Posts

Showing posts from May, 2025

DKT. NCHEMBA AWAKARIBISHA WAWEKEZAJI MRADI WA SGR

Image
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ameishukuru Benki ya Maendeleo ya Afrika Kusini (DBSA), kwa kushiriki katika ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR), mradi ambao ni muhimu kwa uchumi wa Tanzania na nchi jirani zitakazonufaika na mnyororo wa thamani wa mradi huo wa kikanda. Mhe. Dkt. Nchemba amesema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Bi. Buitumelo Mosako, kando ya Mikutano ya Mwaka ya Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) iliyofanyika, Abidjan nchini Ivory Coast. “Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa Benki ya Maendeleo ya Afrika Kusini (DBSA) kwa mchango wenu muhimu katika kufadhili ujenzi wa SGR kipande cha 3 na 4 (Makutupora hadi Isaka) kwa kiasi cha dola za Marekani milioni 100. Zaidi ya hapo, tunatambua na kuthamini msaada wa kifedha wa kiasi cha dola milioni 100 uliotolewa awali kwa ajili ya kujenga kipande cha 2, ambao uliweka msingi imara kwa mradi mzima wa SGR” alisema Dkt. Nchemba Alisema kuwa kuto...

TANZANIA,JAPAN ZATIA SAINI HATI YA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO UWEKEZAJI BIASHARA YA KABONI

Image
              TOKYO JAPAN SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Japan zimetia saini Hati ya Makubaliano ya ushirikiano katika mpango wa pamoja wa uwekezaji katika Biashara ya Kaboni utakaowezesha kampuni za nchi hizo mbili kuwekeza katika Biashara ya Kaboni nchini Tanzania. Utiaji saini wa makubaliano hayo umefanyika Mei 28, 2025  Tokyo, Japan kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ikiongozwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni na Serikali ya Japan ikiongozwa na Waziri wa Mazingira, Mhe. Asao Keiichiro (Kei). Akizungumza mara baada ya utiaji saini huo, Waziri Masauni amesema Makubaliano ya Mashirikiano yaliyosainiwa yamekusudiwa kuimarisha uhusiano kati ya Japan na Tanzania kwa maendeleo endelevu na hatua za kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi. . Go to the bow bow. Amesema mashirikano haya yataongeza  fursa ya kupanua soko la Biashara ya Kab...

EWURA YAHAMASISHA NISHATI SAFI YA KUPIKIA SINGIDA NA IRINGA

Image
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Kati, imeendelea kutoa hamasa ya matumizi ya nishati safi ya kupikia mkoani Singida na Iringa sanjari na kuvutia uwekezaji wa bidhaa hiyo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa nishati safi ya kupikia. Hamasa hiyo imetolewa na Meneja wa EWURA, Kanda ya Kati, Mha. Hawa Shani Lweno, kupitia vipindi vya redio mkoani Singida na Iringa pamoja na semina kwa mama lishe, waendesha bodaboda na wasambazaji wa gesi ya kupikia (LPG), iliyofanyika kati 27 na 29 Mei, 2025.  “ Lengo letu ni kuhakikisha watumiaji wa gesi ya kupikia wanazingatia masuala ya usalama, afya na utunzaji wa mazingira pamoja na kuhakikisha watoa huduma tunaowadhibiti wanafuata na kutii masharti ya leseni zao” Alisisitiza Mha. Lweno.

KAPINGA ATAJA VIGEZO VYA ZIADA UPELEKAJI UMEME VITONGOJINI

Image
-Lengo ni kuhakikisha kila Jimbo linakuwa na vitongoji vingi vilivyofikiwa na umeme* -Vinahusisha mahitaji ya kiuchumi na Kijamii, ukubwa wa Jimbo na Kitongoji* -Mkurugenzi Mkuu REA atakiwa kumsimamia kwa karibu Mkandarasi wa miradi ya Vitongoji Ziwa Tanganyika* Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesema Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inatekeleza miradi ya umeme katika Vitongoji kwa kuzingatia vigezo vya ziada ikiwemo ukubwa wa vitongoji, ukubwa wa Jimbo pamoja na mahitaji ya kiuchumi na kijamii. Lengo la kuweka vigezo hivyo ni kuhakikisha kuwa kila jimbo linakuwa na vitongoji vingi vilivyofikiwa na nishati ya umeme. Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Mei 29, 2025 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la la Mbunge wa Simanjiro, Mhe. Christopher Olesendeka aliyeuliza kwamba Serikali imejipangaje kutekeleza miradi ya Vitongoji kulingana na jiografia ya Wilaya ya Simanjiro ambapo umbali kutoka Kitongoji kimoja hadi kingine ni zaidi ya kilometa kumi.   "...

WAZIRI MKUU MAJALIWA AKUTANA NA WAZIRI MKUU WA JAPAN

Image
-Asema Japan itaendelea kuimarisha ushirikiano na Serikali ya Tanzania_ -Aagiza tathmini ya barabara za Kibiti-Lindi na Morogoro-Dodoma_ Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amekutana na Waziri Mkuu wa Japan, Ishiba  Shigeru ambaye amemuhakikishia kuwa nchi hiyo itaendelea kuimarisha ushirikiano na Tanzania jambo ambalo linalenga kuchochea ukuaji wa uchumi kutokana na fursa zitakazoendelea kupatikana kupitia mahusiano hayo. Amekutana na kiongozi huyo leo (Alhamisi, Mei 29, 2025) katika ofisi ya Waziri Mkuu Tokyo, Japan, ambapo Mheshimiwa Majaliwa amesema ahadi hiyo inazidi kutoa fursa ya wawekezaji na wafanyabiashara wa Japan pamoja na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Japan (JICA) kuendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kumueleza Waziri Mkuu huyo kuwa  pamoja na miradi mingine wanayotekeleza nchini, Japan kupitia JICA iangalie uwezekano wa kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuzifanyia ukarabati mkubwa barabara za Morogo...

DKT. SAMIA AONGOZA KIKAO CHA NEC

Image
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiongoza Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), kilichofanyika katika Ukumbi wa NEC, jijini Dodoma, leo Jumatano, tarehe 28 Mei 2025. 

MAKAMU WA RAIS AFANYA MAZUNGUMZO NA DKT ADESINA

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akifanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) anayemaliza muda wake Dkt. Akinumwi Adesina kando ya Mkutano wa Mwaka wa Bodi ya Magavana wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) unaofanyika katika Hoteli ya Sofitel Ivoire Jijini Abidjan nchini Ivory Coast.

WAZIRI DKT. GWAJIMA AAINISHA VIPAUMBELE VITANO WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII 2025/2026

Image
Waziri wa Maendeleo ya Jamii. Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ameainisha vipaumbele vya Wizara vikubwa vitano katika utekelezaji wa Bajeti kwa mwaka wa fedha 2025/2026. Mhe. Dkt. Gwajima ameainisha hayo wakati akiwasilisha Bajeti ya Wizara hiyo kwa Mwaka husika wa Fedha leo Mei 27, 2025 Bungeni jijini Dodoma. Ameeleza kuwa Wizara kupitia Idara na Taasisi zilizo chini yake zitatekeleza vipaumbele hivyo ambavyo ni kukuza ari ya Jamii kushiriki katika kupanga na kutekeleza miradi ya maendeleo kwa ngazi ya msingi, kuratibu na kuimarisha utoaji wa huduma za ustawi wa maendeleo ya jamii, kutambua pamoja na kuratibu maendeleo ya ustawi kwa Makundi Maalum. Mhe. Dkt. Gwajima ameongeza kuwa vipaumbele vingine ni pamoja kuboresha mazingira ya kufundisha na kujifunzia katika Taasisi na Vyuo vya Ustawi na Maendeleo ya Jamii na kuimarisha mazingira ya ushiriki na mchango wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali katika Maendeleo ya Taifa. Amesema Wizara imeendelea kuratibu uteke...

WAZIRI MASAUNI ATOA ONYO UZALISHAJI NA MATUMIZI BIDHAA ZA PLASTIKI

Image
Serikali imetoa onyo kali kwa watu na kampuni zinazoendelea kuzalisha bidhaa za mifuko ya plastiki iliyopigwa marufuku na kuingiza katika matumizi kwa njia za panya. Imesema itaendelea kufanya doria za kushtukiza katika viwanda, viwanda bubu na masoko ili kuwabaini na kuwachukulia hatua wahusika wote wanaojihusisha na biashara hiyo. Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Mhandisi Hamad Yussuf Masauni amesema hayo leo Mei 27, 2025 jijini Dodoma wakati akitoa tamko la Serikali kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo kilele chake kitakuwa jijini Dodoma na mgeni rasmi anatarajia kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. Hatua hiyo inakuja kutokana na kujitokeza kwa changamoto ya matumizi ya vifungashio vya plastiki aina ya tubings kutumika kama vibebeo na vifungashio ambavyo havina sifa na kutokukidhi matakwa yaliyowekwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS). Kufuatia hatua, Mhandisi Masauni amelielekeza Baraza ...

MITAA 58 HALMASHAURI YA MJI WA TARIME IMEFIKIWA NA UMEME– MHE. KAPINGA

Image
DODOMA. Naibu Waziri wa Nishati, Mhe Judith Kapinga amesema Serikali imefikisha umeme kwenye mitaa 58 ya Mji wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime kati ya mitaa 81 ya Halmashauri hiyo. Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Mei 26, 2025 bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la la Mbunge wa Tarime Mjini, Mhe. Michael Kembaki aliyeuliza Serikali itapeleka lini umeme katika mitaa 18 ya Halmashauri ya Mji wa Tarime.    "Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ya Mji wa Tarime ina mitaa 81, kati ya hiyo mitaa 58 tayari imefikiwa na umeme, na mitaa 23 bado haijafikiwa na umeme." Amesema Kapinga Ameongeza kuwa, mitaa 13 inapelekewa umeme kupitia mradi wa Hamlets Electrification Project - IIA (HEP IIA) unaotekelezwa na Mkandarasi Dyname Construction Engineering, na mitaa 10 iliyobaki itafikishiwa umeme katika miradi inayofuata. Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu Wanawake (UWT), Mhe. Zaytuni Swai aliyeuliza kuhusu jinsi Serikali ilivyojipanga kupeleka umeme maeneo ya pembezoni mwa mji wa ...

RAIS SAMIA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA HALMASHAURI YA CCM DODOMA

Image
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoani Dodoma tarehe 26 Mei, 2025