Posts

Showing posts from December, 2025

MWENYEKITI TBN ATUMA SALAMU ZA MWAKA MPYA

Image
  Ndugu Wasomaji na Watumiaji wa Blogu Tanzania. Tunapouaga mwaka 2025, nachukua fursa hii, kwa niaba ya wanachama wote wa Tanzania Bloggers Network (TBN), kuwapongeza Watanzania wenzangu kwa kumaliza mwaka huu "kibabe".  Tumekuwa na mwaka wenye matukio mengi ya kihistoria, na ninyi wasomaji wetu mmekuwa wadau muhimu kwa kufuatilia habari, uchambuzi, na taarifa mbalimbali kupitia majukwaa yetu ya kidijitali. Kuelekea Mwaka 2026: Makubwa Zaidi Yanakuja! Mwaka 2026 unakwenda kuwa mwaka wa mageuzi makubwa kwa TBN. Tunatarajia kuleta maudhui yenye ubunifu wa hali ya juu, habari za kina, na teknolojia ya kisasa zaidi katika kuhabarisha umma. Wanachama wetu wamejipanga kuwa daraja imara zaidi kati ya serikali na wananchi, tukihakikisha kila Mtanzania anapata habari sahihi na kwa wakati. Ombi Langu kwa Watanzania: Tunapoingia 2026, rai yangu ni kuendelea kudumisha amani na utulivu. Tuepuke vurugu na migawanyiko, badala yake tujikite katika umoja wetu kama Taifa. Huu ni wakati wa kuu...

WANANCHI FUONI WAJITOKEZA KUPIGA KURA KUCHAGUA MBUNGE WAO

Image
Mkazi wa Shehia ya Migombani katika jimbo la Fuoni akipiga kura leo kumchagua Mbunge wa jimbo hilo.  Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taiofa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufaa Mhe. Jacobs Mwambegele akiwa na mkazi wa Shehia ya Fuoni aliyekua akihakiki jina lake kabla ya kuingia kupiga kura leo.  Mjumbe wa Tume, Mhe. Magdalena Rwebangira akizungumza mmoja wa wasimamizi wa viuo vya kupigia Kura katika jimbo la Fuoni Mjini Zanzibar leo.  Mkazi wa Shehia ya Migombani katika jimbo la Fuoni akipiga kura leo kumchagua Mbunge wa jimbo hilo katika kituop cha Skuli ya Raudha B.  Mwenyekiti wa Tume na Mjumbe wa Tume hiyo wakizungumza na Mawakala katika moja ya vituo vya kupigia Kura.  Wananchi wa Jimbo la Fuoni na Siha pamoja na Kata tano za Tanzania bara wamejitokeza kwawingi kupiga kura leo Desemba 30,2025 katika Uchaguzi mdogo uliofanyika katika majimbo yao. Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufaa Mhe. Jacobs Mwambegele leo Desemba 30,2025 ametembelea na kushuhudi...

UMOJA KUWAVUSHA WATANZANIA NA WACHOCHEZI WANAOWEKA MTEGO WA UDINI

Image
Katika hali inayoashiria kuongezeka kwa umakini wa Serikali dhidi ya mbinu mpya za "Wababe wa dunia" wanaotafuta kuvuruga mataifa yanayochipukia, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa onyo kali kuhusu mtego wa kidini unaosukwa kuhujumu amani ya nchi. Akizungumza Desemba 29, 2025, wakati wa ziara ya kikazi jijini Dar es Salaam, Waziri Mkuu amechambua kwa kina namna mataifa mengi yanavyoingizwa kwenye machafuko kupitia mbinu za kupandikiza chuki za kiimani. Waziri Mkuu amebainisha kuwa Tanzania imefanikiwa kuvuka mtego wa ukabila uliolimaliza mataifa mengine, lakini sasa kuna jitihada za makusudi za kutaka kuitumbukiza nchi kwenye mtego wa udini—mtego ambao ameuita kuwa "hauna mshindi." Tofauti na migogoro mingine, mgogoro wa kidini unagusa hisia za ndani kabisa za binadamu. "Ukigusa imani ya mtu, hapo hakuna mshindi," alionya Waziri Mkuu, akisisitiza kuwa moto wa kidini ukishawaka, hauchagui mchochezi wala mnyamazaji. Mkakati wa 'Gawa Uw...

DKT. KIJAJI AWASILI TFS KWA ZIARA YA KIKAZI

Image
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, amewasili ofisi za Makao Makuu ya Wakala wa Misitu Tanzania (TFS), Jijini Dodoma, kwa lengo la kukagua shughuli za uhifadhi na Utalii.  Waziri Kijaji amepokelewa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii Bw. Nkoba Mabula,  Kamishna Mkuu wa Uhifadhi TFS, Prof. Dos Santos Silayo, Menejimenti ya Wizara pamoja na Maafisa wa taasisi hiyo pamoja na kukagua gwaride maalum lililoandaliwa na Jeshi la Uhifadhi

WANANCHI SIHA, FUONI, KATA TANO KUPIGA KURA KUCHAGUA WABUNGE NA MADIWANI KESHO

Image
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji wa Rufaa Mhe. Jacobs Mwambegele leo Desemba 29,2025 amesoma risala maalum kuhusu uchaguzi wa ubunge katika jimbo la Siha lililopo Halmashauri ya Wilaya ya Siha, Mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania Bara na Jimbo la Fuoni lililopo Wilaya ya Magharibi B, Mkoa wa Mjini Magharibi, Tanzania Zanzibar unaotaraji kufanyika Desemba 30,2025.   Jaji Mwambegele amesema, uchaguzi mdogo huo utahusisha pia, kata tano za Tanzania Bara. Kata hizo ni;            Chamwino iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, Mkoa wa Morogoro; Mbagala Kuu iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Mkoa wa Dar es Salaam; na Nyakasungwa iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Buchosa, Mkoa wa Mwanza.   Nyingine ni Kata ya Masoko iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbeya, Mkoa wa Mbeya; na kata ya Ndono iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Uyui, Mkoa wa Tabora.   Aidha, amesema jumla ya wagom...

JESHI LA POLISI LAWASHUKURU WATANZANIA KWA KUDUMISHA AMANI SIKU YA KRISMASI

Image
Na Mwandishi wetu,Dodoma Jeshi la Polisi Tanzania limetoa shukrani kwa wananchi wote nchini kwa ushirikiano waliouonyesha katika kulinda na kudumisha amani kipindi chote cha Sikukuu ya Krismasi, iliyoadhimishwa  25 Desemba 2025.  Kwa mujibu wa Taarifa  iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu, Dodoma DCP David Misime ,amesema hatua hiyo imewezesha sherehe za mwaka huu kufanyika kwa utulivu na bila changamoto  za kiusalama.  Amesema hali ya usalama imeendelea kuwa shwari katika maeneo yote ya nchi, huku wananchi wakiendelea kusherehekea sikukuu kwa kufuata sheria, taratibu na kanuni za nchi bila wasiwasi wala hofu.  " Jeshi la Polisi limeeleza kuwa ushirikiano baina ya wananchi na vyombo vya ulinzi umekuwa nguzo muhimu katika kufanikisha dhamira ya kulinda amani na kutengeneza mazingira mazuri ya kusherehekea, "amesema Akitoa wito kwa umma, Msemaji wa Jeshi hilo amewataka Watanzania kuendelea kuilinda amani kama msingi wa maendeleo ya taifa....

DKT. ABBAS AHAMASISHA WAKAZI WA DAR ES SALAAM KUSHIRIKI TAMASHA LA FUNGA MWAKA KIJANJA TALII

Image
Na Beatus Maganja,Dar Es Salaam. Tamasha la Funga Mwaka Kijanja Talii Msimu wa Pili linaloendelea katika Viwanja vya Sabasaba, jijini Dar es Salaam, limeelezwa kuwa fursa adhimu kwa wakazi wa jiji hilo na Watanzania kwa ujumla kushiriki kikamilifu katika utalii wa ndani kwa kujionea vivutio mbalimbali vya wanyamapori. Tamasha hilo lililoanza mwezi Desemba 2025 na linatarajiwa kufikia tamati Januari 05, 2026, ni sehemu ya kampeni kubwa ya kitaifa ya kuhamasisha utalii wakati wa msimu wa sikukuu na kufunga mwaka. Limeandaliwa na kuratibiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Bodi ya Utalii Tanzania (TTB). Akizungumza mapema leo Desemba 24, 2025, wakati wa ziara ya kutembelea tamasha hilo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbas, ametoa wito kwa wakazi wa Mkoa wa Dar es Salaam na mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi kushiriki tamasha hilo ili kupata elimu ya uwekezaji katika sekta ya utalii, kushiriki biashara ya nyara na kupata kitoweo cha nyama pori kwa njia...

EWURA, TRA KUIMARISHA USHIRIKIANO

Image
Na Mwandishi Wetu, Dodoma. Watendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na wenzao wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), leo 23 Desemba 2025, wamekutana na  kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano wa utendaji hususani katika usimamizi wa masuala ya kikodi yanayotokana na huduma zinazodhibitiwa na EWURA.  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Bwana Gerald Maganga, amesema EWURA ni mshirika mzuri katika kuisaidia TRA kutekeleza wajibu wake wa usimamizi wa kodi nchini.  “Ushirikiano uliopo kati ya taasisi hizi mbili, utatupeleka mbele, tuudumishe na tusimamie utekelezaji wa makubaliano yetu,” alisema.  Meneja wa TRA mkoa wa Dodoma, Bwana Pendolake Elinisafi, ameishukuru EWURA kwa kuipatia TRA ushirikiano mzuri, na kuahidi kuuendeleza ili kuweka msingi imara wa mafanikio ya taasisi hizo mbili na taifa kwa ujumla.

SERIKALI YAHIMIZA MAADILI NA UZALENDO

Image
Serikali imesisitiza umuhimu wa jamii kuimarisha maadili na uzalendo miongoni mwa vijana nchini kwa kutumia taasisi za elimu ili kujenga taifa lenye misingi imara ya utu, uwajibikaji. Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi, akiwa mgeni rasmi katika Mdahalo wa maadili na uzalendo uliofanyika katika Chuo cha Maendeleo ya Jamii Buhare, mkoani Mara. Mahundi amesema, Serikali ya Awamu ya Sita inaamini kuwa maendeleo ya kweli ya taifa hayawezi kupatikana bila kujenga maadili ya wananchi wake, hususan vijana ambao ndiyo nguvu kazi na viongozi wa baadaye. “Huwezi kujenga taifa lenye maendeleo ya kweli bila kujenga maadili ya raia wake. Vijana wanapaswa kulelewa katika misingi ya utu, uzalendo, uwajibikaji na kuheshimu sheria, kwa sababu wao ndiyo nguzo ya sasa na ya baadaye ya taifa letu, vyuo vina nafasi ya kipekee katika kumjenga kijana kwa sababu vinamgusa katika hatua muhimu ya maisha yake hivyo serik...

WAUMINI WAMCHONGEA PADRI KITIMA VATICAN, WAOMBA UCHUNGUZI UFANYIKE WA MWENENDO WAKE

Image
Waumini wa Kanisa Katoliki nchini Tanzania, Stanslaus Thobias Nyakunga na Elia Phaustine Kabote, wamewasilisha rasmi barua kwa Archbishop Angelo Accattino, Balozi wa Vatican nchini, wakiomba kufanyika kwa uchunguzi wa kichungaji na kiutawala kuhusu mwenendo wa Padri Dkt. Charles Kitima, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC). Kwa mujibu wa waumini hao, hatua hiyo imechukuliwa kufuatia malalamiko na mitazamo iliyoenea kwa muda mrefu katika jamii, kwamba Padri Kitima amekuwa akihusishwa na masuala ya siasa za CHADEMA, hususan kuonekana kuingilia au kushiriki katika migogoro ya ndani ya chama hicho—jambo ambalo, wanasema, halijaonekana kwa vyama vingine vya siasa. Waumini hao wanasema mitazamo hiyo, iwe ni ya kweli au la, imeanza kuibua sintofahamu miongoni mwa waumini na kuliweka Kanisa katika mazingira yanayoweza kutafsiriwa kama ya upendeleo wa kisiasa, hali inayohatarisha nafasi ya Kanisa kama taasisi ya amani, upatanisho na mwongozo wa kimaadili kwa jamii. Katika barua yao ...