Posts

Showing posts from July, 2024

MBUNGE NGASSA AWAHIMIIZA WANANCHI KILIMA PAMBA

Image
Mbunge wa Jimbo la Igunga Mhe. Nicholaus George Ngassa ametoa wito kwa wananchi wa jimboni kwake kulima pamba kwa wingi kwani zao hilo ni muhimu kwa maendeleo yao. Mh.Ngassa ameyasema hayo Julai 16,2024 wakati akizungumza na wananchi alipokuwa kwenye ziara yake ya kutoa mrejesho mara baada ya kutoka kwenye Bunge la bajeti. "Wana Igunga tuendelee kulima pamba kwa wingi,kwani zao la pamba ni dhahabu nyeupe"amesema Mh.Ngassa Mh Ngassa ameendelea na Ziara Jimboni huku akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali kwa Wananchi pamoja na Kutoa mrejesho wa Bunge la Bajeti kwa Wananchi,Kuona Maendeleo ya Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo. Aidha Mh.Ngassa ameendelea Kuhamasisha Wananchi kujitokeza kwenye maboresho ya Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na Kujiandikisha kwenye Daftari la Wakazi,kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Mwaka 2024 pamoja na Kusikiliza Kero za Wananchi na kuzipatia ufumbuzi.

RC CHALAMILA APOKEA MELIVITA YA MATIBABU,AWATAKA WATANZANIA KUJITOKEZA KWA WINGI

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Julai 16,2024 amepokea Melivita ya matibabu iitwayo Peace Ark ya Jeshi la ukombozi la watu wa China katika Bandari ya Dar es Salaam. RC Chalamila akizungumza wakati wa mapokezi hayo amesema Melivita hiyo itakuwepo Jijini Dar es salaam kwa ajili ya kutoa huduma za kitabibu kwa wakazi na  watanzania kwa ujumla kuanzia Julai 16,2024 hadi Julai 23,2024 ambapo leo Julai 16, 2024 ni siku maalum ya uzinduzi, na kuanzia Julai 18-23 2024 ndiyo siku rasmi ya kuanza kutoa matibabu kwa wananchi.  Huduma hizo za kitabibu zinatolewa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka sitini(60) ya ushirikiano kati ya Tanzania na China na maadhimisho ya miaka sitini (60) tangu kuanzishwa kwa JWTZ tarehe 01 Septemba,1964. Aidha RC Chalamila amesema huduma za kitabibu zinazotarajiwa kutolewa ni pamoja na vipimo, tiba za kawaida pamoja na upasuaji wa kawaida, magonjwa ya kina mama, mifupa, njia ya mkojo, macho, pua, koo, meno, moyo, utumbo pamoj...

BIL. 8.9 YAONGEZWA KUBORESHA UKARABATI WA BANDARI KIGOMA

Image
  Tanzania imepokea msaada wa nyongeza wa Yen za Japan milioni 548 sawa na shilingi bilioni 8.9 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa ukarabati wa Bandari ya Kigoma baada ya marekebisho ya mikataba miwili ya msaada kati ya Tanzania, Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) na Ubalozi wa Japan. Mikataba ya marekebisho ya msaada imesainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba kwa niaba ya Serikali ya Tanzania, Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Yasushi Misawa na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan  Tanzania, Bw. Hitoshi Ara, kwa niaba ya Japan. Akizungumza baada ya kusainiwa kwa marekebisho ya mikataba hiyo, Dkt. Mwamba amesema kuwa, awali Serikali ya Japan kupitia mikataba iliyosainiwa Februari 4, 2022 ilitoa msaada wa Yen za Japan bilioni 2.73 sawa na shilingi bilioni 44.42 kwa ajili ya ukarabati wa Bandari hiyo. “Jumla ya msaada uliotolewa na Serikali ya Japan unakuwa Yen za Japan bilioni 3.27 sawa na shilingi bil...

SIASA ZA KISASA NI KUTATUA CHANGAMOTO ZA WANANCHI

Image
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora na Mbunge wa Kibakwe, Mhe.George Simbachawene amesema siasa za kisasa ni kutatua changamoto zinazowakabili wananchi na sio kuzungumza maneno matupu huku akiwataka wananchi kuwapuuza wale wote wanaokejeli maendeleo yaliyofanywa na Serikali . Ameyasema hayo leo Julai 11,2024 wakati akizungumza na wananchi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Kibakwe iliyopo Jimbo la Kibakwe, Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa jijini Dodoma ambapo amesema Kibakwe ya  sasa ni  tofauti sana na ile ya miaka kadhaa iliyopita, huku akitolea mfano kuwa mwaka 2005 jimbo hilo lilikuwa dhoofu sana kwenye huduma za kijamii ikiwemo elimu, afya, maji, umeme pamoja na barabara. “Kibakwe ninayoiona leo inafurahisha sana, tumetekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwa vitendo na kwa kiasi kikubwa sana kwani utitiri wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa mnaiona wenyewe” amesema Mhe. Simbachawene. Akizungumzia mradi wa miu...

UCHAGUZI WA WABUNGE,SERIKALI ZA MITAA KUFANYIKA 2026

Image
  Rais wa Cameroon Paul Biya Jumanne alipata kibali kutoka kwa wabunge kurudisha nyuma uchaguzi wa wabunge na wa serikali za mitaa hadi 2026, hatua ambayo vyama vya upinzani vinahofia kutaathiri uwezo wao wa kuwania urais mwaka ujao. Wabunge kutoka chama cha Bw Biya cha Cameroon People’s Democratic Movement (CPDM), ambao wanashikilia kura nyingi katika Bunge la Kitaifa, walipiga kura kuunga mkono mswada huo wa kuongeza muda wao kwa mwaka mmoja hadi Machi 2026. Hivyo, uchaguzi wa wabunge na manispaa utafanyika baada ya 2025 kura ya urais. Kuahirishwa huku kulihalalishwa na hitaji la “kupunguza kalenda ya uchaguzi”, kulingana na François Wakata Bolvine, Waziri Mjumbe wa Urais, nchi ambayo hapo awali ilikuwa imepanga chaguzi nne za mwaka ujao, pamoja na ile ya mabaraza ya kikanda. Akiwa na umri wa miaka 91, Bw Biya ni mmoja wa marais waliokaa muda mrefu zaidi barani Afrika. Akimrithi Ahmadou Ahidjo mwaka 1982, ameshinda mfululizo wa chaguzi, ukiwemo ule wa mwisho wa 2018, uliokumbwa n...