Posts

Showing posts from August, 2025

UCHIMBAJI WA URANIUM NAMTUMBO KUAJIRI 104,000

Image
Chini ya Rais Samia,Tanzania itaanza uchimbaji wa uranium katika Wilaya ya Namtumbo, Ruvuma, yenye akiba ya tani milioni 139 na uhai wa mgodi ni miaka 22.  Mradi huu una gharama ya shilingi trilioni 3.06 na unajumuisha uchimbaji na kuongeza thamani ya uranium ndani ya nchi, pamoja na mpango wa kuunda kiwanda cha nguvu kwa kutumia uranium kilichochimbwa hapa nchini.  Utekelezaji unatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 4,000 za moja kwa moja na zaidi ya 100,000 zisizo za moja kwa moja, huku ukilenga sera ya serikali ya kuongeza thamani ya ndani kwenye Sekta ya madini chini ya Rais Samia.

INEC YATOA TAARIFA KUHUSU RUFAA DHIDI YA UAMUZI WA WASIMAMIZI WA UCHAGUZI NA PINGAZIMIZI ZA WAGOMBEA UBUNGE NA UDIWANI

Image
 

UTABIRI WA HALI YA HEWA AGOSTI 31,2025

Image

DKT. SAMIA ATIKISA KILOSA

Image
  Mgombea wa Urais kupitia CCM Dkt Samia Suluhu Hassan ameendelea na ziara za kampeni za uchaguzi mkuu wa 2025 ambapo janaamefanya mikutano ya kampeni katika Wilaya ya Kilosa, ambapo amenadi sera zake kwa umati mkubwa uliomlaki katika wilaya hiyo.  Dkt. Samia ameahidi kuendelea kuimarisha miundombinu ya barabara kwa kukamilisha ujenzi wa barabara ya Kilosa–Ulaya–Mikumi, ambayo imeanza kujengwa na itakamilika ndani ya kipindi cha miaka mitano ijayo.  Sambamba na hili, ameahidi kuwa endapo atachaguliwa tena katika uchaguzi mkuu wa Oktoba serikali yake itaendeleza ushoroba unaopita reli ya SGR kwa kujenga viwanda na maghala ili kuufanya kuwa kitovu cha biashara na uwekezaji mpya.  Huku akiwahimiza wananchi wa Kilosa kujitayarisha kwa fursa hizo zinazokuja kupitia uwekezaji wa kimkakati katika kipindi cha 2025-2030. Kuhusu changamoto za upatikanaji wa maji, Mhe. Dkt Samia ameahidi kuendeleza na kukamilisha miradi iliyokwisha kuanza sambamba na kuibua miradi mipya ya maji...

TANZANIA , ZIMBABWE ZAKUBALIANA KUENDELEZA UHUSIANO

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Zimbabwe Kanali Mstaafu Kembo Campbell Mohadi, Mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya siku mbili ya Makamu wa Rais wa Zimbabwe hapa nchini.   Katika siku ya kwanza ya Ziara ya Makamu wa Rais Zimbabwe, viongozi hao wameongoza Ujumbe wa Tanzania na Jamhuri ya Zimbabwe katika mazungumzo rasmi ambayo yamelenga namna ya kukuza uhusiano na ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili.  Mazungumzo hayo yamegusia zaidi urafiki wa muda mrefu wa kihistoria baina ya Tanzania na Zimbabwe tangu enzi za harakati za ukombozi wa Taifa la Zimbabwe, ambapo Tanzania chini ya uongozi wa Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ilitoa msaada wa hali na mali kwa wapigania uhuru wa Zimbabwe. Tanzania na Zimbabwe zimekubaliana kuendeleza uhusiano uliopo pamoja na kutunza historia ya mataifa hayo. halikadhalika majadiliano hayo ya...

DK.MWINYI:CCM ITAFANYA KAMPENI ZA KISTAARABU KWA SERA ZENYE TIJA KWA WANANCHI

Image
  RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ambaye pia ni Mgombea Mteule wa Urais wa Zanzibar kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), amechukua fomu ya kugombea nafasi hiyo katika Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) na kuahidi kuwa CCM itafanya kampeni za kistaarabu zitakazozingatia Utamaduni, Silka na Desturi za Wazanzibari. Dkt. Mwinyi amechukua fomu hiyo katika Afisi za Tume ya Uchaguzi leo, tarehe 30 Agosti 2025, asubuhi, na hatimaye msafara wake ukaelekea Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui kupitia Barabara ya Miembeni, Kariakoo, Rahaleo na Michenzani, akisindikizwa na mamia ya wanachama wa chama hicho waliokuwa wamejipanga pembezoni mwa barabara. Aidha, Dkt. Mwinyi amezuru Kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Hayati Abeid Amani Karume, na kisha kuzungumza na Wazee wa Chama Cha Mapinduzi afisini hapo. Akizungumza na mamia ya wanachama wa CCM katika Uwanja wa Mao Tse Tung, Mgombea Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesisitiza kuwa CCM itafanya kampeni zitaka...

TUME YAKUTANA NA VYAMA KUFANYA MABADILIKO MADOGO YA RATIBA YA KAMPENI

Image
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Ndugu. Kailima Ramadhani leo tarehe 30 Agosti, 2025 ameongoza kikao cha wawakilishi wa vyama vya siasa kupitia na kufanya mabadiliko madogo kwenye ratiba ya mikutano ya hadhara ya kampeni za wagombea wa Kiti cha Rais na Makamu wa Rais. Mikutano hiyo iliyoanza tarehe 28 Agosti, 2025 inaendelea hadi tarehe 28 Oktoba, 2025 kwa Tanzania Bara na tarehe 27 Oktoba, 2025 kwa Tanzania Zanzibar. Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano na Madiwani kwa Tanzania Bara utafanyika tarehe 29 Oktoba, 2025.

NISHATI SAFI YA KUPIKIA SIO GESI NA UMEME PEKEE-BW. MLAY

Image
Mkurugenzi wa Nishati safi ya kupikia kutoka Wizara ya Nishati Bw. Nolasco Mlay amesema kuwa nishati safi ya kupikia sio gesi na umeme pekee bali ni zaidi ambapo ameeleza uwepo wa kuni smart,pamoja na teknolojia mbalimbali zinazotumika katika kupikia.  Ameeleza hayo wakati alipotembelea kiwanda cha kuzalisha Kuni Smart cha Chabri Energy Company Limited kilichopo Kijiji cha Kitumba,kitongoji cha Kisha,Kata ya Kisesa, Wilaya ya Magu, jijini Mwanza Agosti 29, 2025. Aidha, ameeleza kuwa kumekua na dhana katika jamii kuamini kuwa nishati safi ya kupikia ni gesi na umeme pekee lakini ukweli ni kuwa nishati safi ya kupikia ni pamoja na mkaa safi (Kuni Smart) ambao unatengenezwa katika kiwanda hiki kwa kutumia mabaki ya mbao. Vilevile, Bw.Mlay ameeleza kuwa nishati safi ya kupikia ni fursa ambayo inawainua wananchi kiuchumi pamoja na kukuza uwekezaji kama huu ambao umefanywa na Chabri Energy Company Limited ambao umekua njia ya kufungua fursa za kuajiri vijana ambao wanaendesha maisha yao ...

SHIMIWI NI MAHALA PA KAZI – Bi ZIANA MLAWA

Image
Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Wizara ya Nishati, Bi. Ziana Mlawa leo amesema kushiriki michezo mbali mbali inasaidia katika kujenga afya ya mwili na akili hivyo mtumishi anapopata nafasi ya kushiriki michezo yeyote aitumie ipasavyo pia husaidia hali itakayowajengea uwezo kujiamini zaidi ikiwemo katika maeneo ya kazi. Bi. Mlawa ameyasema hayo alipokuwa akiwaaga watumishi wa Wizara ya Nishati watakao shiriki michezo ya SHIMIWI itakayofanyika jijini Mwanza kwanzia tarehe 1 Septemba 2025 " Pamoja na kushiriki michezo ambapo ni mbali na eneo la kazi mkumbuke mkiwa huko ni eneo la kazi nidhamu na uadilifu uwe kipau mbele mdaa wote muwapo kwenye michezo  hiyo." Amesisitiza Bi. Mlawa Ameongeza kuwa watumishi hao wajitahidi wapate ushindi ambapo kwa ushindi huo Wizara itapata heshima njee na ndani ya Wizara

HIFADHI YA MPANGA-KIPENGERE YAKONGA NYOYO ZA WALIMBWENDE MISS UNIVERSE 2025

Image
📍Rais Samia Apongezwa uboreshaji Miundombinu Na Beatus Maganja, Mbeya Walimbwende wa Miss Universe Tanzania 2025 wametoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kutokana na maono yake ya kukuza sekta ya utalii nchini kupitia maboresho ya miundombinu ya Hifadhi ya Mpanga Kipengere jambo linaloifanya Hifadhi hiyo kuwa kivutio kikubwa cha watalii nyanda za juu kusini. Kauli hiyo imetolewa Agosti 29, 2025 na walimbwende hao mara baada ya  kufanya ziara maalum katika hifadhi hiyo iliyopo Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya ambayo inasimamiwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA ambapo walibaini fursa kubwa ya kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia urithi wa asili wa eneo hilo. "Tumeona historia ya Chifu Mkwawa, maji ya baraka na maajabu ya asili ya kipekee. Mpanga-Kipengere ni hazina ya Taifa letu. Sasa ni jukumu letu kama mabalozi kuutangaza urithi huu Kwa dunia nzima " alisema Nais Sayona ambaye ni mshindi wa Miss Universe Ta...

VITONGOJI VYOTE KUWAKA UMEME 2025- 2030

Image
Mgombea wa Urais kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameahidi wananchi wa mkoa wa Morogoro kuwa endapo watamchagua katika uchaguzi mkuu kufikisha umeme katika vitongoji vyote vilivyosalia katika mkoa wa Morogoro.  Katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake vijiji na mitaa yote ya mkoa wa Morogoro vimefikishiwa huduma za umeme sambamba na vitongoji vingi.  Kwa mujibu wa takwimu katika kpindi cha uongozi wa miaka minne ya uongozi wake vijiji vilivyofikishiwa huduma ya umeme vimeongezeka kutoka vijiji 437 mwaka 2020 hadi 659 mwaka 2025. Hali ya upatikanaji wa umeme ilikuwa chini asilimia 46 mwaka 2020 ila sasa hali ya upatikanaji wa umeme ni zaidi ya asilimia 90 mwaka 2025.  Dkt. Samia ameahidi kuwezesha ongezeko la upatikanaji wa umeme ili kuwezesha matumizi ya nishati safi katika ngazi ya kaya, sambamba na hili ameongeza kuwa serikali atakayoiunda itajenga vituo vya kupooza umeme katika mkoa wa Morogoro. 

MAKAMU WA RAIS AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA GHANA NCHINI TANZANIA

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Jamhuri ya Ghana nchini Tanzania anayemaliza muda wake Mhe. Damptey Bediako Asare, mazungumzo yaliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam.   Katika mazungumzo hayo, Makamu wa Rais amesema Tanzania na Ghana zimeendelea kunufaika na uhusiano uliopo wa kihistoria ulioanza tangu kipindi cha utafutaji uhuru wa mataifa hayo ukichagizwa na urafiki wa Baba wa Mataifa hayo, Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere pamoja na Baba wa Taifa la Ghana hayati Kwame Nkurumah. Amesema Tanzania inatambua mchango wa Jamhuri ya Ghana katika ukombozi wa Mataifa ya Kusini mwa Afrika wakati wa kupigania uhuru.   Makamu wa Rais amesema mataifa hayo mawili yameendeleza ushirikiano uliopo ambapo kwa sasa yamejikita zaidi katika mahusiano ya kiuchumi. Ameongeza kwamba ni muhimu kuendelea kushirikiana zaidi katika uwekezaji na biashara kupitia mpango wa Eneo Huru la Biashara Af...