DAWASA YATEKELEZA MIRADI 25 YA BIL 987.6 KUANZIA KIPINDI CHA JULAI 2021
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (DAWASA) Mhandisi Mkama Bwire ameeleza kuwa Mamlaka hiyo imeendelea na utekelezaji wa Miradi zaidi ya 25 yenye thamani Shilingi Bilioni 987.6.
Mhandisi Bwire ameyasema hayo leo hii Jijini Dodoma Machi 11,2025 wakati akizungumza na Wanafishi wa habari akielezea mafanikio ya Mamlaka hiyo na mwelekeo wake kuelekea Maadhimisho ya miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita.
Amesema kati ya hizo Bilioni 987.6, miradi yenye thamani ya 232.9 imekamilika na kutoa huduma kwa wananchi na miradi yenye thamani ya Shilingi 754.7 bado ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.
"Katika kipindi cha kuanzia Julai 2021 DAWASA imeendelea na utekelezaji wa miradi zaidi ya 25 yenye thamani ya fedha za Kitanzania Shilingi Bilioni 987.6"
"Kati ya hizo Bilioni 987.6, miradi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 232.9 imekamilika na inatoa huduma kwa wananchi na miradi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 754.7 bado ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji ".
Aidha miradi iliyopo katika mipango ya muda mfupi na mrefu yenye thamani ya Shilingi Trilioni 3.1 imebuniwa na iko katika hatua mbalimbali za Maandalizi.
Pia Kaimu Mkurugenzi huyo amesema mtandao wa majitaka umeongezeka kutoka kilomita 450 hadi kilomita 519.4 sawa na ongezeko la kilomita 69.4.
Mhandisi Bwire ameongezea kuwa idadi ya maunganisho ya wateja wa majisafi imeongezeka kutoka 343,019 hadi 455,720 sawa na ongezeko la wateja 112,701 Kuongezeka kwa upatikanaji wa huduma ya majisafi kutoka wastani wa asilimia 89 hadi asilimia 93 na huduma ya usafi wa mazingira kutoka asilimia 25 hadi asilimia 45 




Comments
Post a Comment