Posts

Showing posts from April, 2026

WATENDAJI WA UCHAGUZI WATAKIWA KUSIMAMIA UCHAGUZI KWA WELEDI

Image
  Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakjati akifunga mafunzo ya watendaji wa uchaguzi yaliyofanyika Mkoani Morogoro. Mafunzo hayo yamefungwa leo tarehe 30 Aprili, 2026 na yaliyofanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 28 Aprili, 2026. Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk akizungumza wakjati akifunga mafunzo ya watendaji wa uchaguzi yaliyofanyika Mkoani Morogoro. Mafunzo hayo yamefungwa leo tarehe 30 Aprili, 2026 na yaliyofanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 28 Aprili, 2026. Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa rufani Jacobs Mwambegele akiwa katika ufungaji wa mafunzo hayo.  Na. Mwandishi Wetu, Morogoro Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imetoa wito kwa watendaji wa uchaguzi kuhakikisha wanatumia muda wao kusoma Katiba, sheria za uchaguzi, kanuni na maelekezo ya Tume ili waweze kusimamia uchaguzi kwa w...

WATENDAJI WA UCHAGUZI WATAKIWA KUEPUKA KUFANYA KAZI KWA MAZOEA

Image
Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufaa, Jacobs Mwambegele akizungumza Mkoani Morogoro leo tarehe 28 Aprili, 2026 wakati akifungua mafunzo ya siku tatu kwa  watendaji wa uchaguzi. Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Kisheria wa Tume, Ndg. Cyprian Mbugano akiwasilisha mada kuhusu majukumu ya Watendaji wa Uchaguzi na mambo muhimu ya kuzingatia.  Sehemu ya washiriki ambao ni watendaji wa Uchaguzi kutoka katika Jimbo la Isimani na Kata 12 za Tanzania Bara wakifuatilia hotuba ya ufunguzi. Sehemu ya washiriki ambao ni watendaji wa Uchaguzi kutoka katika Jimbo la Isimani na Kata 12 za Tanzania Bara wakifuatilia hotuba ya ufunguzi. Mkurugenziu wa Ofisi ya Zanzibar, Ndg. Adam Mkina akiwasilisha mada  Meza Kuu ikiwa katika ukumbi wa mafunzo Sehemu ya washiriki ambao ni watendaji wa Uchaguzi kutoka katika Jimbo la Isimani na Kata 12 za Tanzania Bara wakifuatilia hotuba ya ufunguzi. Waratibu wa Uchaguzi wa Mikoa, Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasai...

MAZINGIRA BORA YA ELIMU YAIMARISHWA MBINGA, SHULE YA MASHAUJAA LITEMBO YAZINDULIWA

Image
  Ili kuwawezesha wanafunzi kuingia kikamilifu kwenye ushindani wa maarifa na fikra, ni muhimu kuwaandalia mazingira bora ya kujifunzia pamoja na huduma muhimu zinazochochea upatikanaji wa elimu yenye ubora. Katika kutimiza azma hiyo, Serikali imejenga Shule ya Sekondari Mashujaa Litembo iliyopo Kata ya Litembo, Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma, kwa gharama ya shilingi milioni 701,952,701. Akizungumza na wananchi pamoja na wanafunzi tarehe 26 Aprili 2026 wakati wa uzinduzi wa shule hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Mbinga, Mhe. Kisare Makori, amesisitiza kuwa jukumu la kuwaandaa watoto kwa ajili ya ushindani wa kifikra ni la pamoja kati ya serikali na wazazi. Ameeleza kuwa mazingira bora ya kujifunzia ni msingi muhimu utakaowawezesha wanafunzi kupata maarifa sahihi na kufikia malengo yao kielimu. Aidha, Mhe. Makori amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuwekeza katika sekta ya elimu kwa kutoa fedha zinazowezesha utekelezaji ...

TEEA YAOMBA USHIRIKIANO NA WIZARA YA MADINI KUIMARISHA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

Image
Taasisi ya Wataalamu wa Mazingira Tanzania (TEEA) imeomba kushirikiana kwa karibu na Wizara ya Madini ili kuhakikisha shughuli zote za utafutaji, uchimbaji na uchakataji wa madini nchini zinafanyika kwa kuzingatia misingi ya utunzaji na uendelezaji wa mazingira. Ombi hilo limetolewa leo Aprili 1, 2026, katika ofisi za Wizara ya Madini zilizopo Mtumba jijini Dodoma, ambapo uongozi wa taasisi hiyo umefanya kikao na baadhi ya maafisa wa wizara hiyo kujadili namna bora ya kushirikiana katika kukabiliana na changamoto za kimazingira. Katika kikao hicho, viongozi wa TEEA walitaja maeneo yanayochangia kwa kiasi kikubwa uharibifu wa mazingira kuwa ni pamoja na uchafuzi wa vyanzo vya maji, uharibifu wa ardhi unaotokana na uchimbaji holela, ukataji wa miti bila udhibiti, pamoja na matumizi ya kemikali hatarishi kama zebaki katika shughuli za uchimbaji mdogo. Akizungumza katika kikao hicho, Mwenyekiti wa Taasisi hiyo, Mhandisi. Emmanuel Hanai amesema ushirikiano kati ya TEEA na Wizara ya Madini u...

RAIS MSTAAFU DKT JAKAYA MRISHO KIKWETE AHANI MSIBA WA RAIS WA ZAMANI WA ALGERIA JENERALI MSTAAFU LIAMINE ZEROUL

Image
Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2026 ametia saini kitabu cha maombolezo kufuatia kifo cha Rais wa zamani wa Algeria, Jenerali Mstaafu Liamine Zeroual,  aliyefariki dunia mnamo Machi 28, 2026 akiwa na umri wa miaka 84 baada ya kuugua kwa muda mrefu. Jenerali Zeroual, aliyependwa na kuheshimikka sana, alichaguliwa kuwa rais mwaka 1995 katika kipindi kigumu cha vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Algeria. Alianzisha mageuzi ya kisiasa, ikiwa ni pamoja na kuratibu uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi. Hata hivyo alijiuzulu mapema mwaka 1998 kabla ya kumaliza muhula wake wa miaka mitano ili kutoa nafasi kwa mpito wa kisiasa, na tangu hapo aliishi maisha ya faragha bila kujihusisha sana na siasa. Hadi leo anakumbukwa kama kiongozi aliyetoa mchango muhimu katika kuiongoza Algeria katika kipindi cha mpito na changamoto kubwa za kisiasa na kiusalama. Akiongea na Balozi wa Algeria nchini Mheshimiwa Ghalib Zermane, Dkt Kikwete alisema Algeria na Tanzania imekuwa rafiki wa ka...

MAFUTA KUPANDA BEI, SERIKALI YAAHIDI SULUHISHO KWA WANANCHI

Image
  Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali itaendelea kusimamia upatikanaji wa bidhaa za mafuta ya petroli na mafuta mengine ili kuhakikisha bei zake zinaendelea kuwa himilivu, licha ya kuwepo kwa changamoto za kiusalama za kikanda na kimataifa ikiwemo za Mashariki ya Kati zilizosababisha kupanda kwa bei ya mafuta nchini. “Tumeona bei zimeanza kupanda, tutakaa ndani ya Serikali kuweza kuhakikisha tunakabiliana nalo vipi, ili wananchi wananchi wanaendelea kupata mafuta kwa bei wanazoweza kumudu na kudhibiti kupanda kwa gharama za maisha,” amesema Dkt. Mwigulu  Amesema hayo leo, tarehe 1 Aprili 2026, wakati akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2026/2027 Bungeni, jijini Dodoma.  Katika hatua nyingine, amesema Serikali imeendelea kusimamia mifumo ya kuagiza, kuhifadhi na kusambaza mafuta, pamoja na kuongeza uwezo wa kupokea na kuhifadhi mafuta katika bandari za Dar es Salaam na Mtwara. Aidha, amesema Serikali inaendelea kutekeleza mradi wa...