RC CHALAMILA AWEKA WAZI MIKAKATI YA JIJI LA DAR 2025



Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila katika salamu zake za Christmas amesema Jiji la Dar es Salaam linatarajia kuanzisha mfumo wa ufanyaji biashara kwa saa 24 kwa mara ya kwanza, hatua inayolenga kuboresha uchumi na kuwa kitovu cha biashara ndani na nje ya nchi.
Hayo amesema leo wakati akitoa taarifa ya mwisho wa mwaka ya mkoa wa Dar es salaam pamoja na salamu za Siku ya Christmas na mwaka mpaya ambapo amesema huduma hiyo itazinduliwa rasmi Januari 2025 katika eneo la Kariakoo, kabla ya kusambazwa katika maeneo mengine yatakayobainishwa na viongozi wa wilaya na halmashauri.
Comments
Post a Comment