Skip to main content

PAPA FRANCIS AFARIKI DUNIA

 



 Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis, amefariki dunia leo Aprili 21,2025 kwenye Jumatatu ya Pasaka akiwa na umri wa miaka 88.

Vatican imethibitisha na kusema Papa amefariki akiwa kwenye makazi yake katika Casa Santa Marta, Vatican

na taarifa zaidi kuhusu kifo chake zitatolewa.

Papa ambaye alizaliwa mwaka 1936 hivi karibuni amepitia changamoto ya upumuaji hadi kuhitaji mashine ya kusaidia kupumua na amekuwa akikabiliwa na matatizo ya kiafya ikiwemo maambukizi ya mapafu(nimonia) hadi kupelekea kulazwa kwa wiki kadhaa kabla ya baadaye afya yake kuimarika.

Comments

Popular posts from this blog

SEKTA YA NISHATI IWE KICHOCHEO CHA KUIUNGANISHA AFRIKA KUJENGA UCHUMI