Skip to main content

PROF. LIPUMBA APANGA SAFU YA UONGOZI/ AFANYA UTEUZI


Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) Prof. Ibrahim Lipumba.

THE CIVIC UNITED FRONT (CUF- Chama Cha Wananchi)

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTEUZI:

Kwa kuzingatia Katiba ya CUF- Chama Cha Wananchi ya mwaka 1992 Toleo la 2019, Ibara za 91(1) na 92(1), nimemteua Mhe. Rajab Mbarouk Mohamed kuwa Katibu wa Kamati ya Itifaki na Udhibiti na Mhe. Juma Wandwi kuwa Naibu Katibu wa Kamati ya Itifaki na Udhibiti.

Wateule wanaanza kazi mara moja na watathibitishwa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa kikao kijacho. Uteuzi wa Wakurugenzi wengine utatangazwa kwa kadri Uteuzi utavyokamilika.

HAKI SAWA NA FURAHA KWA WOTE!


Prof. Ibrahim Lipumba
Mwenyekiti Taifa
CUF- Chama Cha Wananchi
Januari 13, 2025```

Comments

Popular posts from this blog

SEKTA YA NISHATI IWE KICHOCHEO CHA KUIUNGANISHA AFRIKA KUJENGA UCHUMI