CUF WAOMBA KIKAO NA RAIS SAMIA KUJADILI SUALA LA UCHAGUZI 2025
Chama Cha Wananchi CUF kimemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kuwaita wadau wa Demokrasia na Uchaguzi kwa ajili ya kufanya majadiliano yenye tija yatakayoamua kuwa Uchaguzi kuwa huru na wa haki.
Wito huo umetolewa na Mwenyekiti wa chama Cha Wananchi CUF prof.Ibrahim Haruna Lipumba Leo April 12,2025 wakati akizungumza na Wananchi kwenye Uzinduzi wa mikutano hadhara uliofanyika Manzese ,Jijini Dar es salaam.
Prof.Lipumba amesema kuwa Pamoja na kasoro zilizojitokeza kwenye Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 CUF inamtambua Rais Samia kama Rais halali wa nchi yetu na kuwa kauli yake ya "hakuna mwenye haki miliki ya nchi hii" iko haja ya kufanya majadiliano ya kina ili kuwawezesha Wananchi kufanya maamuzi sahihi kwenye uchaguzi wa Mwaka huu .
"Tunatakiwa kuwa na Uongozi unaojali watanzania tukae na Rais kuangalia vipengele vyenye matatizo tuvirekebishe ili Wananchi wawe na Imani kuwa uchaguzi utakuwa wa huru na haki.
Aidha Ameongeza kuwa hali ya Maisha ya Watanzania ni magumu vijana hawana ajira na nchi Ina rasilimali nzuri ,tukiwa na sera nzuri zitapatikana ajira na kuweza kupunguza makali ya maisha na kuleta mabadiliko.
Ametoa Mfano kwa Mkoa wa Dar es salaam Kuna maneno ambayo kunweza kuanzishwa viwanda na vijana wakapata ajira.
Kwa upande wa Elimu Prof. Lipumba amesema kuwa sekta hiyo ni muhimu kwa maendeleo ya nchi,inapaswa kuwekeza kwenye Elimu kwani tusipowekeza tutaachwa nyuma.
Amesema Iko haja ya kuwekeza kuanzia kwenye Elimu ya shule za Msingi sambamba na kudundisha masomo ya computer(Tehama),

Comments
Post a Comment