Waziri wa Maliasili na Utalii,  Mhe. Dkt. Pindi Chana(Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Kenya nchini Tanzania, Mhe. Isaac Njenga pembezoni mwa Onesho la Kimataifa la Swahili International Tourisim Expo-S!TE (S!TE 2024) jijini Dar es Salaam leo Oktoba 12,2024.

Lengo la kikao hicho ni kujadiliana masuala mbalimbali ya ushirikiano katika Sekta ya Maliasili na Utalii baina ya nchi za Kenya na Tanzania. 

Kikao hicho kimehudhuriwa na Naibu Waziri wa  Maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Utalii Tanzania(TTB), Dkt. Ramadhan Dau, Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Utalii, Nkuba Mabula, Mkurugenzi Mkuu Bodi za Utalii Tanzania(TTB), Ephraim Mafuru na Mkurugenzi wa Idara ya Utalii, Dkt. Thereza Mugobi


Comments

Popular posts from this blog

SEKTA YA NISHATI IWE KICHOCHEO CHA KUIUNGANISHA AFRIKA KUJENGA UCHUMI