Posts

Showing posts from November, 2024

SHULE ZA MSINGI 139 MBINGA, KUPEWA KOMPYUTA

Image
  WA ELIMU" - JUDITH KAPINGA November 28, 2024 Naibu Waziri wa Nishati ambaye pia ni Mbunge wa Vijana Mkoa wa Ruvuma (CCM), Mhe.Judith Kapinga ameahidi kutoa kompyuta 139 katika Shule za Msingi 139 zilizopo Halmashauri ya wilaya ya Mbinga Vijijini ili kuchochea kasi ya ukuaji wa Elimu katika wilaya hiyo. Mhe. Kapinga ametoa ahadi hiyo Novemba 28, 2024 wakati wa hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi kwenye ujenzi wa Nyumba ya Mwalimu katika Shule ya Msingi Mbungani iliyopo Halmashauri ya wilaya ya Mbinga Vijijini. "Nitatoa kompyuta 139 ifikapo Januari 2025 ili zitumike katika Shule za Msingi 139 zilizopo Halmashauri ya Wilaya Mbinga Vijijini kwa lengo la kuendelea kuchochea kasi ya ukuaji wa maendeleo ya Elimu nchini." Amesema Mhe. Kapinga Aidha, pamoja na kuweka Jiwe la Msingi la ujenzi wa nyumba ya Mwalimu katika Shule ya Msingi Mbungani wilayani Mbinga, Mhe.Kapinga amechangia fedha ili kuongeza nguvu katika ujenzi wa nyumba hiyo Akizungumza na Wazee wa Kijiji cha Kindimba...

TMA YATOA TAHADHARI KUFUATIA HALI MBAYA YA HEWA KWA SIKU TANO MFULULIZO

Image

ADO ATIMIZA HAKI YAKE KIKATIBA,APIGA KURA KIJIJINI KWAO

Image
     Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo,.Ado Shaibu akipiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji katika Kijiji cha Ngalinje, Wilaya ya Tunduru.

NIMEPIGA KURA,NIMETIMIZA HAKI YANGU KIKATIBA

Image
Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga leo ameshiriki zoezi la kupiga  kura katika Kitongoji cha Mheza kijiji cha Mkumbi Halmashauri ya Mbinga Vijijini ili kuchagua viongozi wa eneo husika. Kapinga ameeleza kuwa, kwa kufanya hivyo ametimiza haki yake ya kikatiba na kutoa wito kwa Watanzania wote kuitumia haki hiyo kikamilifu. Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni miongoni mwa mihimili muhimu ya Demokrasia inayowezesha ushiriki wa wananchi katika uongozi wa maeneo yao.

DKT NDUGULILE AFARIKI DUNIA

Image
      Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb) anasikitika kutangaza kifo cha Mbunge wa Kigamboni, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulile kilichotokea usiku wa kuamkia leo tarehe 27 Novemba, 2024 chini India alipokuwa akipatiwa matibabu.  "Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mbunge wa Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika, Mheshimiwa Dkt. Faustine Ndugulle. Kwa niaba ya Wabunge natoa pole kwa familia, wakazi wa Kigamboni na Watanzania wote. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi", amesema Spika.  Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia inaendelea kuratibu shughuli za mazishi na taarifa zaidi zitaendelela kutolewa. 

TUJITOKEZE KWA WINGI KUPIGA KURA-MH KAPINGA

Image
Mbunge wa Vijana Mkoa wa Ruvuma (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amewaasa wananchi kujitokeza kwa wingi tarehe 27 Novemba 2024 kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ikiwa pia ni utekelezaji wa haki ya kikatiba. Kauli hiyo ameitoa Novemba 26, 2024 wakati wakihitimisha kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Halmashauri ya wilaya ya Mbinga Vijijini. Akizungumza na Wananchi waliojitokeza katika shughuli hiyo ya ufungaji wa kampeni, Kapinga amewaasa wajitokeze kwa wingi kuchagua wagombea kutoka CCM kwani ndio wenye uchungu na maendeleo ya nchi na ustawi wa jamii. "Chama cha Mapinduzi (CCM) ni tumaini la watanzania wanaohitaji maendeleo, hivyo ifikapo Novemba 27, 2024 jitokezeni katika vituo vya kupigia kura ili mkachague Viongozi kutoka CCM watakaosimamia miradi ya maendeleo kwa kipindi cha miaka mitano ijayo katika Mitaa na Vijiji." Amesema Kapinga Ameeleza kuwa, CCM imekuwa na utaratibu mzuri wa ku...

KAPINGA AENDELEA NA MCHAKAMCHAKA KUHAMASISHA WANANCHI KUSHIRIKI UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.

Image
  Mbunge wa Vijana Mkoa wa Ruvuma (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga anaendelea na kazi ya kuhamasisha Wananchi katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Ruvuma ili waweze kujitokeza kwa wingi kupiga kura katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27 mwaka huu. Baada ya ziara ya mafanikio aliyoifanya wilayani Namtumbo, Mhe. Kapinga amefanya ziara pia wilayani Mbinga kwa kuanza na Vijiji vya Mkako na Kigonsera ambapo amewaasa Wananchi kuchagua Viongozi bora watakaosimamia shughuli za maendeleo katika Mitaa, Vijiji na Vitongoji hapa nchini. "Wananchi mliopo katika Kata ya Kigonsera, Mkako na maeneo yote ya Mbinga ifikapo Novemba 27, 2024 jitokezeni kushiriki uchaguzi wa Serikali za mitaa ili mchague Viongozi makini kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM)." Amesisitiza Kapinga Amesema lazima umakini uwepo katika uchaguzi wa Viongozi kwani ndio watakuwa wasimamizi wakuu wa miradi ya maendeleo kwenye maeneo ya Wananchi hivyo waangaliwe watu watakao...

TMA YAELEZA ATHARI ZA MABADILIKO YA TABIANCHI KWENYE KILIMO CHA MWANI

Image
Baku,Azerbaijan;  Kaimu Mkurugenzi wa TMA, Zanzibar, Masoud Faki ameeleza namna kilimo cha mwani kinavyoweza kuathiriwa na mabadiliko ya hali ya hewa na tabianchi. Faki Amesema hayo wakati akiwasilisha mada katika Banda la Tanzania, lililopo kwenye Mkutano wa 29 wa Nchi wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya Tabianchi (COP29), unaofanyika Baku,Azerbaijan.. Alieleza kuwa kilimo cha mwani kinaathiriwa zaidi na mabadiliko ya hali ya hewa hususani mvua nyingi,joto kali na upepo mkali. Aidha, alifafanua, TMA inatoa huduma za utabiri ikiwemo Msimu na utabiri wa hali mbaya ya hewa wa siku tano ambao huwezesha wakulima kufanya maamuzi sahihi kama vile uchaguzi wa eneo linafaa ili kukabiliana na hali ya mvua nyingi ambayo husababisha upungufu wa kiwango cha chumvi na hivyo kusababisha magonjwa. Maamuzi mengine ni uvunaji wa zao hilo ili kukabiliana na upepo mkali unaoweza kuleta madhara ya mwani kukatika na kupotelea baharini.

TANZANIA,UGANDA KUENDELEA KUIMARISHA USHIRIKIANO

Image
  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio amesema nchi za Tanzania na Uganda zitaendelea kushirikiana katika uendelezaji wa miradi mbalimbali ya Nishati ikiwemo Sekta ya Mafuta na Gesi. Dkt. Mataragio ameyasema hayo Novemba 22, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Waandishi wa habari baada ya kushiriki Jukwaa la Kibiashara kati ya Tanzania na Uganda . “Tunaangalia ni kwa jinsi gani sekta hii ya Mafuta na Gesi inaweza ikachangia katika maendeleo ya Nchi hizi mbili, tumekuwa na mijadala mbalimbali inayolenga kuiendeleza sekta hii ya mafuta na gesi.” Amesema Dkt. Mataragio Ameongeza kuwa, mjadala mkubwa katika Jukwaa hilo ni kuangalia namna gani Nchi za Tanzania na Uganda zinaweza kushirikiana katika sekta za mafuta na gesi. Mataragio amesema Tanzania na Uganda zinahistoria ndefu ndefu za mashirikiano akitolea mfano mradi wa kimkakati wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi wa EACOP. Akiuelezea mradi huo wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi (EACOP), Dkt. Mata...

RAIS SAMIA ATOA BILIONI 24 KUTEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO NAMTUMBO

Image
Mbunge wa Vijana Mkoa wa Ruvuma (CCM) ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga amempongeza Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa zaidi ya shilingi bilioni 24 kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya Namtumbo mkoani Ruvuma. Kauli hiyo ameitoa Novemba 21, 2024 wakati wa uzinduzi wa Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wilaya ya Namtumbo, Mkoa wa Ruvuma ambao unalenga kupata Viongozi wa ngazi za Mitaa, Vijiji na Vitongoji hapa nchini. "Serikali kupitia kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kutoa fedha ili kufanikisha utekelezaji wa shughuli za maendeleo ikiwemo ujenzi wa shule ya Wasichana, miradi ya kusambaza umeme kwenye Vijiji na Vitongoji, Elimu, Afya, Kilimo, Maji, Ujenzi wa Kituo cha Polisi na Mahakama katika wilaya hii ya Namtumbo."  Ameeleza Mhe. Kapinga Katika Sekta ya Umeme amesema kuwa, Vijiji zaidi ya 12,000 Tanzania Bara vimepata umeme na kazi hiyo imefanyika kwa maf...

TANAPA YAMKABIDHI DKT YONAZ MILLION 20 KUSAIDIA ZOEZI LA UOKOAJI KARIAKOO

Image
Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania(TANAPA) limekabidhi Hundi ya shilingi milioni 20 katika kitengo cha maafa Ofisi ya Waziri Mkuu ,ikiwa ni mchango wa kuwezesha shughuli za uokoaji katika Jengo la ghorofa  lililoporomoka Kariakoo hivi karibuni Jijini Dar es salaam. Akizungumza leo Novemba 21, 2024 Katika eneo la tukio kariakoo Jijini Dar es salaam wakati wa kukabidhi hundi hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA, Jenerali mstaafu George Waitara amesema kuwa tukio hilo limesababisha maafa makubwa ikiwemo vifo,uharibifu wa mali pamoja na matatizo ya kisaikolojia kwa waathirika wa tukio hilo. " TANAPA ni sehemu ya wananchi wa Tanzania,hivyo tumeguswa tukaona tutoe chochote ili kusaidia zoezi la Uokoaji" amesema Jenerali Waitara. Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge na Uratubu  Dr.Jimmy Yonazi ameishukuru TANAPA kwa msaada huo,nakuwaomba Watanzania walioguswa na maafa hayo  waendelee kutoa michango yao ili kufanikisha zoezi la uokoaji kwa hara...

SERIKALI YAONGEZA SAA 24 UOKOZI KARIAKOO

Image
  NA MWANDISHI WETU  MKURUGENZI wa Idara ya Habari-Maelezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali, Thobias Makoba, amesema zoezi la uokoaji wa watu walionasa kwenye jengo lililoporomoka Jumamosi ya Novemba 16, 2024 Kariakoo kwenye Mtaa wa Congo na Mchikichi Jijini Dasr es Salaam, litaendelea tena kwa saa 24 za ziada baada ya saa 72 za kawaida za kiwango cha kimataifa kumalizika. Makoba ameyasema hayo leo Novemba 19, 2024, wakati akizungumza na waandishi wa habari Kariakoo kwenye eneo la tukio, ambapo amesema kuongezeka kwa saa hizo 24 za ziada, ni agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, alilolitoa kupitia kwa Waziri Mkuu  Kassim Majaliwa, katika kikao cha tathmini kuhusu zoezi hilo la uokoaji ambapo amelitaka jeshi la zimamoto na uokoaji, kuendelea na shughuli hiyo ili kunusuru uhai wa watu ambao bado wamekwama kwenye jengo hilo. “Tukiwa kwenye kikao cha tathmini cha kazi inayoendelea, moja ya ajenda iliyozungumzwa ni kuhusiana na utaratibu ...

NAIBU WAZIRI UMMY AWASHUKURU RED CROSS NA TPA KWA MISAADA YA VIFAA SAIDIZI MAAFA KARIAKOO

Image
  NA. MWANDISHI WETU Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mheshimiwa Ummy Nderiananga amewashukuru wadau kutoka Shirika la Msalaba Mwekundu (Red Cross Tanzania) pamoja na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania TPA kwa kutoa misaada ya vifaa saidizi kwa ajili ya kuendelea kusaidia katika zoezi la uokoaji linaloendelea kufuatia janga la kuporomoka jengo la ghorofa eneo la Congo na Mchikichi Kariakoo Wilaya ya Ilala Jijini Dar es Salaam. Ametoa shukrani hizo hii leo Novemba 19, 2024 na kueleza kuwa miongoni mwa vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na machela tisa (9) mashuka 100 kutoka Shirika la Msalaba Mwekundu (Red Cross Tanzania) Pamoja na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania TPA, reflectors pamoja na  cover white. Naibu Waziri huyo ameendelea kutoa rai kwa wadau mbalimbali kuendelea kujitokeza kuchangia huku akipongeza namna zoezi la uokoaji linavyoendelea kwa kushirikiana na wadau.

UTABIRI WA HALI YA HEWA SAA 24 ZIJAZO

Image
  Share This:          

KASI YA MAENDELEO DAR ES SALAAM INACHANGIA ONGEZEKO LA MAHITAJI YA UMEME- MHE. KAPINGA.

Image
DAR ES SALAAM. Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga amesema ukuaji wa kasi wa maendeleo na uchumi katika Mkoa wa Dar es Salaam unachangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa ongezeko la mahitaji ya umeme. Ameyasema hayo leo 18 Novemba, 2024 wakati wa ziara yake kwenye Kituo cha kuzalisha umeme cha Kinyerezi jijini Dar es Salaam iliyolenga kukagua maendeleo ya maboresho ya miundombinu ya umeme katika kituo hicho ili kukiongezea uwezo.  Kituo hicho kinachohudumia wakazi wa Gongo la Mboto, Mbagala, Kigamboni na Dege kinafungwa Transfoma yenye uwezo wa jumla ya 400 MVA huku Transfoma za ukubwa wa 175 MVA zikiwa zimeshafungwa. ‘’Nipende kuwatoa hofu wakazi wa Dar es Salaam na Pwani hususani Gongo la Mboto, Dege na Mkuranga kuwa TANESCO imekamilisha maboresho iliyokuwa ikifanya siku tatu zilizopita na tayari transfoma zimefungwa na hivyo kupunguza mzigo kwenye vituo vya Mbagala Ubungo na Dege na Gongo la Mboto‘’. Amesema Mhe. Kapinga Ameeleza kuwa, kwa sasa kasi ya ukuaji wa Mkoa wa Dar ...