Posts

Showing posts from October, 2024

TMA YAWAPA TAHADHARI WAKULIMA,WAFUGAJI

Image
Wakulima na Wafugaji Nchini wameshauriwa kutumia taarifa sahihi kutoka kwa maafisa ugani kwa kuzingatia utabiri wa wilaya husika katika kuchagua mbegu na zao sahihi kulingana na utabiri wa msimu.  Wito huo umetolewa leo Oktoba 31,2024 Jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (IPCC), Dkt. Ladislaus Chang'a wakati akitoa taarifa ya mwelekeo wa mvua za Msimu wa Novemba, 2024 hadi Aprili 2025. Amesema kuwa  Mvua hizo zimeanza katika baadhi ya maeneo ya ukanda wa Ziwa Victoria na pwani ya kaskazini kama ilivyotabiriwa nakwamba maeneo ya nyanda za juu kaskazini mashariki yameendelea kutawaliwa na vipindi virefu vya ukavu.  Aidha,meendelea kufafanua kuwa utabiri wa mvua za Vuli unatarajiwa kuendelea kama ulivyotabiriwa ambapo Mwelekeo wa mvua za Msimu wa Novemba, 2024 hadi Aprili, 2025, Mvua hizo ni mahususi katika maeneo ya ma...

SERIKALI KUJA NA MRADI WA KUIMARISHA UPATIKANAJI UMEME VITONGOJINI- MHE. KAPINGA

Image
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe Judith Kapinga amesema Serikali inatarajia kuanza mradi mpya wa upelekaji umeme  vitongojini utakaohusisha ujenzi wa njia za kati na ndogo za kusafirisha umeme.  Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Oktoba 31, 2024 bungeni jijini Dodoma  wakati akijibu swali la Mhe. George Mwanisongole, Mbunge wa Mbozi aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itaanza kupeleka umeme mkubwa kwenye Vitongoji ambavyo havijapata umeme mkubwa na hivyo kukosa sifa ya kuwepo kwenye miradi ya maendeleo.  "Kwenye mradi huu utakaoanza Desemba 2024 tumeboresha zaidi kwani tutakuwa na transfoma zenye ukubwa wa KVA 50, 100 na 200 kulingana na ukubwa wa Kitongoji." Amesema Mhe. Kapinga Ameongeza kuwa, maeneo ya Vitongoji ambayo hayakunufaika na mradi wa awali wa vitongoji 15 yatanufaika kwa mradi utakaoanza Desemba 2024. Akijibu swali la Mbunge wa Iringa Mjini, Mhe. Jesca Msambatavangu aliyeuliza ni lini Serikali itatekeleza ahadi ya umeme jazilishi maeneo ya Miji yenye sura za V...

NAIBU KATIBU MKUU UCHUKUZI ATEMBELEA OFISI ZA TMA

Image
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Ndg. Ludovick Nduhiye amefanya ziara ya kutembelea ofisi za Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) zilizopo katika jengo la Ubungo Plaza, Dar es Salaam ikiwa ni moja ya malengo yake ya kuzitambua Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Uchukuzi, kufahamu majukumu ya kiutendaji na kuelewa changamoto zinazowakabili na Mikakati ya kuimarisha Taasisi na utoaji wa huduma. Baada ya taarifa ya utendaji kutoka TMA, Naibu Katibu Mkuu, Uchukuzi aliipongeza TMA kwa kuendelea kuimarisha na kuboresha huduma za haki ya hewa nchini, ikiwemo kuongeza usahihi wa utabiri,  akieleza kuwa yeye ni mmoja wa wadau wa Mamlaka na anafuatilia, kuzingatia na kutumia taarifa za hali ya hewa. Kiuekweli taarifa zenu ni nzuri, niwapongeze sana TMA, mimi ni mdau wa taarifa zenu na nimekuwa nikizifuatilia, kuzizingatia na pia kuzitumia, naweza kusema TMA ya sasa si kama ile za zamani." Alisisitiza Ndg. Nduhiye. Aidha, akiwasilisha awali salamu za ukaribisho Kaimu Mkurugenzi Mkuu w...

NI DHAMIRA YA SERIKALI KULIPA FIDIA WANANCHI WANAOPISHA MIRADI YA MAENDELEO- MHE. KAPINGA

Image
Naibu Waziri Nishati, Mhe Judith Kapinga amesema ni dhamira ya Serikali kuhakikisha kuwa wananchi wote wanaopisha miradi ya maendeleo wanalipwa fidia   kulingana na taratibu zilizopo. Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Oktoba 30, 2024 bungeni jijini Dodoma  wakati akijibu swali la Mhe. Silvestry Koka, Mbunge wa Kibaha Mjini aliyetaka kufahamu ni lini Serikali italipa fidia kwa Wananchi na kampuni zipatazo 18 zilizopo kwenye eneo la viwanda la Zegereni Mji wa Kibaha mkoani Pwani ambao wamepitiwa na njia ya umeme ya kV 400. Mhe. Kapinga  ameeleza kuwa,  Serikali imelipa fidia  awamu ya kwanza kwa takriban shilingi bilioni 29.4 kati ya shilingi Bilioni 33 zinazotakiwa kulipwa kwa wananchi wanaopisha mradi huo wa njia ya kusafirisha umeme msongo wa Kilovoti 400 kutoka Chalinze hadi Mkuranga mkoani Pwani. "Katika eneo la viwanda la Zegereni kuna wananchi na kampuni 18 ambao wanadai fidia yenye thamani ya Shillingi billioni 1.1. Serikali inaendelea kulipa fidia hizi...

VIJIJI VYOTE NEWALA VIMEFIKIWA NA UMEME - MHE. KAPINGA.

Image
  Naibu Waziri Nishati, Mhe Judith Kapinga amesema Vijiji vyote 76 vya Jimbo la  ya Newala Vijijini Mkoa wa Mtwara vimefikiwa na huduma ya umeme kwa umbali wa kilometa 1.  Mhe. Kapinga ameyasema hayo leo Oktoba 29, 2024 Bungeni Jijini Dodoma  wakati akijibu swali la Mhe. Maimuna Mtanda Mbunge wa Newala Vijijini aliyetaka kufahamu lini Serikali itaanza ujenzi wa nguzo za Kilomita 2 katika Vijiji ambavyo mradi wa  REA mzunguko wa Pili unatekelezwa. "Kwa nyongeza ya umbali wa kilomita 2, REA kupitia Mkandarasi Central Electrical International Limited anaendelea na kazi na amefanikiwa kufikisha umeme kwenye vijiji 32 kati ya vijiji 76. Vijiji vilivyosalia vinatarajiwa kukamilika hivi karibuni", Amesema Mhe. Kapinga Akijibu swali la Mbunge wa Kilombero, Mhe. Abubakar Asenga aliyeuliza lini Serikali itaunganisha umeme katika Kitongoji cha Upendo, Tupendane, Ikwambi na Misheni katika mji wa Ifakara,  Mhe. Kapinga amesema vijiji hivyo vipo katika mradi wa vitongoji...

DKT BITEKO ATAKA UMOJA,USHIRIKIANO NA UBUNIFU TAASISI ZA NISHATI

Image
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka Watendaji na Watumishi katika Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati kuwa na umoja, ushirikiano na ubunifu ili kusogeza huduma bora kwa wananchi ikiwemo za umeme, mafuta, na Nishati Safi ya Kupikia. Amesema hayo tarehe 28 Oktoba, 2024 jijini Dodoma wakati wa Kikao chake na Menejimenti ya Wizara ya Nishati na Taasisi zilizo chini yake ambacho ni cha pili kutoka uanzishwe mfumo mpya ndani ya Wizara na Taasisi zake wa kujifanyia tathmini ili kuona namna inavyofanya kazi ya kuhudumia wananchi. “Ikumbukwe kuwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wote amekuwa akisisitiza kuwepo na ubunifu kwenye Wizara na Taasisi ili kusogeza huduma za uhakika kwa wananchi na huduma hizo bora haziwezi kutokea kama hakuna umoja na ushirikiano ndani ya Taasisi za Serikali.” Amesema Dkt. Biteko Katika Kikao hicho, Dkt. Biteko amewataka watendaji wa Wizara na Taasisi kufanya kazi kwa bidii na weledi huku wakimuangalia mtanzania wa kawai...

WASHIRIKI WA KONGAMANO LA JOTOARDHI AFRIKA WATEMBELEA VYANZO VYA JOTOARDHI MBEYA

Image
  Picha mbalimbali zikionesha Washiriki wa Kongamano la Kimataifa la Jotoardhi Afrika (ARGeo-C10) wakitembelea vyanzo vya nishati ya Jotoardhi nchini. Washiriki hao kutoka ndani na nje ya nchi wametembelea maeneo ya Ngozi na Kiejo-Mbaka mkoani Mbeya ikiwa ni sehemu ya programu za Kongamano la Siku Saba la ARGeo-C10 ambalo pia lililenga kutangaza hazina ya Jotoardhi iliyopo Tanzania ili kuvutia uwekezaji.

TUNAIMARISHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NA MIUNDOMBINU YA NISHATI ILI KUFIKISHA HUDUMA KWA WOTE- DKT.MATARAGIO

Image
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati,  Dkt. James Mataragio amesema Serikali inaendelea kuimarisha mazingira ya uwekezaji  na miundombinu ya Sekta ya Nishati nchini ili  kuwezesha wananchi kufikiwa na huduma stahiki bila kujali umbali na vipato vyao. Dkt. Mataragio ameyaeleza hayo  jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya utoaji Tuzo kwa Mawakala na Wadau wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania ambayo  inaunga mkono juhudi za Serikali za kuelimisha jamii kuhusu matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kupitia bidhaa za Puma Gas. Dkt. Mataragio amesema  moja ya majukumu ya Wizara ya Nishati ni kukutana na wadau mbalimbali wakiwemo watoa huduma na watumiaji ili kuimarisha ushirikiano kati ya  sekta binafsi na Serikali utakaopelekea utoaji wa huduma bora kwa wananchi  ikiwa ni moja ya vipaumbele vya Serikali. Katika hafla hiyo,  Dkt.Mataragio ameipongeza  kampuni ya Puma  kwa jitihada  zinazounga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali katika ...

CHUO CHA MIPANGO YA MAENDELEO VIJIJINI CHATOA VIFAA VYA KISASA KWA WAKULIMA WA MWANI

Image
   Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini imetoa vifaa kwa kwa vikundi vya  wanawake na vijana wanaojishughulisha na kilimo cha mwani ili waweze kuongeza thamani ya zao hilo na kukuza kipato chao. Akikabidhi vifaa hivyo leo Jijini  Dar es salaam Octoba 25, 2024 Mkurugenzi Mkazi wa shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa(UNDP) Tanzania Shigeki Komatsubara amesema UNDP itaendelea kutoa msaada kwa wanawake na vijana wanaojishughulisha na kilimo cha mwani ili kukuza sekta ya uchumi wa bluu. "Ufadhili wa vifaa hivi ni sehemu ya utekelezaji wa agenda ya kimataifa ya uchumi wa bluu,Tanzania ni miongoni mwa nchi  zinazopiga hatua kubwa kwenye uchumi wa bluu katika sekta ya mwani "amesema Komatsubara  Awali Naibu katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Dkt Edwin Mhede amesema suala la kuchagiza maendeleo ya Uvuvi na Kilimo cha mwani ni utekelezaji wa azimio namba 14 la Maendeleo endelevu ya Dunia,kwamba ifikapo mwaka 2030 tuwe tumepiga hatua,nakwamba  ...

UJENZI BOMBA LA MAFUTA GHAFI LA EACOP WAFIKIA ASILIMIA 43.5

Image
  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Mussa Makame amesema utekelezaji wa mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki ( EACOP), umefikia asilimia 43.5 huku baadhi ya kazi za ujenzi katika makambi na vituo vya kuhifadhia mabomba zikikamilika kwa asilimia 100. Amesema hayo leo wakati akitoa taarifa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Chongoleani Tanga, Tanzania.  "Kazi za mradi wa EACOP zinahusisha ujenzi wa bomba la urefu wa kilomita 1,443 na miundombinu mingine huku kilomita 1,147 sawa na asilimia 80 zikiwa upande wa Tanzania." Amesema Makame Ameeleza kuwa, ujenzi wa kiwanda cha kuweka mfumo wa joto kwenye mabomba (thermal Insulation System Plant - TIS) umefikia asilimia 92. Ameongeza kuwa, bomba litapita katika Mikoa nane ya Kagera, Geita, Shinyanga, Tabora, Singida, Dodoma, Manyara na Tanga. Amesema bomba hilo l...

SERIKALI ITAENDELEA KUSHIRIKISHA WAWEKEZAJI UENDELEZAJI NISHATI JADIDIFU- DKT.MATARAGIO

Image
  Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio amesema Serikali itaendelea kuwashirikisha wawekezaji katika maeneo yenye nishati jadidifu ili kuyaendeleza na hivyo  kuwezesha azma ya nchi kuwa na umeme unaotokana na  vyanzo mchanganyiko. Amesema hayo jijini Dodoma  wakati Wizara ya Nishati ikiwasilisha taarifa kuhusu utekelezaji wa miradi ya Nishati Jadidifu  inayotokana na Jotoardhi, Upepo na Jua kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini. "Tumeshayatambua maeneo ambayo nishati jadidifu inapatikana, kwa upande wa Jotoardhi tunaendelea na uhakiki wa rasilimali hiyo ambayo inahusisha uchorongaji wa visima." Amesema Dkt. Mataragio  Dkt.Mataragio amesema Nishati Jadidifu kama Jotoardhi, Jua na Upepo ni miongoni mwa nishati safi ambazo zinaendana na malengo ya dunia ya kupunguza uzalishaji wa hewa  ya ukaa. Awali,  Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga alisema rasilimali ya Jotoardhi ni jadidifu na endele...

TANZANIA KUJIFUNZA TEKNOLOJIA YA MAGARI YA UMEME SINGAPORE - DKT. BITEKO

Image
  Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Biteko, amesema kuwa Tanzania inayo nafasi kubwa ya kujifunza Teknolojia ya uwambaji wa magari (Assembling) yanayotumia umeme kutoka kiwanda cha magari cha HYUNDAI kwani ni rafiki kwa mazingira na hupunguza uchafuzi wa hali ya hewa. Dkt. Biteko ameyasema hayo leo Oktoba 23, 2024 nchini Singapore mara baada ya kutembelea kiwanda hicho ikiwa ni ziara mojawapo kwenye mkutano wa Wiki ya Nishati nchini Singapore na kusema kuwa Teknolojia kama hizi zina mchango mkubwa kwenye kuinua uchumi wa nchi na kuongeza pato la Taifa. ‘’ Nawapongeza sana wenzetu hasa kwa Teknolojia na ubunifu wa haya magari pamoja na Teknolojia ya Kilimo janja (smart farm) ambapo kwanza inatumia nafasi ndogo lakini matokeo yake ni makubwa sana’’ Alisema Dkt. Biteko. Kuhusu Teknolojia ya kilimo janja ambacho kinaendeshwa na kampuni ya ubunifu ya HYUNDAI kwa kutumia Teknolojia mnemba (Robot) Dkt. Biteko amesema, uwepo wa Teknolojia kama hii unaongeza tija, inapun...

KONGAMANO LA ARGeo-C10 LINALENGA KUONGEZA KASI YA UENDELEZAJI JOTOARDHI AFRIKA- DKT. MATARAGIO

Image
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dkt. James Mataragio, amesema kuwa moja ya malengo ya Kongamano la Kimataifa la Jotoardhi (ARGeo-C10) linalofanyika nchini Tanzania ni kuwezesha Afrika kuongeza kasi ya uendelezaji wa rasilimali ya Jotoardhi. Amesema rasilimali ya Jotoardhi ikiendelezwa ipasavyo barani Afrika itaweza kutumika kwa namna mbalimbali ikiwemo kuzalisha umeme pamoja na matumizi mengine ya moja kwa moja kwenye Sekta ya Kilimo na Ufugaji. Dkt. Mataragio amesema hayo jijini Dar es Salaam katika hafla ya ufungaji wa mafunzo ya Jotoardhi kwa washiriki wa Kongamano la Kimataifa la ARGeo-C10 linaloendelea jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya programu za kongamano hilo. “Tanzania ina maeneo mengi yaliyotambuliwa yenye viashiria vya Jotoardhi na tayari Kampuni ya Uendelezaji wa Jotoardhi (TGDC) inaendelea na shughuli za utafiti katika maeneo mbalimbali ikiwemo Songwe, Kiejo-Mbaka na Ngozi.” Amesema Dkt.Mataragio Ameeleza kuwa, kwa Tanzania kuweka mkazo kwenye uzalishaji wa u...