Posts

Showing posts from December, 2024

NAIBU WAZIRI NDERIANANGA ASHIRIKI DUA YA KUMUOMBEA MAREHEMU MHE. JAJI MWANAISHA KWARIKO

Image
Mh.Ummy Nderiananga NA. MWANDISHI WETU – DAR ES SALAAM Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Ummy Nderiananga ameshiriki dua maalum ya kumuombea marehemu Mheshimiwa Mwanaisha Athumani Kwariko, Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mjumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (INEC) Tarehe 29 Disemba, 2024 nyumbani kwake Masaki Jijini Dar es Salaam. Dua hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo, Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Profesa Ibrahim Juma, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila, Naibu Katibu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. James Henry Kilabuko, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) Mhe. Jaji George Kazi pamoja na baadhi ya wajumbe wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania akiwemo, Mhe. Asina Omari na Mhe. Balozi Omary Mapuri. Akitoa salamu wakati wa dua hiyo Jaji Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Profesa Ibrahim Juma ametoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wote waliofikwa na ms...

CUF YAMTAKA DKT.SAMIA KUSISITIZA UHURU NA HAKI UCHAGUZI MKUU 2025

Image
  Na Mwandishi Wetu. Chama Cha Wananchi( CUF) kimemtaka Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha uchaguzi mkuu unaofanyika Mwaka 2025 uwe wa  uhuru nawa haki ili kuendelea kulinda na kukuza Demokrasia Nchini. Hatua hiyo ya CUF imetokana na kile ilichodai kuwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2024 ulikua hauna uhuru na  haki kwa wagombea wa vyama vya upinzani kutokana na Demokrasia kusiginwa na TAMISEMI iliyopewa jukumu la kusimamia uchaguzi huo. Taarifa hiyo imetolewa  leo Desemba 29,2024 Jijini Dar es salaam na Mwenyekiti CUF Taifa Profesa Ibrahim Lipumba wakati akizungumza na Waandishi wa habari kwa ajili ya kutoa tathmini ya baadhi ya mambo yaliyofanyika mwaka 2024 ikiwemo uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambao amesema kuwa ulikua na dosari kubwa na kuharibu Demokrasia kwa ujumla. Prof.Lipumba amesema kuwa uchaguzi Mkuu wa Madiwani,Wabunge na Rais utakaofanyika mwishoni mwa mwaka 2025 unapaswa kusimamiwa na tume huru ya Taifa ya uchaguzi( INEC) na sio TAMISEMI...

SOKO LA MACHINGA COMPLEX BIASHARA SASA NI SAA 24

Image
  Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam imeanza kutekeleza agizo la Waziri Mkuu mheshimiwa Kassim Majaliwa alilolitoa wakati wa ziara yake mkoani Dar es salaam ya kuhakikisha mitaa na maeneo muhimu yote yanafungwa taa za mtaani kuwezesha biashara kufanyika nyakati zote. Mkuu wa wilaya ya Ilala Mhe. Edward Mpogolo Disemba 28,2024 alizindua taa 21 zenye thamani ya Shilingi milioni 63,700,000 kwenye soko maarufu la "Machinga Complex" ili kuwezesha biashara katika eneo kufanyika saa 24. "Na hili niliweke wazi, kuanzia leo baada ya uzinduzi wa taa hizi hakuna kupoteza muda,biashara sasa katika Soko hili ni saa 24. jambo la kufurahisha tuna kituo cha Polisi kilichopo katika eneo hili ambapo ulinzi utaimarishwa zaidi".Alisema Mkuu huyo wa Wilaya. Aidha amesema mbali na taa hizo katika Soko la Machinga,Serikali pia imefunga taa 33 zenye thamani ya Shilingi milioni 136,290,000 kuzunguka soko la Kariakoo huku kamera za usalama zikifungwa pia katika Soko hilo la Kimataifa. Baad...

MV SERENGETI YAPINDUKA SIKU TATU BAADA YA KUFANYIWA UKAGUZI

Image
  Mwanza  - Kampuni ya Meli Tanzania (TASHICO) imetoa taarifa kwa umma kuhusu tukio la kupinduka kwa meli ya Mv. Serengeti lililotokea usiku wa kuamkia Desemba 26 mwaka huu katika Bandari ya Mwanza Kusini. Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Mwanza, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo Paul Sebukoto amesema kuwa Meli hiyo imelalia upande wa nyuma baada ya maji kuingia ndani. ‘’Meli hii ilikuwa kwenye eneo la Maegesho, Maji yameingia ndani zikiwa zimepita kama siku mbili au tatu baada ya kufanyiwa ukaguzi uliobaini iko sawa, kwa hiyo ni lazima kutakuwa na chanzo ambacho kimesababisha maji kuingia ndani ya meli na kuipeleka chini upande wa nyuma’’ alisema Sebukoto na Kuongeza kuwa ‘’Sasa tofauti na Tafsiri kuwa meli imepinduka au imezama ni kwamba meli hii haijapinduka wala haijazama isipokuwa tunasema imeegemea upande wa nyuma baada ya kulemewa na maji yaliyoingia ndani’’ Sebukoto amesema kuwa shughuli zinazofanyika kwa sasa ni kuinyanyua Meli hiyo kwa nyuma ili iwez...

TUSHEREHEKEE KRISMASI,MWAKA MPYA TUKIJIVUNIA MABADILIKO MAKUBWA SEKTA YA NISHATI

Image
Katika kusherehekea SIkukuu za Krismasi na Mwaka Mpya 2025, Watanzania hatuna budi kujivunia safari ya mafanikio katika Sekta ya Nishati, hususan umeme. Je Unajua kabla ya kupata Uhuru mwaka 1961 Nchi ilizalisha umeme kwa kutumia mafuta ambapo kila mkoa ulijitegemea na hapakuwepo na mfumo wa gridi ya Taifa? Safari ya Mabadiliko (yaani Journey of Transformation) ilianza mwaka 1967 kwa ujenzi wa kituo cha kuzalishaji umeme cha Hale megawati chenye uwezo wa megawati 21 pamoja na ujenzi wa njia ya umeme kutoka Hale hadi Dar es Salaam na hivyo kuanza kwa mfumo wa gridi ya Taifa. Kutokana na nishati ya umeme kuwa ndio kichocheo cha ukuaji wa uchumi, utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umeme iliendelea ambapo mwaka 1968 ulifanyika ujenzi wa kituo cha kuzalisha umeme cha Nyumba ya Mungu cha megawati 8, mwaka 1975 kikajengwa Kituo cha Kidatu cha megawati 204 pamoja na ujenzi wa njia ya umeme ya Kidatu – Morogoro – Dar es Salaam. Safari ya Mabadiliko iliendelea kufanyika kupitia Viongozi Wakuu w...

RC CHALAMILA AWEKA WAZI MIKAKATI YA JIJI LA DAR 2025

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila. Muonekano katika picha wa Jijini la Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila katika salamu zake za Christmas amesema Jiji la Dar es Salaam linatarajia kuanzisha mfumo wa ufanyaji biashara kwa saa 24 kwa mara ya kwanza, hatua inayolenga kuboresha uchumi na kuwa kitovu cha biashara ndani na nje ya nchi. Hayo amesema leo wakati akitoa taarifa ya mwisho wa mwaka ya mkoa wa Dar es salaam pamoja na salamu za Siku ya Christmas na mwaka mpaya ambapo amesema huduma hiyo itazinduliwa rasmi Januari 2025 katika eneo la Kariakoo, kabla ya kusambazwa katika maeneo mengine yatakayobainishwa na viongozi wa wilaya na halmashauri.

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO

Image
 

ZAIDI YA MIL. 17 KUTUMIKA KULIPA KIFUTA JASHO NKASI

Image
SERIKALI imekamilisha mchakato wa kufanya tathmini ya malipo ya kifuta jasho kwa wananchi 27 wa wilaya ya Nkasi Mkoani Rukwa ambao mazao yao yaliathiriwa na  wanyamapori wakali na waharibifu katika kipindi cha mwaka 2022 mpaka 2024 Kauli hiyo imetolewa Desemba 22, 2024 na Ofisa  Wanyamapori Wilaya ya Nkasi   Anorld Ngagashi akiongea na wananchi wakati wa ziara ya mafunzo ya mbinu za kukabaliana na wanyamapori wakali na waharibifu hususani tembo, ziara iliyofanywa na TAWA wilayani humo. "Kwa sasa wananchi wa wilaya ya Nkasi suala la kifuta jasho lipo asilimia 98, kuna wananchi 27 wanakwenda kulipwa hivi karibuni shil Mil. 17, 750,000 amesema Anorld Ngagashi Anorld amesema mpaka sasa wananchi watatu kutoka Kata ya Kabwe (2) na Wampembe (1) wameshalipwa jumla ya shilingi mil 3, malipo yaliyofanyika Desemba 20, 2024  na kusisitiza kuwa wananchi 24 waliosalia malipo yao yatakamilika muda wowote kuanzia sasa. Aidha Afisa huyo amepongeza ushirikiano mkubwa wanaoupata k...

GRIDI ZA TANZANIA,KENYA KUIMARISHA UPATIKANAJI WA UMEME NCHINI - MHA. GISSIMA NYAMO-HANGA

Image
  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO) Mha. Gissima Nyamo-Hanga amesema kuimarika kwa mfumo wa Gridi za Umeme za Tanzania na Kenya kutasaidia kuimarisha upatikanaji wa umeme katika ukanda wa Kaskazini Mashariki mwa Afrika  . Mha.Gissima ameyasema hayo Desemba 20,2024 wakati wa Ziara yake akiongozana na Viongozi wengine wa Shirika katika kituo cha kupokea, kupoza na kusafirisha umeme cha Lemuguru kilichopo Mkoani Arusha.  "Niwahimize  wataalamu mnaosimamia mfumo wa Gridi mnapoendelea na zoezi la kuunganisha mifumo ya Gridi za Tanzania na Kenya kuhakikisha zoezi hilo haliathiri upatikanaji wa umeme kwenye Mfumo wa Gridi yetu nchini ". Alisisitiza Mha Gissima. Mha. Gissima amesema kituo hicho cha Lemuguru ni muhimu kutokana na kuunganisha mfumo wa Gridi ya Taifa na mifumo mingine ya Gridi ya nchi za ukanda wa Kaskazini Mashariki mwa Afrika( EAPP ).  Muunganiko huu kikanda wa Eastern African Power pool  una jumla ya Nchi wanachama 13. Mba...

DKT. KAZUNGU ATEMBELEA MIRADI YA UMEME DAR ES SALAAM

Image
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. Khatibu Kazungu ametembelea miradi mbalimbali ya uzalishaji na usafirishaji umeme inayoendelea kwa lengo la kufahamu utekelezaji wa miradi hiyo na maendeleo yake leo tarehe 21 Desemba, 2024 jijini Dar es Salaam. Pamoja na kukagua miradi hiyo ya umeme inayoendelea, Dkt. Kazungu ametembelea vituo mbalimbali vya umeme kwa lengo la kuhakikisha kuwa vinafanya kazi ipasavyo na hivyo kuendelea kutoa uhakika wa uwepo wa umeme wa kutosha nchini. Aidha, katika ziara hiyo Dkt. Kazungu amekagua mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi asilia ya Ubungo I, II na III, na amekagua maendeleo ya ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Kimara – Ubungo – Mabibo hadi Ilala pamoja na kukagua maendeleo ya ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Mabibo. Katika hatua nyingine, ametembelea kituo cha kupoza umeme cha Kinyerezi I, II na Kinyerezi I Extension pamoja na kukagua maendeleo ya ufungaji wa Transfoma ya ukubwa wa 175MVA katika kituo hicho. Vilevile, ...

TANZANIA, SAUDI ARABIA KUIMARISHA USHIRIKIANO SEKTA YA NISHATI

Image
  Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na Saudi Arabia katika kuimarisha Sekta ya Nishati hususan katika Mafuta na Gesi, Nishati Safi ya Kupikia na Nishati Jadidifu. Mhe. Kapinga amesema hayo wakati alipokutana na Naibu Waziri wa Nishati wa  Saudi Arabia,          Mhandisi Mohammed  Albrahim katika Mji wa Riyadh tarehe 19 Desemba, 2024 nchini Saudi Arabia. Amesema kuwa, Tanzania imekuwa ikishirikiana na nchi hiyo kwa muda mrefu katika Biashara ya Mafuta na Maeneo Mengine ya Maendeleo hivyo mahusiano hayo yanaendelea kuimarika zaidi kwa kuwa mahitaji ya nishati yanazidi kuongezeka   na uwekezaji zaidi unahitajika katika kuendeleza Sekta ya Nishati ikiwemo Mafuta na Gesi Asilia, Nishati Jadidifu na  Nishati Safi ya Kupikia. "Mahusiano ya Tanzania na Saudi Arabia katika Sekta ya Nishati ni ya muda mrefu, nchi hizi mbili zimekuwa na lengo la kuboresha ushirikiano wao katika kuendeleza sek...

SERIKALI YAKABIDHI NYUMBA 109 KWA WAATHIRIKA WA MAAFA HANANG

Image
 NA MWANDISHI WETU  WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa leo (Ijumaa, Desemba 20, 2024) amekabidhi nyumba 109 kwa waathirika wa maafa ya maporomoko ya tope yaliyotokea Desemba, mwaka jana wilayani Hanang, mkoani Manyara. Akizungumza mara baada ya kukabidhi na kuzindua nyumba hizo zilizojengwa katika kitongoji cha Waret, Wilaya ya Hanang, mkoani Manyara, Waziri Mkuu amesema kuwa Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anawapa pole waathirika wote na amesisitiza kuwa Serikali itawasaidia ili waendelee na maisha yao kama ilivyokuwa awali.  Amesema kuwa ujenzi wa nyumba 73 kati ya 109 umegharamiwa na Serikali Kuu na kujengwa na Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA-JKT); nyumba nyingine 35 zimejengwa na Shirika la Msalaba Mwekundu Tanzania, ilhali nyumba moja imejengwa na Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi Taifa (UWT). “Kufuatia maafa hayo, nyumba 109 zilihitaji kujengwa upya kwa haraka. Hivyo, kwa kuzingatia athari hizo, na kwa upendo wake, Mheshimiwa Rais...

MRADI WA KUFUA UMEME BWAWA LA JULIUS NYERERE MBIONI KUKAMILIKA

Image
  Uongozi wa Shirika la Umeme Tanzania ( TANESCO) Desemba 19, 2024 umetembelea Mradi wa Kufua umeme wa Bwawa la Julius Nyerere kujionea kasi ya maendeleo ya ujenzi unavyoendelea na kuweka mkazo kwa wasimamizi kuhakikisha usimikaji wa mashine nne zilizobakia unafanyika ipasavyo ili umeme utakapozalishwa uingizwe kwenye Gridi ya Taifa kwa mafanikio  yatakayoleta tija inayotarajiwa kwa watumiaji wa umeme. Akizungumza wakati wa Ziara hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Mha. Gissima Nyamo-Hanga amesema kwasasa jumla ya mashine tano (05) zimekamilika kwa asilimia 100 yaani mashine namba 9, 8, 7, 6 na 5 na tayari zimeanza uzalishaji wa umeme.  " Tumetembelea mradi huu kujionea shughuli zinazoendelea na kuweka msisitizo wa usimamizi bora kwa maeneo ambayo bado hayajakamilika ambapo utekelezaji kwa ujumla umefikia asilimia 99.55 huku shughuli za uzalishaji wa umeme zikiwa zimeanza na wastani wa megawati 1175 zinazozalishwa  kutoka mashine tano za mradi huu zimeingizwa kw...