Skip to main content

DKT. BITEKO AMUWAKILISHA RAIS SAMIA UWEKWAJI WAKFU ASKOFU MTEULE JIMBO LA IRINGA


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akisalimiana na Askofu wa Mafinga, Mhashamu Vincent Mwagala wakati alipowasili katika Ibada ya kumsimika na kumuweka wakfu Askofu wa Jimbo la Iringa, Mhashamu Romanus Mihali iliyofanyika katika Viwanja vya Kichangani, Mjini Iringa, Aprili 27, 2025.


Dkt. Biteko anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Sherehe za kuwekwa wakfu Askofu Mteule, Romanus Elamu Mihali kuwa Askofu wa Jimbo la Kitume la Iringa.







Comments

Popular posts from this blog

SEKTA YA NISHATI IWE KICHOCHEO CHA KUIUNGANISHA AFRIKA KUJENGA UCHUMI