MAJUKWAA YA MAZUNGUMZO KUIMARISHA SEKTA YA MADINI
Makongamano na majukwaa yanayojadili mwenendo, changamoto na maendeleo ya sekta ya madini ni nguzo muhimu katika kuimarisha sekta hiyo na kuhakikisha inatoa mchango mkubwa zaidi katika maendeleo ya Taifa. Hayo yamebainishwa na Kaimu Kamishna wa Madini, Mhandisi Moses Kongola, kwa niaba ya Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, wakati akifunga kongamano la siku mbili lililoandaliwa na HakiRasilimali, lililojadili tafiti mbalimbali, maendeleo na nafasi ya Tanzania katika sekta ya madini mkakati. Mhandisi Kongola amesema majukwaa hayo ni muhimu kwa kuwa yanatoa fursa kwa Serikali, wadau wa sekta ya madini, watafiti, wachimbaji na jamii kujadili kwa pamoja namna ya kukabiliana na changamoto zilizopo na kutumia ipasavyo fursa zinazotokana na utajiri wa madini nchini. Amesema Serikali inaendelea kuweka mkazo katika uongezaji thamani madini nchini kabla ya kusafirishwa nje ya nchi, hatua ambayo itasaidia kuongeza mapato ya Serikali, ajira na fursa za kiuchumi kwa Watanzania. “Ni wajibu wa ki...