Posts

Showing posts from September, 2025

DKT.YONAZI TUIMARISHE LISHE,TUPUNGUZE MAGONJWA SUGU

Image
KATIBU Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi amewataka wadau kushirikiana na Serikali katika kuimarisha hali ya lishe nchini ili kupunguza kasi ya kuenea kwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza. Amesema ulaji usio faa na mitindo mibaya ya maisha vimechangia kuongezeka kwa magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza jambo linalohatarisha maendeleo ya Taifa. Dkt. Yonazi ameyasema hayo jijini Dar es salaam leo 29 Septemba, 2025 katika Mkutano Mkuu wa 11 wa Wadau wa Lishe unaoendelea katika kituo cha mikutano cha APC Bunju.    Dkt. Yonazi amesema tafiti zinaonesha kuwa uzito uliozidi na uliokithiri ni chanzo kikuu cha magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza yakiwemo  kisukari, moyo, figo na baadhi ya saratani. “Napenda kukumbusha wadau, taasisi na wataalam kushirikiana na serikali kufanya tafiti zitakazosaidia kuleta majibu ya changamoto za lishe, pamoja na kusaidia watu kubadili tabia za ulaji na mtindo wa maisha ili kuzuia magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza yanayo...

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO

Image
 

MAJALIWA: RAIS SAMIA NI MAMA WA MAENDELEO

Image
-Amnadi Chande ambaye ni mgombea ubunge Jimbo la Kojani -Asema Dkt. Mwinyi ni Daktari wa Maendeleo Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kuthibitisha kuwa ni mama wa maendeleo kwa kusimamia utekelezaji wa miradi mikubwa ya kijamii na kiuchumi nchini. Akihutubia wananchi wa Jimbo la Kojani, Pemba Jumamosi (Septemba 27, 2025), Majaliwa amesema Serikali ya Awamu ya Sita imefanikisha ujenzi wa vituo vya afya vyenye uwezo wa kutoa huduma zote za msingi, hali iliyopunguza adha ya wananchi kusafiri umbali mrefu kufuata huduma hizo.  “Kwa sasa wananchi hawaendi umbali mrefu kupata huduma za afya, wataalamu wa afya wameajiriwa,” alisema. Alibainisha kuwa Rais Dkt. Samia ametekeleza pia maono yake ya kummtua mama ndoo kichwani kupitia utekelezaji wa miradi mikubwa, ya kati na midogo ya maji, sambamba na kuvutia wawekezaji waliowekeza katika miradi mikubwa iliyotoa ajira kwa Watanzania. Majaliwa a...

DR. ABBASI INVITES PRIVATE SECTOR TO INVEST IN SWAGASWAGA GAME RESERVE

Image
The Permanent Secretary of the  Ministry of Natural Resources and Tourism , Dr. Hassan Abbasi, has invited the private sector to invest in protected areas across the country, including the Swagaswaga Game Reserve, which serves as a tourism hub in Dodoma City. Dr. Abbasi made the remarks on September 26, 2025, during his official visit to the Swagaswaga Game Reserve, which spans across the Dodoma and Singida regions. “We have set aside investment areas within the reserves, so we welcome the private sector to collaborate with us,” said Dr. Abbasi. He also commended the Tanzania Wildlife Management Authority (TAWA) for developing initial infrastructure in the Swagaswaga Game Reserve, including the construction of tourist hostels, offices, staff houses, and access roads. He further emphasized that the Ministry will continue allocating funds to enhance tourism infrastructure in protected areas. Earlier, while welcoming Dr. Abbasi, the Acting Conservation Commissioner of TAWA, Mlage Yuss...

INEC YASITISHA UCHAGUZI JIMBO LA FUONI KUFUATIA KIFO CHA MGOMBEA WA CCM JIMBO HILO

Image
Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imesitisha uchaguzi wa ubunge katika Jimbo la Fuoni, Wilaya ya Magharibi B, Zanzibar kufuatia kifo cha mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abass Ali Mwinyi. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo hilo, Miraji Mwadini Haji, kusitishwa huko kumetokana na taarifa rasmi iliyowasilishwa kwa Tume na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar kwa barua yenye Kumb. Na. CCM/AKZ/U30/22/VOL XIV/109 ya tarehe 25 Septemba 2025. To Kwa mujibu wa kifungu cha 71 cha Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani Na. 1 ya mwaka 2024, Tume itapanga tarehe mpya ya uteuzi wa wagombea na kuanzisha upya mchakato wa uchaguzi katika jimbo hilo, kwa notisi itakayotolewa kupitia Gazeti la Serikali. Msimamizi wa Uchaguzi ameeleza kuwa wagombea waliokwishaidhinishwa awali wataendelea kubaki kwenye orodha, isipokuwa iwapo mgombea atajitoa, na kusisitiza kwamba hakutakuwa na kampeni zozote za ubunge katika Jimbo la Fuoni mpaka mgombea mpya atakapoteuliwa.

MWENYEKITI INEC AKAGUA MAANDALIZI YA UCHAGUZI MKUU CHAMWINO,MTERA

Image
  Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Rufani Jacobs Mwambegele leo Septemba 25, 2025 ametembelea  Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma  katika majimbo ya Chamwino na Mtera ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya kukagua maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 ambapo pamoja na mambo mengine alipokea taarifa ya majimbo hayo kutoka kwa msimamizi wa Uchaguzi wa Halmashauri kuhusu maandalizi ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani wa Mwaka 2025 na kisha kukagua vifaa ambavyo tayari vimepokelewa katika Halmashauri hiyo.   Kwa mujibu wa ratiba iliyotangazwa na Tume, Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 unatarajiwa kufanyika Oktoba 29, mwaka huu. "Kura Yako Haki Yako Jitokeze Kupiga Kura"

DKT. YONAZI ATOA WITO WATUMISHI KUBEBA MAONO YA DIRA YA TAIFA 2050

Image
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonazi, ametoa wito kwa Viongozi, Menejimenti na Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu na taasisi zake kubeba malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 kama sehemu ya wajibu wao wa kitaifa ili kuweza kufikia maono yaliyopo kufikia mwaka 2050.   Dkt. Yonazi ametoa wito huo wakati ufunguzi wa Kikao cha Mazingativu ya Menejimenti, Wakuu wa taasisi na Watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu na taasisi zake kinachofanyika leo Septemba 25, 2025 Jijini Arusha.   “Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 tayari imeshazinduliwa, Dira hii ni ramani ya mustakabali wa nchi yetu, ikitupa taswira ya nchi ambayo tunaihitaji kuwa nayo katika ndani ya miaka 25 ijayo, ili kufanikisha maono haya kila mmoja wetu anawajibu na anajambo la kulifanya, ni wajibu wetu kujiuliza kwamba nitachangia nini kuhakikisha nchi yangu inafikia maono haya kufikia mwaka 2050” ameeleza Dkt. Yonazi.   Aidha, amebainisha kuwa, kila mmoja mah...

MGOMBEA URAIS CUF ATAKA AMANI, AAHIDI MABADILIKO MAKUBWA

Image
Na Woinde Shizza, Arusha  - Mgombea urais kupitia Chama cha Wananchi (CUF) Samandito Gombo ameendelea na kampeni zake jijini Arusha, akifanya mkutano mkubwa katika eneo la Morombo ambapo amewataka wananchi kulinda amani na mshikamano wa taifa, huku akihimiza wajitokeze kwa wingi kupiga kura Oktoba 29 mwaka huu. Akihutubia umati wa wafuasi na wananchi wa eneo hilo, mgombea huyo alisema kura za wananchi ni chachu ya mabadiliko na maendeleo ya kweli, akisisitiza kuwa taifa linahitaji viongozi wapya wenye maono mapya ya kuwaletea wananchi nafuu ya maisha. “Mimi nawaomba Watanzania wenzangu, tuendelee kulinda amani ya nchi yetu, amani ni nguzo ya maendeleo, na ninawaomba mkanichague ili kwa pamoja tulete mabadiliko makubwa yatakayogusa kila sekta ya maisha,” alisema. Aliahidi kusimamia uchumi kwa kupunguza gharama za maisha, kupambana na mfumuko wa bei na kuhakikisha wananchi wananufaika moja kwa moja na rasilimali za taifa, Vilevile, alisema kilimo kitawekwa kipaumbele ili wakulima wap...

MAKAMU WA RAIS AFANYA MAZUNGUMZO NA MKURUGENZI MTENDAJI WA MFUKO WA HASARA NA MAAFA

Image
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Hasara na Maafa kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi (Loss and Demage Fund) Ibrahima Diong, mazungumzo yaliyofanyika pembezoni mwa Kikao cha 80 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Jijini New York nchini Marekani.   Mazungumzo hayo yamelenga masuala mbalimbali yahusuyo mabadiliko ya tabianchi na athari zake kwa mataifa ya Afrika ikiwemo Tanzania. Pia ukusanyaji wa fedha kwaajili ya mfuko huo na hivyo kuziunga mkono nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania ambazo zinaendelea kuchukua hatua ya kukabiliana na madhara yanayosababishwa na mabadiliko ya tabianchi licha ya uhaba wa fedha.   Mfuko Mfuko wa Hasara na Maafa kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi (Loss and Damage Fund), ni utaratibu wa fedha ulioundwa ili kutoa msaada wa kifedha kwa nchi zinazoendelea ambazo zinakabiliwa na athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi. Athari hizo ...

KAMANDA MULIRO AFANYA UKAGUZI

Image
Picha mbalimbali katika ukaguzi wa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam SACP Murilo Jumanne Murilo leo Septemba 24, 2025 Mkoa wa Kipolisi Ilala. Kamanda Murilo ameanza ukaguzi katika Mkoa wa Ilala kwa mujibu wa kanuni za Jeshi la Polisi ili kuhakikisha huduma bora za usalama zinaendelea kutolewa kwa wakazi wa Jiji la Dar es Salaam

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO

Image

SERIKALI YAONDOA VAT KWA VITUO VYA GESI ASILIA ILIYOSHINDILIWA (CNG)

Image
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mha. Felchesmi Mramba amesema  Serikali imeondoa kodi ya ongezeko la thamani  (VAT) kwa vituo vyote vya Gesi iliyoshindiliwa (CNG) nchini  ili kuhamasisha matumizi ya gesi asilia  kwenye vyombo vya moto kupitia uwepo wa vituo vingi vya kutoa huduma hiyo kwa wananchi.  Amesema kuwa Serikali pia imeondoa kodi kwenye vifaa vya kuwekea mifumo hiyo ya gesi  kwenye vyombo vya moto kama vile magari na bajaji ikiwa ni hatua pia ya kuhamasisha matumizi ya gesi asilia katika vyombo vya moto. Mhandisi Mramba ameeleza hayo leo Septemba 24, 2025 jijini Dar es Salaam wakati  akizindua kituo cha Gesi Asilia iliyoshindiliwa (CNG) cha  kampuni ya Puma Energy kilichopo Bagamoyo road.  " Serikali inafanya jitihada hizi ili kutoa nafasi kwa watanzania kutumia gesi kwenye vyombo vyao vya moto kwa kurahisisha mazingira ya upatikanaji wake na pia kwa kuwa kuna unafuu wa gharama pale unapotumia  Gesi Asilia ikilinganishwa na ma...