Posts

Showing posts from June, 2025

ENG.NGULANGWA ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE KILWA KASKAZINI

Image
Eng. Mohamed Ngulangwa akirejesha Fomu kwa Katibu wa Wilaya ya Kilwa, Mhe. Masendera. KILWA, Juni 29 -  Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma wa CUF–Chama Cha Wananchi, Eng. Mohamed Mshamu Ngulangwa, leo Jumapili amechukua na kurejesha rasmi fomu ya uteuzi ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Kilwa Kaskazini kupitia chama hicho. Hatua hiyo imekuja kufuatia wito wa wazee na vijana wa Jimbo la Kilwa Kaskazini pamoja na Wilaya ya Kilwa waliomhimiza mjukuu na ndugu yao huyo kugombea nafasi hiyo ya uongozi, wakionesha imani kubwa juu ya uwezo na uadilifu wake. Eng. Ngulangwa, ambaye ni mzaliwa wa Kilwa na mmatumbi halisi, anabeba sifa za kipekee kielimu na kitaaluma. Ana Shahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Ujenzi (Master in Engineering Management - MEM), Shahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Biashara (MBA), pamoja na Shahada ya Uhandisi wa Ujenzi (BSc in Civil Engineering). Aidha, ana elimu ya dini ya Kiislamu katika kiwango cha Thanawi. Jimbo la Kilwa Kaskazini ni mojawapo ya...

JAJI MWAMBEGELE AKAGUA MWENENDO UBORESHAJI DAFTARI LA WAPIGA KURA KWENYE MAGEREZA

Image
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele leo Juni 28, 2025 ametembelea na kukagua mwenendo wa zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika Magereza ya Bukoba, Muleba, Biharamulo mkoani Kagera na Chato mkoani Geita.  Mzunguko wa tatu wa awamu ya pili ya uboreshaji Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa Wafungwa chini ya miezi sita na mahabusu waliopo katika Magereza kwa Tanzania Bara na Vyuo vya Mafunzo Zanzibar umeanza leo Juni 28, 2025 na utaendelea kwa siku saba hadi Julai 04, 2025

RAIS SAMIA ATAJA MAFANIKIO SEKTA YA NISHATI 2020-2025

Image
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, . Dkt. Samia Suluhu Hassan ameeleza kuwa Sekta ya Nishati imekuwa na mafanikio makubwa  katika kipindi cha miaka mitano.  Ameyasema hayo wakati akihitimisha shughuli za Bunge Jijini Dodoma tarehe  28 Juni 2025. "Mheshimiwa Spika kutokana na umuhimu wa Sekta ya Nishati kwa maendeleo ya nchi, Serikali imeimarisha upatikanaji wa nishati nchini ikiwemo kukamilisha mradi wa bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere (JNHPP)”. Amesema Mhe. Samia Ameongeza kuwa, mbali ya kukamirisha mradi wa Julius Nyerere pia Serikali imekamilisha upelekaji wa umeme katika Vijiji vyote 12,318  nchini. Ameongeza kuwa, msukumo uliofanywa na Serikali katika sekta ya nishati umewezesha uzalishaji wa umeme kuongezeka hadi kufikia megawati 4031.71 kutoka megawati 1,601.84 mwaka 2020. "Hali hii imechangiwa na miradi mbalimbali ya uzalishaji umeme ukiwemo mradi wa kielelezo wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere wenye megawati 2115, vilevile mradi wa Kinyerezi I ...

WACHIMBAJI WADOGO DODOMA WAPATIWA MAFUNZO YA USALAMA, AFYA NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA MIGODINI

Image
-Mafunzo yanalenga kukuza uchimbaji salama, endelevu na wenye tija katika sekta ya madini ya shaba Wachimbaji wadogo kutoka migodi ya shaba iliyopo katika Mkoa wa Dodoma wamepatiwa mafunzo maalum kuhusu usalama mahali pa kazi, afya, utunzaji wa mazingira na usimamizi wa shughuli za uchimbaji.  Mafunzo hayo ni sehemu ya jitihada za kuimarisha uchimbaji salama na endelevu nchini. Mafunzo hayo yamewahusisha wachimbaji kutoka Mgodi wa Shengde uliopo Nala, Mgodi wa Hussein Pilly uliopo Tambi (Wilaya ya Mpwapwa) na Mgodi wa Canada uliopo Chamkoroma (Wilaya ya Kongwa) ambapo yamewezeshwa na Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa kushirikiana na Tume ya Madini. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, Mhandisi Chacha Megewa kutoka Tume ya Madini ameeleza kuwa ni muhimu kwa wachimbaji kufanya kazi katika mazingira salama kwa kutumia vifaa kinga kama kofia ngumu, reflekta, buti, gloves na barakoa (maski). "Ulipuaji wa baruti ni mojawapo ya shughuli hatarishi migodini, hii...

DKT BITEKO MGENI RASMI NISHATI BONANZA 2025

Image
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe Dkt Doto Biteko anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika  Bonanza la Wizara ya Nishati na Taasisi zake litakalofanyika jumamosi Juni  28, 2025  jijini Dodoma. Akizungumzia maandalizi ya Bonanza  hilo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Nishati, Bi. Neema Mbuja amesema kuwa, Nishati Bonanza litafanyika kwenye Viwanja vya Jamhuri mjini Dodoma na kushirikisha taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati na wadau kutoka Wizara nyingine. ‘’ Nipende kuchukua fursa hii kuzikaribisha taasisi zilizo chini ya  Wizara ya Nishati  kushiriki kikamilifu  bonanza ambalo linaleta fursa ya kufahamiana na kubadilishana mawazo baada ya muda wa kazi pamoja na  kufanya mazoezi ili kujenga afya." Amesema Mbuja Ameongeza kuwa, kwa  mwaka huu Nishati Bonanza  linaongozwa na kauli mbiu ya "Michezo kwa Afya bora, Shiriki uchaguzi 2025 ikiwa na lengo pia la kuhamasisha wafanyakazi na wananchi kwa ujumla kutumia ...

RAIS SAMIA AMELITENDEA HAKI TAIFA - SPIKA DKT. TULIA

Image
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ametoa pongezi za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa uongozi wake thabiti na wenye maono, ambao umeleta mageuzi ya kweli ya maendeleo kwa Taifa. Akizungumza leo Alhamisi, tarehe 26 Juni 2025, wakati wa kuhitimisha Mkutano wa 19 wa Bunge la Kumi na Mbili, Dkt. Tulia amesema kuwa katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wake, Rais Samia amelihudumia Taifa kwa haki kwa kuhakikisha utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo, ustawi wa jamii na kuimarika kwa huduma za msingi kwa wananchi. Akitaja baadhi ya mafanikio makubwa yaliyopatikana chini ya uongozi wa Rais Samia, Dkt. Tulia alieleza kuwa Serikali imefanikiwa kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati, ikiwemo Ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Dar es Salaam kupitia Morogoro hadi Dodoma, Ujenzi wa Daraja la JP Magufuli (Kigongo–Busisi) mkoani Mwanza, Mradi wa kuzalisha ...

UTABIRINWA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO

Image
Date:  June 25, 2025 Author:  mtezamedia 0 Share this:   X   Facebook Utabiri wa Hali ya Hewa kwa saa 24 zijazo Januari 25/2025. January 25, 2025 In "Social" Utabiri wa Hali ya Hewa kwa saa 24 zijazo Machi 25/2025. March 25, 2025 In "Social" Utabiri wa Hali ya Hewa kwa saa 24 zijazo Februari 25/2025. February 25, 2025 In "Social" Post navigation PREVIOUS Previous post: Tanzania itaendelea kuweka kipaumbele kwenye Madini mkakati-Mbibo. NEXT Next post: Mbunge Mavunde akabidhi jengo la kupumzikia wananchi Hospitali ya rufaa ya Dodoma. LEAVE A COMMENT Search for: Search ARCHIVES June 2025  (157) May 2025  (185) April 2025  (178) March 2025  (198) February 2025  (146) January 2025  (150) December 2024  (166) November 2024  (180) October 2024  (184) September 2024  (139) August 2024  (113) July 2024  (143) June 2024  (105) May 2024  (98) April 2024  (116) March 2024  (116) February 2024  (...