DKT.KAZUNGU AFANYA MAZUNGUMZO NA TAASISI YA AEE INTEC YA AUSTRIA
Naibu katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Khatibu Kazungu amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Teknolojia Endelevu ya Nishati (AEE INTEC) ya nchini Austria, Bw. Christopher Brunner ambaye ameeleza nia ya kampuni hiyo kuwekeza katika teknolojia mpya ya Joto la Jua (Solar thermal) inayotumika katka kuchemsha maji yanayoweza kutumika katika Shule, Hospitali, Vyuo, Viwanda na Masoko ambayo inawezesha kupunguza matumizi ya umeme. Mazungumzo hayo yamefanyika jijini Gaborone nchini Botswana ambapo Dkt Kazungu anaongoza Ujumbe wa Tanzania kushiriki Wiki ya Nishati Endelevu kwa Nchi za Jumuiya ya Kusini mwa Afrika (SADC). “Tanzania tuna rasilimali ya kutosha ya Jua ambayo inaweza kutumika kwa shughuli mbalimbali za kijamii na kiuchumi. tunahitaji teknolojia rahisi za kisasa na za gharama nafuu katika kuendeleza nishati ya Jua.” Amesema Kazungu Katika kuhakikisha Tanzania inanufaika na programu hiyo kupitia Jumuiya ya Nchi za Kusini m...