JESHI LA POLISI WATOA ONYO KWA VIONGOZI WA CHADEMA
Jeshi la Polisi limewataka Viongozi wa Chama Cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kutohamasisha watu kukusanyika tarehe 24/04/2025 mahakama ya hakimu mkazi kisutu kwa lengo la kufanya vurugu na kushindikiza mamlaka za kisheria kumwachia mwenyekiti taifa wa chama chao Tundu Lissu.Akizungumza mapema Leo April 17, 2025, kamanda wa polisi Kanda maalum ya Dar es salaam Jumanne Muliro amesema jeshi la polisi alitasita kuwashughulika vikali yeyote atakayeshiriki kufanya vurugu kwa mujibu wa Sheria za nchi.
"Jeshi la polisi linawakumbusha wahusika kuwa mahakama ni mamlaka za kisheria zilizo huru na hazipaswi kutishwa ama kuingiliwa" Amesema Muliro.
Sambamba na hilo kamanda Muliro ametowa wito kwa wazazi na walezi kuwa na uangalizi wa karibu kwa watoto wakati wa matembezi na mikusanyiko mbalimbali katika sherehe ya sikukuu ya pasaka.
Aidha amesema nyumba na makazi yasiachwe bila uangalizi wakati wa sherehe za pasaka lakini pia amesisitiza swala la usalama barabarani kwa madereva wa vyombo vya moto na watumiaji wengine wa Barabara kuzingatia Sheria ili kuepusha ajali.
Katika hatua nyingine kamanda Muliro amesema Jeshi la polisi limejipanga kuhakikisha ulinzi katika kipindi Cha sikukuu ya Pasaka wamejipanga vizuri kuhakikisha waumini wanashiriki na kusherekea sikukuu hiyo kwa amani na utulivu.
"Jeshi la Polisi tumejipanga kuhakikisha kuwa katika kipindi chote za sikukuu inasherekewa kwa amani na utulivu nitoe rai kwa wakazi wa jiji na maeneo ya jirani kusherekea sikukuu" Alisema Kamanda Muliro


Comments
Post a Comment