Na Mwandishi Wetu, TABORA Zaidi ya watalii 500 wamefurika leo, Oktoba 18, 2025, katika Bustani ya Wanyamapori Tabora (Tabora Zoo) kushiriki katika Tamasha la Nyamapori Choma lililoandaliwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Kanda ya Magharibi. Tamasha hilo lililolenga kuhamasisha utalii wa ndani pamoja na matumizi endelevu na halali ya rasilimali za wanyamapori, limevutia watalii kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi, likihudhuriwa na viongozi wa Serikali wakiwemo Wakuu wa Wilaya za Tabora na Uyui, wananchi wa Mkoa wa Tabora na mikoa jirani, pamoja na wageni kutoka mataifa mbalimbali duniani. Wananchi waliohudhuria tamasha hilo wameipongeza TAWA kwa ubunifu wa kuandaa tukio hilo, wakieleza kuwa limewapa fursa ya “kuonja ladha ya matunda ya uhifadhi” unaotekelezwa na Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii Kwa kuhakikisha wananchi wananufaika na rasilimali hizo Kwa njia halali bila kuathiri uhifadhi endelevu. Kwa siku nzima ya leo, anga la Tabora ...