JKI YATOA MKONO WA IDDI KWA WENYE UHITAJI KIPUNGUNI, ILALA
****** Taasisi ya isiyo ya Kiserikali ya Jamii Kwanza initiative (JKI) kwa Kushirikiana na Ofisi ya Serikali ya Mtaa wa Amani Kata ya Kipunguni,Ilala Jijini Dar es salaam Leo Machi 29,2025 imefanikisha kutoa mkono wa Iddi kwa watu wenye uhitaji wakiwemo Yatima na Wajane ili waweze kusherehekea sikukuu ya Eid El Fitri inayotarajiwa siku ya Jumatatu inategemea na kuandama kwa mwezi. Akizungumza mara baada ya kugawa sadaka hiyo Mkurugenzi wa JKI Daniel Migera amesema kuwa kitendo walichokifanya ni moja ya jukumu lao kama Taasisi kurejesha kwa Jamii shukurani na kudumisha amani,upendo na furaha. "Tumeamua kunyoosha mkono ili kudumisha amani na Umoja,tumetoa swadaka hiyo ili Kuwawezesha na wao kufurahia hii muhimu kwao mara baada ya kumaliza Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani " Amesema Migera. Bw. Migera ametoa Rai kwa Taasisi zingine wakiwemo Wadau mbalimbali, watu wenye Uwezo kuwasaidia wenye uhitaji Maalum kwani kufanya jambo kama hilo ni muhimu kwa kujenga amani,Umoja, mshik...