Posts

Showing posts from March, 2026

WIZARA YA MADINI YAKUTANA NA UJUMBE WA WAWEKEZAJI KUTOKA CHINA KUJADILI FURSA ZA USHIRIKIANO SEKTA YA MADINI

Image
📍 Dodoma Wizara ya Madini imekutana na ujumbe wa wawekezaji kutoka Jamhuri ya Watu wa China unaotoka katika Kampuni ya Kimataifa ya Liaoning Fangda Group, kwa lengo la kujadili na kubaini maeneo ya kimkakati ya ushirikiano katika kuendeleza Sekta ya Madini nchini Tanzania. Ujumbe huo uliongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kampuni hiyo, Bw. Ao Xinhua, ambaye ameambatana na wataalamu mbalimbali kutoka Sekta za Viwanda, Madini na Teknolojia. Kikao hicho kilifanyika Machi 30, 2026 katika Ukumbi wa Tume ya Madini jijini Dodoma, kikiongozwa na Kamishna wa Madini, Dkt. AbdulRahman Mwanga. Katika majadiliano hayo, pande zote mbili zilijikita katika kuchambua fursa mbalimbali zilizopo katika mnyororo mzima wa thamani wa Sekta ya Madini, ikiwemo utafiti wa madini, uchimbaji, uongezaji thamani (beneficiation), pamoja na uwekezaji katika teknolojia za kisasa za uchakataji wa madini. Akizungumza wakati wa kikao hicho, Dkt. Mwanga alieleza kuwa Tanzania ina mazingira rafiki ya uwekezaji, sera thabiti n...

NAIBU WAZIRI WA NISHATI AKABIDHI VITENDEA KAZI KWA TANESCO MKOA WA SHINYANGA

Image
-Ni katika muendelezo wa mkakati wa shirika wa kuwahudumia wananchi kwa ufanisi -Awasihi wananchi kutumia nishati safi umeme kupikia Naibu Waziri wa Nishati Mh. Salome Makamba amekabidhi vitendea kazi vya usafiri kwa TANESCO Mkoa wa Shinyanga kwa lengo la kuimarisha utoaji wa huduma kwa wananchi na kutatua changamoto zao kwa haraka. Akizungumza leo tarehe 27, Machi 2026 wakati wa hafla ya kukakabidhi vitendea kazi hivyo iliyofanyika katika Manispaa ya Kahama Mkaoni Shinyaga Mhe. Salome amesema  hatua hiyo ya kukabidhi vitendea kazi hivyo ni kuyaishi maono ya Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha wananchi wanapata huduma za Umeme wa uhakika. Amesema vitendea kazi  hivyo vinakwenda kuongeza ufanisi katika utendaji kazi kwa watumishi wa TANESCO Mkoa wa Shinyanga na kuwawezesha kutatua changamoto za wateja kwa wakati.  “Kupitia vyombo hivi vya usafiri vitakwenda kuleta mabadiliko makubwa katika kumfikia mteja kwa haraka na kumhudumia, niwaombe mvitumie kutatua chan...

TANZANIA, ZAMBIA KUIMARISHA MIUNDOMBINU YA KIMKAKATI SEKTA YA MADINI

Image
Serikali za Tanzania na Zambia zimeazimia kuongeza kasi ya uboreshaji wa miundombinu ya usafirishaji wa madini ili kuchochea ukuaji wa sekta ya madini katika ukanda wa Kusini mwa Afrika.  Hatua hiyo ilisisitizwa Machi 25, 2026 na  Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa wakati wa  ufunguzi wa Mkutano wa 13 wa Kimataifa wa Madini na Nishati nchini Zambia (ZIMEC 2026) unaofanyika katika mji wa Kitwe. Dkt. Kiruswa alisema kuwa, mradi wa uboreshaji wa reli ya TAZARA itakuwa suluhisho la kudumu la kupunguza gharama za usafirishaji wa madini ya shaba na kobati kutoka Zambia kwenda soko la dunia kupitia Bandari ya Dar es Salaam nchini Tanzania. Dkt. Kiruswa alieleza kuwa,  kupitia maboresho ya reli ya TAZARA kutawezesha  usafirishaji wa madini ya shaba na kobati kwa wakati ikiwa pamoja na kufika sokoni kwa haraka na gharama nafuu. Awali, wakati akifungua mkutano  Waziri wa Migodi na Maendeleo ya Madini nchini Zambia , Mhe. Paul Kabuswe aliwataka wawekezaji...

LUKUVI AFARIKI DUNIA

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, anasikitika kutangaza kifo cha Mheshimiwa William Vangimembe Lukuvi (Mb.), aliyekuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu) na Mbunge wa Jimbo la Isimani, kilichotokea leo Machi 25, 2026, majira ya saa moja asubuhi katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, jijini Dodoma alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa mshtuko wa moyo. Mheshimiwa Rais anatoa pole kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, familia, wananchi wa Jimbo la Isimani, ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote kwa msiba huo.

TANESCO YAGUSA MIOYO YA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

Image
-Ni sehemu ya uwajibikaji wake kwa jamii  -Yatoa misaada mbalimbali kwa vituo vitatu Dar es Salaam. Katika kuendeleza dhamira ya uwajibikaji kwa jamii, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), tarehe 19 Machi 2026, lilifanya ziara ya kutembelea vituo vitatu vya watoto wenye mahitaji maalum jijini Dar es Salaam, na kutoa misaada mbalimbali kwa lengo la kuleta faraja na matumaini. Akizungumza wakati wa ziara hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji ,Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO, Bi. Irene Gowelle, alisema kuwa lengo la ziara hiyo ni kushirikiana na jamii kwa vitendo kwa kutoa misaada hususan kwa makundi ya watoto yenye uhitaji . Alieleza kuwa msaada huo haujalenga tu kukidhi mahitaji ya msingi, bali pia kuwajengea watoto hao imani, matumaini na ujasiri wa kuendelea kuamini katika ndoto zao licha ya changamoto wanazokabiliana nazo. “Leo TANESCO tumeshiriki na watoto hawa wenye mahitaji maalum kwa kutoa misaada mbalimbali, ikiwa ni sehemu ya kurejesha kwa ja...

TANESCO YAZINDUA NDEGE NYUKI (DRONES) KUBORESHA UKAGUZI WA MIUNDOMBINU YA UMEME NCHINI

Image
Shirika la Umeme Tanzania, TANESCO, limezindua rasmi matumizi ya ndege nyuki (drones) kwa ajili ya kufanya ukaguzi wa njia za kusafirisha na kusambaza umeme ikiwa ni hatua inayolenga kuongeza ufanisi wa utoaji huduma na kupunguza muda wa kutatua changamoto za kukatika kwa umeme. Uzinduzi huo umefanyika tarehe 17 Machi 2026 katika Ofisi za TANESCO, Ubungo jijini Dar es Salaam, ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo, Bw. Lazaro Twange. Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Bw. Twange amesema TANESCO inasimamia mtandao mkubwa wa miundombinu ya umeme nchini unaohitaji ufuatiliaji wa karibu kwa kutumia teknolojia za kisasa. “Tuna njia za kusafirisha umeme ambazo zimetembea urefu wa takribani kilomita 8,500, na tuna njia za kusambaza umeme ambazo zimetembea karibu kilomita 200,000. Njia hizi zimepita ardhini kwenye mapori, pembezoni mwa barabara na maeneo yetu,” amesema Bw. Twange. Ameeleza kuwa jukumu la msingi la Shirika hilo ni kuhakikisha wateja wanapunguziwa muda wa utatuzi wa ...

NAIBU WAZIRI UMMY ATOA MSUKUMO KWA WATUMISHI KUONGEZA UFANISI, AAGIZA UTEKELEZAJI THABITI WA BAJETI

Image
Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Mhe. Ummy Nderiananga, amewahimiza watumishi wa ofisi hiyo kuendelea kufanya kazi kwa bidii, ufanisi na weledi ili kuhakikisha malengo yaliyoainishwa katika bajeti ya Serikali yanatekelezwa ipasavyo. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Baraza la Wafanyakazi uliofanyika leo Jijini Dodoma, Mhe. Ummy—aliyemwakilisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu), Mhe. William Lukuvi—alisisitiza umuhimu wa watumishi kushirikiana na kuzingatia misingi ya uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku. Alifafanua kuwa mabaraza ya wafanyakazi yameanzishwa kufuatia Tamko Na. 1 la mwaka 1970 lililotolewa na Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, likiwa na lengo la kuongeza ufanisi na tija mahali pa kazi. “Kupitia mabaraza haya, wafanyakazi na waajiri hupata fursa ya kujadili na kubadilishana mawazo kwa manufaa ya taasisi. Ni matumaini yangu kuwa majadiliano yen...

SERIKALI KUIFANYA TANZANIA KITOVU CHA BIASHARA- DKT YONAZI

Image
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Uratibu na Wenye Ulemavu Dkt. Jim Yonazi amesema Serikali imefanya juhudi mbalimbali za Kisera, Sheria na Kimkakati ili kuhakikisha Tanzania inakuwa kitovu cha biashara Afrika Mashariki na Kati.   Dkt. Yonazi aliyasema hayo katika kikao  cha Kikundi Kazi cha Mazingira ya Biashara cha Baraza la Taifa la Biashara TNBC kilichofanyika jijini Dar es salaam.   Alisema Serikali imefanya jitihada za kukuza biashara nchini huku akizitaka sekta binafsi kuendelea kushirikiana na serikali.   “Serikali imefanya juhudi mbalimbali katika uwekezaji nchini ikiwemo mazingira ya ufanyaji wa biashara ya kisera, kisheria na lengo ni kuhakikisha Tanzania inakuwa kitovu cha biashara Afrika mashariki na kati. Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Dkt. Godwill Wanga  alisema kikao hicho kimefanyika ili kujadili maendeleo ya biashara nchini. Alisema kikao hicho kimejadili vivutio  ambavyo serikali inaweza ...

UWEKEZAJI WA SHILINGI BILIONI 50 KITUO CHA MPOMVU WAIMARISHA UPATIKANAJI WA UMEME KANDA YA ZIWA

Image
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imefanya ziara ya ukaguzi katika Kituo cha Kupokea na Kupoza Umeme cha Mpomvu kilichopo mkoani Geita tarehe 15 Machi 2026, ikiwa ni sehemu ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya Nishati inayolenga kuimarisha upatikanaji wa umeme nchini. Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Subira Mgallu amesema ziara hiyo imelenga kukagua maendeleo ya miradi ya nishati pamoja na kuhakikisha uwekezaji unaofanywa na Serikali unaleta matokeo yaliyokusudiwa kwa wananchi. “Kama Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini tuna jukumu la kuisimamia Wizara ya Nishati ili kuhakikisha inatekeleza majukumu yake kikamilifu. Tumeridhishwa na uwekezaji uliofanywa katika kituo hiki ambacho kina mchango mkubwa katika kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa wananchi na shughuli za kiuchumi,” amesema Mhe. Mgallu. Ameongeza kuwa Kituo hicho kina uwezo wa kupokea na kusambaza takribani megawati 90, huku jitihada zikiende...

KAMATI YA BUNGE NISHATI NA MADINI YASHANGAZWA NA TEKNOLOJIA YA KITUO CHA UCHENJUAJI DHAHABU KATENTE

Image
  Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wameonyesha kuridhishwa na kushangazwa na kasi ya teknolojia inayotumika katika Kituo cha Mfano cha Uchenjuaji Dhahabu cha Katente, kilichopo wilaya ya Bukombe, mkoani Geita. Hayo yamebainishwa leo Machi 15 , 2026 na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya  Nishati na Madini Subira Mgalu  wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua maendeleo ya kituo cha mfano cha Katente kilichoanzishwa na Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kikilenga kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini katika uchenjuaji bora  ili kuachana na matumizi ya kemikali hatarishi kama zebaki. Mgalu ameeleza kuwa , kamati imefurahishwa na  teknolojia ya uchenjuaji dhahabu  inayotumika Katente, inatumia mifumo ya kisasa ya Vat Leaching, imefanikiwa  kuongeza kiwango cha upatikanaji wa dhahabu kutoka asilimia 40 hadi kufikia zaidi ya asilimia 90. Pia, ameipongeza STAMICO kwa kurahisisha upatikanaji wa kemikali , na vil...

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI YAIPONGEZA TANESCO UTEKELEZAJI WA MRADI WA UMEME JUA KISHAPU

Image
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imelipongeza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa usimamizi na utekelezaji mzuri wa Mradi wa Uzalishaji Umeme kwa nguvu ya Jua wa Kishapu wenye uwezo wa Megawati 50 unaotekelezwa katika Mkoa wa Shinyanga. Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Subira Mgallu, mara baada ya Kamati kutembelea mradi huo tarehe 13 Machi, 2026 kwa lengo la kujionea maendeleo ya utekelezaji wake pamoja na ufanisi wa matumizi ya fedha zilizotolewa na Serikali. Akizungumza mara baada ya ziara hiyo, Mhe. Mgallu alisema mradi huo ni hatua muhimu katika mageuzi ya sekta ya nishati nchini kutokana na matumizi ya teknolojia ya nishati jadidifu. “Tumetembelea mradi huu wa uzalishaji wa umeme kwa kutumia teknolojia ya jua na tunaona ni mapinduzi makubwa katika sekta ya nishati nchini. Hii ni hatua muhimu kwani kwa mara ya kwanza Tanzania inapata Megawati 50 za umeme kutoka kwenye nishati ya jua,” alisema Mhe. Mgallu. Alisema Kamati imeridhishwa na n...