MADINI YA YODERITE YATAKIWA KUHIFADHIWA KWA MANUFAA YA VIZAZI VIJAVYO
📍Dodoma – Kongwa Imeelezwa kuwa kuna umuhimu wa kuchukua hatua madhubuti za kuhifadhi na kulinda madini adimu aina ya Yoderite yanayopatikana katika eneo la Mlima wa Mautia, Wilaya ya Kongwa, Mkoa wa Dodoma, ili kuhakikisha urithi huo wa kipekee wa kijiolojia unabaki salama kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo. Hayo yalisemwa Juni 30, 2026 na Meneja wa Jiolojia kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), Solomon Maswi, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea eneo hilo kwa ziara maalumu. Maswi alisema kuwa uhifadhi wa Yoderite unaweza kuiwezesha Tanzania kuwa kitovu cha kimataifa cha tafiti kuhusu madini adimu, sambamba na kuongeza idadi ya watalii wanaotembelea maeneo yenye urithi wa jiolojia. Aliongeza kuwa Yoderite ni miongoni mwa madini adimu yanayoifanya Tanzania kutambulika duniani kutokana na historia yake ya kugunduliwa kwa mara ya kwanza katika Mlima wa Mautia. Aidha, alifafanua kuwa madini hayo yana mchango mkubwa katika tafit...