KOROGWE WAIPONGEZA SERIKALI KWA UTEKELEZAJI WA MIRADI YA UMEME.









📌 Ni katika ziara ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan mkoani Tanga
📌 Vijiji vyote 118 vyafikishiwa umeme
📌 Naibu Waziri Kapinga ashiriki ziara

Wananchi wa Wilaya ya Korogwe Mkoani Tanga wameipongeza serikali kwa utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini, ambapo sasa vijiji vyote 118 vya wilaya hiyo vimeunganishwa na nishati ya umeme.

Pongezi hizo zimetolewa na Mbunge wa Korogwe Vijijini, Mhe. Timotheo Mzava, leo Februari 24, 2025, wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliyekuwa Wilayani Korogwe kukagua miradi ya maendeleo.

"Tarehe 15 Machi 2021 ulikuwa kwenye viwanja hivi na sisi wabunge tulipata nafasi ya kusema. Tuliyoyaomba, ikiwemo umeme vijijini, umeyatekeleza. Tunakushukuru sana," amesema Mhe. Mzava.

Ameeleza kuwa wakati wa ziara ya awali ya Rais Samia, vijiji 54 kati ya 118 vya Korogwe Vijijini vilikuwa havina umeme. Hata hivyo, hadi sasa, vijiji vyote vimeunganishwa na wananchi wameanza kunufaika kwa kujihusisha na shughuli mbalimbali za kiuchumi zinazotegemea nishati hiyo.

Katika ziara hiyo, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga, alishiriki akimwakilisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko.


Comments

Popular posts from this blog

SEKTA YA NISHATI IWE KICHOCHEO CHA KUIUNGANISHA AFRIKA KUJENGA UCHUMI