KERO YA MAJI VIJIJI VYA MSISIMA,MNALAWI,NAMTUMBO YAPATA MUAROBAINI

 


 Wananchi wa vijiji vya Msisima na Mnalawi vilivyopo katika halmashauri ya wilaya ya Namtumbo sasa wanaanza kuona mwanga wa matumaini kufuatia kuanza kutekelezwa kwa mradi mkubwa wa maji unaogharimu zaidi ya shilingi bilioni 1.1, chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA).


Kwa muda mrefu, wakazi wa vijiji hivyo wamekuwa wakikabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa maji safi na salama, hali iliyowalazimu wanawake wajawazito kuchota maji mtoni wanapokwenda kujifungua katika vituo vya afya – maji ambayo si salama kwa matumizi ya binadamu.

Akizungumza wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi la mradi huo tarehe 15 Mei 2025, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa, Ndugu Ismail Aly Ussi, alisema kuwa mradi huu umejengwa kwa ubora wa hali ya juu na unatarajiwa kuondoa kabisa tatizo la maji kwa wananchi wa vijiji hivyo kwa asilimia 100.

Wananchi wa vijiji hivyo wameipongeza serikali kwa hatua hiyo, wakisema kuwa mradi huo unawapa matumaini makubwa ya kuondokana na mateso ya kutafuta maji safi kila siku, hasa katika kipindi cha kiangazi.

Mradi huu ni sehemu ya jitihada za serikali kuhakikisha kuwa wananchi waishio vijijini wanapata huduma bora za msingi, ikiwa ni pamoja na maji safi na salama, kama sehemu ya utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa.

Comments

Popular posts from this blog

SEKTA YA NISHATI IWE KICHOCHEO CHA KUIUNGANISHA AFRIKA KUJENGA UCHUMI