Posts

Showing posts from January, 2025

RC KENANI ATOA UFAFANUZI VIDEO INATOSAMBAZWA MITANDAONI KUHUSU SHULE YA BUDALA BUJIGA B

Image
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mheshimiwa Kenani Kihongosi ametolea Ufafanuzi taarifa iliyosambaa katika Mitandao ya kijamii kuhusu Shule ya Budala Bujiga B ambayo ilionyesha wanafunzi wanakaa chini. Mkuu wa mkoa ameeleza kuwa Video hio ni ya mwaka 2018 na Tangu alipoingia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Samia Suluhu Hassan madarasa katika Shule hio yalishajengwa pamoja na fedha za Madawati zilitoleea na kwasasa hakuna upungufu wa aina yoyote katika Shule hio. Mkuu wa Mkoa amesisitiza kuwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan imeendelea kuboresha miundombinu ya elimu kwa kujenga shule mpya Ikiwemo Simiyu Girls ambayo imeshakamilika na wanafunzi wanasoma. Pia ameeleza wamepokea fedha zaidi ya bilion 4 za ujenzi wa Shule mpya ya Wavulana ambayo inajengwa Katika Wilaya ya Bariadi,pia ujenzi wa Shule katika kata unaendelea kwa kasi kubwa. Hivyo amewaeleza wananchi kuzidi kushirikiana na serikali katika kuleta maendeleo na amewaasa wananchi Habari...

DKT. KAZUNGU AKAGUA VITUO VYA UMEME HALE, PANGANI NA NYUMBA YA MUNGU, lengo ni kuhakikisha vinafanya kazi kwa ufanisi

Image
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Khatibu Kazungu, amemtaka Mkandarasi   anayekarabati mitambo katika kituo cha kufua umeme Hale kufanya kazi kulingana na makubaliano ya kimkataba ili kituo hicho kiweze kuingiza umeme wa kutosha kwenye gridi ya Taifa. Dkt. Kazungu ametoa agizo hilo wakati wa ziara yake ya ukaguzi wa mitambo ya kufua umeme katika kituo cha Hale-Tanga, Nyumba ya Mungu- Moshi na New Pangani Falls ambapo  ameisisitiza TANESCO kumsimamia ipasavyo mkandarasi. "Lengo la ziara hii ni kukagua maendeleo ya Miradi hii ya umeme  na kujionea hatua za ukarabati unaofanyika na nimemuagiza mkandarasi anayefanya ukarabati kufuata sheria na kanuni za mkataba ili kukamilisha kazi lakini pia ni lazima asimamiwe ili amalize kazi kwa wakati na kwa ufanisi." Amesema Kazungu   Meneja wa Vituo hivyo vya Kuzalisha umeme kwa njia ya maji,  Mhandisi Kulwa Byemelo amesema "hali ya mitambo ya  kuzalisha umeme ni nzuri katika kituo cha Nyumba ya Mungu amb...

GATES FOUNDATION YAIPONGEZA TANZANIA UBORESHAJI AFYA YA MSINGI NA KUPUNGUZA VIFO VYA KINA MAMA NA WATOTO

Image
  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepongezwa kutokana na jitihada madhubuti za kuimarisha afya ya msingi na kupunguza idadi ya vifo vya kina mama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano. Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Gates Foundation Barani Afrika, Dkt. Paulin Basinga alipotembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambapo alipata fursa ya kuona jinsi inavyotoa mchango wake kwa Serikali kuimarisha upatikanaji huduma ngazi ya afya ya msingi, hospitali za rufaa za mikoa hadi Kanda na hatimaye kupunguza rufaa za wagonjwa kufika hospitalini hapo ikiwemo kupunguza rufaa za wagonjwa kwenda nje ya nchi. Dkt. Basinga amesema taasisi anayoiongoza imefanya kazi na Serikali ya Tanzania katika maeneo ya uboreshaji programu za kilimo, masuala ya fedha kwa ujumla wake, sekta ya afya hususani kufanya tafiti zilizoibua afua mbalimbali za kupunguza vifo vya kina mama wajawazito na watoto chini ya umri wa miaka mitano. Katika hatua nyingine, Dkt. Basinga ameipongeza M...

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO

Image
  Comments

KUUNGANISHA UMEME MAENEO YA VIJIJI NI ELFU 27 – KAPINGA

Image
  Naibu Waziri wa Nishati, Mhe Judith Kapinga kwa niaba ya Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko  amesema uunganishaji wa umeme kwenye maeneo ya Vijiji ni shilingi 27,000/- na maeneo ya Vijiji mji ni shilingi 320.960/-. Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Januari 30, 2024 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la la Mbunge wa Bukene, Mhe. Selemani Zedi aliyetaka kufahamu kwa nini maeneo ya Bukene na Itobo hayaunganishiwi umeme kwa gharama ya Shilingi 27,000/-. "Mheshimiwa Spika maeneo ya Bukene na Itobo ni Vijiji Mji ambapo gharama ya kuunganisha umeme maeneo ya Vijiji Mji ni shilingi 360.960," Amesisitiza Mhe. Kapinga Ameongeza kuwa Serikali inaendelea kuangalia kama kuna uwezekano wa kufanya maboresho kulingana na tathmini amabayo imefanyika.  Aidha, Mhe. Kapinga amesema tayari amemuagiza Meneja wa Mkoa wa Tabora na wa Wilaya ya Nzega kufanya tathmini ya kina ili yaweze kupatikana majibu ya kina iwapo maeneo ya Bukene na Itobo ili kuweza kuondoa ...

TANZANIA,SOMALIA WASAINI MKATABA WA KUBADILISHANA WAFUNGWA

Image
Serikali ya Tanzania na Jamhuri ya Shirikisho la Somalia zimesaini mikataba miwili ya makubaliano ya kushirikiana na katika masuala ya Ulinzi na Usalama pamoja na kubadilishana Wafungwa. Mikataba hiyo imesainiwa Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Somalia, Balozi Ahmed Moalim Fiqi Somalia. Akizungumza baada ya kusaini mikataba hiyo, Waziri Bashungwa amesema Mkataba wa kubadilishana Wafungwa utaziwezesha nchi hizo mbili kuruhusu ubadilishanaji wa wafungwa ili waweze kutumikia adhabu katika nchi zao na kusaidia kupunguza gharama za kifedha za kuwahudumia wafungwa. “Inapotokea kuna Watanzania wenzetu wameingia katika hali ya kuwa wafungwa wakiwa kule Somalia, kupitia mkataba tuliosaini utatuwezesha kuwachukuwa Watanzania kuwaleta kwenye magereza yetu, vile vile kwa wafungwa wa Somalia watarudishwa kuendelea na vifungo vyao nchini kwao,” ameeleza. Aidha, Bashungwa amesema mkataba wa ush...

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO

Image
   

TANZANIA YAAHIDI KUENDELEZA USHIRIANO NA BURUNDI SEKTA YA NISHATI

Image
Serikali imeahidi kuendelea kushirikiana na nchi ya Burundi katika nyanja mbalimbali za maendeleo ikiwemo sekta ya nishati.  Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko katika mazungumzo yake na Waziri wa Nishati na Madini wa Burundi, Mhe Ibrahim Uwizeye aliyemtembelea ofisini kwake jijini Dar es Salaam.  "Rais Samia ni kinara katika kujenga mahusiano na ndani ya nchi na kimataifa, kama ilivyo kwa uhusiano kati yetu na Burundi ambayo  imewezesha kutekeleza miradi kadhaa ukiwemo mradi wa umeme wa RUSUMO unaoendeshwa kwa ubia wa nchi Tatu za Rwanda, Burundi na Tanzania" Amesema Dkt. Biteko.  Ameongeza kuwa, Tanzania itaendelea kuimarisha ushirikiano na Burundi na kuwataka kuimarisha mahusiano kwa wafanyabiashara ili kuondoa migogoro inayoweza kujitokeza na kusababisha usumbufu kwa wananchi.  Kwa upande wake, Waziri wa Nishati na Madini wa Burundi, Mhe. Uwizeye amemshukuru Rais Samia kwa utayari wa kuisaidia nchi hiyo katika ...

AFRIKA KUUNGANISHA NGUVU USAMBAZAJI UMEME

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema nchi za Afrika zinapaswa kuunganisha nguvu katika kuhakikisha wananchi wake wanafikiwa na nishati ya umeme ili kuchochea ukuaji wa uchumi. Akihutubia wakati wa mkutano wa wakuu wa nchi za Afrika kuhusu nishati unaoendelea jijini Dar es Salaam, Rais Samia amesema Tanzania imepiga hatua kwa kusambaza umeme katika vijiji vyote na sasa inaweka mkazo katika kufikisha nishati hiyo ngazi ya vitongoji. "'Mpaka sasa tumefanikiwa kuunganisha umeme katika vijiji vyote 12,318 na vitongoji 32,827 kazi inayoendelea ni kuunganisha umeme kwenye vitongoji 31,532 vilivyobakia kabla ya mwaka 2030" Rais Samia amesema kupitia mpango wa nishati Tanzania inafanya kazi ya kuongeza uzalishaji na uimarishaji wa miundombinu ya usambazaji wa umeme akiongeza kuwa nchi za Afrika lazima ziunganishe nguvu za wadau kwa lengo la kuwafikishia nishati ya umeme wananchi milioni 300 kufikia 2030. Aidha, amesema Tanzania inatekeleza ...

BASHUNGWA ALIPONGEZA JESHI LA POLISI ULINZI MKUTANO WA NISHATI

Image
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa   amepita baadhi ya maeneo Jiji la Dar es Salaam kujionea namna Jeshi la Polisi na Vyombo vingine vya Usalama wanavyotekeleza majukumu yao wakati Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati ukiendelea katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere. Bashungwa wakati akipita katika maeneo ya Jiji hilo, leo tarehe 28 Januari 2025, amempongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP. Camillus Wambura kwa kuendelea kushirikiana na Vyombo vingine vya Serikali kuimarisha usalama katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati, unaofanyika tarehe 27 na 28 Januari 2025.  “Watanzania wameona nchini yetu ipo imara, tunamshukuru Rais na Amri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyoendelea kuwezesha Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kuwa timamu muda wote kwa kukabiliana na jambo lolote na lenye ukubwa wowote” amesema Bashungwa. Bashungwa ameeleza kuwa Serikali inajivunia kazi nzuri inayoende...

UKOSEFU WA UMEME HUPUNGUZA PATO LA TAIFA-AFDB

Image
  Ukosekanaji wa umeme wa kutosha hupunguza pato la Taifa (GDP) kwa asilimia 2 hadi 4 kwa kila mwaka.Upatikanaji wa umeme ni muhimu kwa ukuaji wa uchumi wa Afrika. Hayo yameelezwa na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB) Dkt.Akinumwi Adesia wakati akizungumza katika Mkutano wa Nishati wa wakuu wa nchi za Afrika unaoendelea jijini Dar es salaam. “Sasa ni wakati wa kuchukua hatua madhubuti ndio maana mimi pamoja na Ajay Banga Rais wa Benki ya Dunia tulishirikiana kuzindua M300 lengo likuwa ni kuhakikisha upatikanaji wa umeme kwa watu milioni 300 ifikapo 2030” Aidha ameeleza kuwa Mission 300 imekuwa ni harakati ya kitaifa hivyo tukiungwa mkono na tume ya umoja wa Afrika na washirika mbalimbali wa kimataifa wakiwemo Rockefeller foundation, Sustainable energy for All ya umoja wa mataifa na Global Alliance energy for people and the planet ili kuharakisha matumizi ya Nishati safi. Hatuko peke yetu katika kufanikisha mradi huu tumeungwa mkono na Benki ya Maendeleo ya Kiislamu , Benki...

PICHA: KUTOKA MKUTANO WA NISHATI WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKA 2025

Image
  Matukio Kutoka Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Julius Nyerere (JNICC) ambapo Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika 2025 (Mission 300) unaendelea, mkutano huo unalenga kuwapelekea umeme waafrika milioni 300 katika nchi za Afrika.

DKT. BITEKO AWAPA POLE BUKOMBE KUFUATIA AJALI YA RADI

Image
  Mbunge wa Jimbo la Bukombe ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ametoa pole kwa wananchi wa Wilaya ya Bukombe mkoani Geita kufuatia ajali ya radi iliyotokea leo Januari 27, 2025 katika Kata ya Ushirombo. Sehemu ya taarifa hiyo salamu za pole ya Dkt. Biteko iliyotolewa leo Januari 27, 2025 inaeleza kuwa ajali hiyo ya radi imesababisha vifo vya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Businda. “ Nimepokea taarifa ya vifo vya watoto wetu wa Businda Sekondari kwa masikitiko makubwa. Naomba kuwapa pole sana wazazi, walezi, walimu, wanafunzi wa shule hii na ndugu wote waliguswa na msiba huu mkubwa,” amesema Dkt. Biteko. Ameendelea “Vifo vya vijana wetu vimetushtua sana wana Bukombe wote. Tunawaombea faraja familia zote zilizofikwa na msiba huu aidha, tunawaombea uponyaji wa haraka majeruhi wote kwenye kadhia hii.” Aidha, Dkt. Biteko ameelekeza Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri na Ofisi ya Mbunge kufuatilia kwa karibu matibabu ya...

DK.BITEKO AFUNGUA MKUTANO WA NISHATI WAKUU WA NCHI AFRIKA,AHIMIZA MSHIKAMANO

Image
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, ameongoza juhudi mpya za kikanda kwa kuhimiza mshikamano wa nchi za Afrika katika kuhakikisha upatikanaji wa nishati endelevu na nafuu kwa kila mwananchi ifikapo mwaka 2030. Akizungumza leo Januari 27, 2025, wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Nishati wa Nchi za Afrika jijini Dar es Salaam, Dkt. Biteko alibainisha kuwa mkutano huu ni fursa muhimu kwa bara la Afrika kuimarisha mikakati ya kuongeza upatikanaji wa umeme na matumizi ya nishati safi. “Tuna jukumu la pamoja kuhakikisha tunafanikisha lengo la kuwafikishia umeme wa uhakika watu milioni 300 katika ukanda wa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara ifikapo mwaka 2030,” alisema Dkt. Biteko. Aliendelea kusisitiza kuwa uwekezaji mkubwa katika sekta ya nishati ni nguzo muhimu kwa maendeleo ya viwanda, sekta ya madini, na huduma za kijamii, akihimiza nchi za Afrika kuongeza juhudi katika kuboresha miundombinu ya nishati. Dkt. Biteko pia aliweka msisitizo juu ya matumizi ya nishati...

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA MKUTANO WA NISHATI WA WAKUU WA NCHI ZA AFRIKAUMEHUSISHA MAWAZIRI WA NISHATI NA FEDHA BARANI AFRIKA NA MARAIS WA BENKI YA DUNIA NA BENKI YA MAENDELEO AFRIKA

Image
   AMBAO LEO TAREHE 27.1.2025 

NAIBU WAZIRI WA ESWATINI AWASILI

Image
  Naibu Waziri Mkuu wa Ufalme wa Eswatini, Mheshimiwa Thulisile Dladla, amewasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati, unaotarajiwa kufanyika tarehe 27 hadi 28 Januari 2025. Katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Mheshimiwa Dladla amelakiwa na Waziri wa Madini Mheshimiwa Anthony Mavunde. Mkutano wa Kilele wa Wakuu wa Nchi unalenga kuimarisha juhudi za pamoja katika kukabiliana na changamoto za nishati barani Afrika, sambamba na kupitisha Azimio la Dar es Salaam, linalosisitiza dhamira ya Viongozi wa Nchi na Serikali za Afrika kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika, nafuu, na endelevu barani Afrika