Posts

Showing posts from September, 2024

HESLB,TRA WABADILISHANA HATI ZA USHIRIKIANO

Image
  Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu(HESLB) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) leo Septemba 13,2024 Wamebadilishana za ushiriakiano baina yao kwa lengo la kuboresha huduma kwa Watanzania. Akizungumza wakati wa Hafla hiyo fupi ya kubadilishana hati ya ushirikiano na wadau wa kimkakati,Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bill Kiwia amesema TRA ina jukumu la kuwatambua watu waliokatika Sekta mbalimbali hivyo ni furs adhimu kwetu kushirikiana nao kimkakati. Kiwia Amesema kuwa kuna malengo makuu mawili ambayo yamewafanya kushirikiana na TRA ambalo lengo lake ni kuweza kuwafikia wanufaika wote ambao wana kipato na kuwatafuta hasa kwenye sekta zisizo rasmi pamoja na kuwafikia Watanzania kwa ujumla kwa lengo la kuboresha huduma zao. Kwa upande wake Mkurugenzi wa TRA Yusuph Mwenda ameipongeza HESLB kwa kazi kubwa ya kutoa mikopo ambayo imekuwa na wanufaika wengi na hii ni kwa sababu ya watanzania wanaolipa kodi ambayo inaenda kuwasaidia watoto na ndugu zao ambao wanasoma. Aidha amewapongeza Watanz...

NLD KUENDESHA KAMPENI ZA UCHAGUZI KWA AMANI

Image
  Kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Novemba, Chama cha National League for Democracy (NLD),  Kimesema kuwa kitaendesha  Kampeni za Chama  hicho Kwa njia ya amani.  Akizungumza kwenye Kikao Cha ndani na Viongozi wa Chama hicho kutoka Chaani Zanzibar,Katibu wa Uenezi na Itikadi wa Chama hicho, Ahmed Hamad,amewataka viongozi wa NLD Zanzibar kuongozwa na busara wanapoeneza sera na itikadi ya chama cha NLD, Alisisitiza.  "Chama cha NLD kitaendesha kampeni za busara, kuepuka uchochezi, udanganyifu, au vurugu, na badala yake tutaweka msisitizo kwenye hoja na sera, kwani NLD ina sera nzuri kuliko chama chochote nchini." Aidha Hamad aliwahimiza viongozi wa NLD kuhakikisha wanajenga mahusiano bora na wananchi wa ngazi za chini huku akitaka Viongozi hao kutatua Changamoto za wananchi kupitia Sera za Chama hicho. Chama cha NLD kipo kwenye Ziara ya siku nne visiwani Zanzibar, inayoongozwa na Katibu Mkuu wa NLD, Mhe. Doyo Hassan Doyo, Ziara hiyo inashirikisha viong...

MWENYEKITI NLD AWATAKA WANACHAMA KUMUUNGA MKONO DOYO

Image
Wanachama wa Chama cha National League for Democracy (NLD), wameombwa kumuunga mkono Katibu Mkuu  Doyo Hassan Doyo kwani ni mtu muadilifu na mtendaji mzuri wa kazi ili kuleta mabadiliko na maendeleo ndani ya chama hicho   Hayo yamesemwa Septemba 11, 2024  na Mwenyekiti wa Chama hicho Mfaume Khamis Hassan wakati alipokuwa akizungumza na Wanachama na kusema kuwa ili kuleta mabadiliko na Maendeleo kwenye chama ni muhimu kumuunga mkono na kusimama nae kwa pamoja   "Hakuna chama chochote kinachoweza kumkataa mtu kama Doyo, mtu mwenye historia ya utendaji bora katika siasa za nchi hii."  Amesema Hassan   Mwenyekiti wa NLD, Katibu Mkuu wa Chama hicho walifanya kikao cha ndani na baadhi ya wanachama wa chama hicho upande wa Zanzibar, ambapo wote kwa pamoja walitoa mwito wa kuimarisha ujenzi wa chama na ushirikiano kati ya wanachama wa NLD kutoka Bara na Zanzibar. Katika ziara hiyo, Doyo ameambatana na viongozi mbalimbali wa chama hicho kutoka upande wa Bara n...

UDART,DART ZATAKIWA KUSHIRIKIANA KUTATUA KERO USAFIRI WA MWENDOKASI

Image
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mohamed Mchengerwa, amewaagiza Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART) na Wakala wake (DART) kushirikiana kwa pamoja kwa ili kuweza kuhakikisha kuwa  changamoto zote zilizopo kwenye usafiri wa huo ili kuwawezesha wananchi kusafiri kwa raha. Mchengerwa ametoa maagizo hayo leo jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa Mageti Janja na Kadi Janja ambazo zitatumika kufanya malipo ya nauli katika usafiri wa mabasi yaendayo haraka hali itakayosaidia kujibu maswali ya watanzania kuhusu changamoto za usafiri wa mwendo kasi. Awali akizungumzia uzinduzi wa Mageti janja na Kadi Janja, amesema pongezi ziende kwa Dart kutokana na kuja na mfumo huo ambao unakwenda kujibu maswali ya namna ya ukusaji nauli kwa kuachana na karatasi na kuanzia kesho kadi zitaanza kutumika ni mapinduzi makubwa katika huduma uya usafiri. Ameongeza kuwamfumo huo wa kutumia kadi unafanya usafiri wa mwendokasi kuwa katika kiwango cha juu, “...