Popular posts from this blog
MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI , DARASA LA NNE 2025
SEKTA YA NISHATI IWE KICHOCHEO CHA KUIUNGANISHA AFRIKA KUJENGA UCHUMI
📌 *Yasisitiza utekelezaji wa miradi ya kipaumbele ya Nishati* 📌 *Kapinga ataka SADC kuweka dhamira thabiti na mikakati madhubuti ya utekelezaji wa Ajenda ya Nishati Safi ya Kupikia* Mawaziri wanaoshughulikia masuala ya Nishati na Maji wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wametaka Sekta ya Nishati kuwa kichocheo cha kuiunganisha Afrika katika kujenga uchumi wake. Wamesema hayo leo Julai 4, 2025 wakati wakihitimisha mkutano wa SADC jijini Harare nchini Zimbabwe ambao ulilenga kuimarisha na kujadili masuala mbalimbali yatakayowezesha mtangamano wa Kikanda katika sekta za nishati na maji. Akizungumza wakati akihitimisha mkutano huo, Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Umeme wa Zimbabwe, Mhe. Dkt. July Moyo, ameitaka jumuiya hiyo ya SADC kuipa kipaumbele sekta ya nishati na maji ili kuifanya kuwa na tija kwa wananchi katika kukuza uchumi wao kwa kuwa nishati ni chanzo kikubwa cha maendeleo. Aidha, ameipongeza Tanzania kwa kuandaa na kuwa mwenyeji wa kufanikisha Mkut...
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga wakati wa uwasilishaji wa taarifa ya hali ya uhifadhi wa mafuta nchini katika Bohari za Tanga na Mtwara kwa wajumbe wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Jijini Dodoma, Januari 20, 2025.
“Serikali ipo katika taratibu za kuboresha miundombinu ya upokeaji na uhifadhi wa bidhaa za mafuta katika Bandari za Tanga na Mtwara ili kuendana na ukuaji wa mahitaji ya bidhaa za mafuta katika maeneo hayo.” Amesema Kapinga.
Amesema Serikali inaendelea kushirikisha wadau mbalimbali katika sekta ya mafuta ili kuhamasisha uwekezaji wa miundombinu ya upokea mafuta katika Bandari za Tanga na Mtwara ikiwemo kampuni binafsi zenye bohari za bidhaa za mafuta.
Vile vile, Kapinga amesema kuwa Serikali kupitia Shirika la Viwango Tanzania (TBS) inaendelea na ujenzi wa Maabara ya kupima ubora wa mafuta katika Bandari ya Tanga ili kufupisha muda wa kupata majibu ya vipimo vya ubora wa bidhaa hizo.
Aidha, Serikali kupitia shirika la Maendeleo ya Petrol Tanzania (TPDC) inaendelea na mikakati ya uwekezaji wa Bohari ya bidhaa za mafuta katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Mkoa wa Dodoma.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Mhe. David Mathayo David ameipongeza Wizara ya Nishati, Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) pamoja na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) kwa kuendelea kuimarisha mazingira wezeshi ya upatikanaji wa bidhaa ya mafuta nchini.
Kwa kuendelea kuimarisha miumbombinu mbalimbali ya uzalishaji, usambazaji na usafirishaji wa umeme katika maeneo mbalimbali nchini