Posts

Showing posts from August, 2024

RAIS MWINYI ASHIRIKI MAZIKO YA MVITA KABENDERA

Image
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi amewaongoza wananchi na viongozi mbalimbali katika mazishi ya Mwanasiasa mkongwe, marehemu Mvita Mussa Kibendera, aliyefariki jana tarehe: 26 Agosti 2024.  Marehemu Mvita Mussa Kibendera amezikwa leo, tarehe: 27 Agosti 2024, katika Makaburi ya Mwanakwerekwe. Mapema, Alhaj Dk. Mwinyi alijumuika na waumini wa dini ya Kiislamu katika sala ya maiti iliyofanyika Msikiti wa Mwembeshauri, wilaya ya Mjini, Mkoa wa Mjini Magharibi. Marehemu Mvita Kibendera wakati wa uhai wake aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali katika Chama Cha Mapinduzi na Serikali, ikiwemo Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi, Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Katibu wa CCM Wilaya ya Mjini, na Mwenyekiti wa CCM jimbo la Kikwajuni. Baada ya maziko, Alhaj Dk. Mwinyi alifika nyumbani kwa marehemu Maungani kuwafariji na kuwapa pole wafiwa, na kuwataka kuwa na subira katika kipindi hiki cha msiba mzito. Viongozi mbalimbali walijumuika katika ...

HALMASHAURI YA KIGOMA YAPATIWA MAFUNZO JINSI YA KUKABILIANA NA MAAFA

Image
 Serikali inasimamia na kuratibu shughuli za kuzuia na kukabiliana na majanga kwa kuzingatia Sera ya Taifa ya Menejimenti ya Maafa ya mwaka 2004 na Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na 6 ya Mwaka 2022 na kanuni zake za mwaka 2022 kupitia Idara ya Menejimenti ya Maafa inayotekeleza majukumu yake chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ambapo suala la kuzuia na kukabiliana na majanga ni mtambuka na linahitaji nguvu za pamoja katika kulishughulikia. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya kujenga uelewa juu ya upunguzaji wa madhara ya maafa katika jamii iliyofanyika tarehe 26 agosti, 2024 katika Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, Mkurugenzi Msaidizi  Idara ya Menejimenti ya Maafa sehemu ya Afya Moja  Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Salum Manyatta amesema, kuongezeka kwa matukio ya majanga ambayo yamekuwa yakisababisha maafa na kuathiri mfumo wa kawaida wa maisha ya jamii, Maafa haya yamekuwa yakisababisha madhara mbalimbali ikiwemo vifo, ulemavu wa kudumu, upotevu na u...