Mawasiliano Ikulu, Bw. Bakari Machumu, alifanya mkutano wa utambulisho rasmi na wadau muhimu wa sekta ya habari, akianza na wanahabari wa maudhui ya mtandaoni. Mkutano huu ulikuwa ni hatua muhimu ya kuweka msingi wa ushirikiano na mawasiliano bora. Hakukuwa na ajenda iliyofichwa, wala ...

MIKOPO IWE CHACHU YA KUKUA KIUCHUMI NA KUZITUNZA FAMILIA ZENU – MHE. MARYPRISCA

Image
Dodoma. Serikali imeendelea kuanzisha  Majukwaa ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi  kuanzia ngazi ya Vijiji/Mtaa, Kata, Wilaya na Mkoa ambapo  Katika kipindi cha mwaka 2020 hadi 2025, jumla ya Majukwaa 15,147 yameanzishwa, ambayo yameleta chachu kwa wanawake ya kujifunza masuala ya ujasiriamali, elimu ya fedha na uwekezaji. Hayo yamesemwa na Naibu wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia , Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mhandisi MaryPrisca Mahundi wakati akizungumza na wanavikundi vya malezi na matunzo ya watoto Kata ya Ihumwa Jijini Dodoma. Mahundi amesema katika eneo la fursa za kiuchumi, Wizara inaratibu na kusimamia jukumu la kuwezesha kiuchumi wafanyabiashara ndogondogo na wao wakiwa miongoni mwao watatambuliwa na kuwasajili na kutoa mikopo yenye masharti nafuu, katika zoezi linalosimamiwa na Maafisa Maendeleo ya Jamii, Maafisa TEHAMA pamoja na Maafisa Biashara ngazi ya Mikoa na Halmashauri. “Tangu zoezi hili lilipoanza mwezi Februari, 2024 hadi kufikia tarehe 26 Novemba, 2025 j...

MKURUGENZI WA MAWASILIANO YA RAIS IKULU BAKARI MACHUMU AKUTANA NA WANABLOGU NA WAZALISHAJI MAUDHUI MTANDAONI IKULU DAR

Image
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bw. Bakari Machumu akiwa na viongozi mbalimbali kwenye picha ya pamoja na Waandishi wa Habari wa Mtandaoni, pamoja na Wanablogu mbalimbali, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Novemba, 2025. Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bw. Bakari Machumu akizungumza na Waandishi wa Habari wa Mtandaoni pamoja na Wanablogu mbalimbali, Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujitambulisha na kupokea maoni yao, ikiwa ni mfululizo wa mikutano na wadau wa Tasnia ya Habari kwa ajili ya kuboresha masuala mbalimbali ya Mawasiliano baina ya Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu na Vyombo vya Habari, tarehe 27 Novemba, 2025. Viongozi mbalimbali wakizungumza katika Kikao cha pamoja cha Waandishi wa Habari wa Mtandaoni, Wanablogu mbalimbali pamoja na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Bw. Bakari Machumu, Ikulu Jijini Dar es Salaam, tarehe 27 Novemba, 2025. Mwenyekiti wa Tanzania Bloggers Network  (TBN), Beda Msimbe akifafanua jambo .   ...

NAIBU WAZIRI WA NISHATI AKUTANA NA MENEJIMENTI YA EWURA, ATOA WITO WA KASI NA UFANISI ZAIDI

Image
  Naibu Waziri wa Nishati, Salome Makamba, leo tarehe 24.11.2025 amekutana na Menejimenti ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), ikiwa ni mara ya kwanza tangu kuteuliwa katika nafasi hiyo hivi karibuni. Makamba amekutana na viongozi hao kwa lengo la kujadiliana masuala mbalimbali ya utendaji na maboresho ya sekta ya nishati nchini. Mkutano huo umefanyika katika Ofisi za Makao Makuu ya EWURA jijini Dodoma. Aidha, ameipongeza EWURA kwa kazi nzuri katika kusimamia huduma za nishati, na kuitaka Mamlaka hiyo kuongeza kasi, ubunifu na ufanisi. “Mimi si muumini wa kushindwa, hivyo natoa rai kwenu kujipanga ili kuendana na kasi hiyo, ili muendelee kung’ara katika uendeshaji wa shughuli zenu” alisema. Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Andilile, aliwasilisha mbele ya  Makamba taarifa fupi kuhusu majukumu ya Mamlaka, mafanikio yaliyopatikana, pamoja na maeneo yanayoendelea kuimarishwa. Dkt. Andilile aliahidi taasisi yake kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa maj...

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO

Image

ZAIDI YA WAGENI 140 KUTOKA MATAIFA MBALIMBALI WATEMBELEA HIFADHI YA KILWA KISIWANI

Image
-Watopezi wa Masuala ya Malikale Wanogesha Ziara ya Wageni hao Hifadhi ya Urithi wa Utamaduni wa Dunia ya Magofu ya Kale ya Kilwa Kisiwani na Songo Mnara wilayani Kilwa imeendelea kuwa kivutio kikubwa kwa watalii kutoka ndani na nje ya nchi, ambapo tarehe 31 Oktoba 2025 ilipokea jumla ya watalii 147 kutoka mataifa mbalimbali duniani waliowasili hifadhini humo kwa kutumia meli ya kifahari iitwayo SH Diana, kwa lengo la kutalii na kujionea vivutio vya kihistoria vilivyopo katika eneo hilo. Watalii hao walitoka katika nchi 13 zikiwemo Ufaransa, Australia, Ubelgiji, Canada, Uingereza, Uswisi, Ujerumani, Cyprus, New Zealand, Marekani, Urusi, Uturuki na Ukraine. Ziara hiyo iliratibiwa na kampuni za Savannah Tours Ltd kwa kushirikiana na Black Willow Safaris. Akizungumza wakati wa mapokezi ya watalii hao, Kamanda wa Hifadhi hiyo, Mhifadhi Mwandamizi Kelvin Stanslaus, alisema ujio wa wageni hao ni ishara njema kwa ukuaji wa utalii wa urithi nchini, hasa ikizingatiwa umuhimu wa Kilwa Kisiwani n...