WANAFUNZI WAWILI WAJITEKA NA KUDAI PESA KWA WAZAZI WAO

 


Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam limefanikiwa kuwakamata wasichana wawili kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo baada ya kutengeneza mazingira kuwa wametekwa na kwamba watekaji wanataka pesa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Februari 04, 2024, Kamanda Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema kuwa Januari 29, mwaka huu, Jeshi hilo liliwapata na kuwahoji wasichana wawili mwanafunzi wa Kidato cha Pili (16) na mwingine Mwanafunzi wa Darasa la saba (12) wakazi wa Vijibweni, Kigamboni jijini Dar es salaam.

Amesema wasichana hao wamekamatwa kwa tuhuma za kutoa taarifa za uongo baada ya kutengeneza mazingira kuwa wametekwa na kwamba watekaji wanataka pesa.

“Jeshi linalaani vitendo hivyo vya watu vyenye lengo la kujipatia pesa kwa njia za udanganyifu,” amesema.

Comments

Popular posts from this blog

SEKTA YA NISHATI IWE KICHOCHEO CHA KUIUNGANISHA AFRIKA KUJENGA UCHUMI