Watumishi wa Wizara ya Madini na Taasisi zake wamehimizwa kufanya mazoezi ya mwili mara kwa mara kama njia ya kuimarisha afya, kujenga mshikamano na kuongeza tija katika utekelezaji wa majukumu ya kazi. Wito huo umetolewa leo Januari 24, 2026 jijini Dodoma na Waziri wa Madini, Mhe. Anthony Mavunde, alipofungua Bonanza la tatu la michezo lililowakutanisha watumishi wa Wizara ya Madini na Taasisi zake, ikiwemo Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST), Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), Tume ya Madini pamoja na Taasisi ya Uwazi na Uwajibikaji katika Rasilimali Madini, Mafuta na Gesi Asilia (TEITI). Akizungumza katika uzinduzi wa bonanza hilo, Mhe. Mavunde amesema kuwa, mazoezi ya viungo ni nguzo muhimu ya afya njema kwa mtumishi, ufanisi na tija kazini hivyo kuna umuhimu wa watumishi kujitokeza kwa wingi katika shughuli za michezo ili kuimarisha afya zao na kuendeleza mshikamano kazini. Aidha, Waziri Mavunde amezitaka taasisi zote zilizo chini ya Wizara ...