WAPIGA KURA 222,218 KUPIGA KURA JIMBO LA ISMANI NA KATA 12 TANZANIA BARA
NA MWANDISHI WETU, IRINGA WAPIGA Kura 222,218 walioandikishwa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura watashiriki kwenye uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Isimani lililopo Halamashauri ya Wilaya ya Iringa Mkoani Iringa na Kata 12 za Tanzania Bara. Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufaa Mhe. Jacobs Mwambegele ameyasema hayo leo Mei 31, 2026 Mkoani Iringa wakati akisoma risala maalum kuhusu uchaguzi katika jimbo na kata husika utakao fanyika kesho Juni 01, 2026 na kusema kuwa jumla ya vituo 628 vya Kupigia Kura vitatumika. “wapiga kura 89,753 wapo kwenye Jimbo la Ismani na wapiga kura 132,465 wapo kwenye kata 12 zitakazofanya uchaguzi mdogo na vituo 277 vipo kwenye Jimbo la Ismani na vituo 351 vipo kwenye kata 12 zitakazofanya uchaguzi mdogo.,”amesema Jaji Mwambegele. Aidha, amesema Katika Uchaguzi huu, jumla ya wagombea 108 kutoka katika vyama vya siasa 17 wanawania nafasi wazi ya ubunge na udiwani katika maeneo niliyoyataja. “Jimbo la Ism...