MWANAUME MMOJA AKAMATWA KWA TUHUMA ZA MAUAJI YA MSICHANA WA KAZI

Jeshi la Polisi mkoa wa Ruvuma linamshikilia mwanaume mmoja anayefahamika kwa jina la Eric Turuka, mkazi wa kitongoji cha Namihoro, kijiji cha Peramiho A, halmashauri ya wilaya ya Songea. Eric, mwenye umri wa miaka 23 na ambaye ni wa kabila la Wamatengo, anafanya kazi ya kuuza nyama ya nguruwe.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma, SACP Marco Chilya, Eric anatuhumiwa kumuua kwa kumkaba shingoni na kumchinja kwa kisu msichana anayefanya kazi za ndani, aliyefahamika kwa jina la Shukrani Ajiriwa, mwenye umri wa miaka 19 na mkazi wa kitongoji hicho hicho cha Namihoro.


Kamanda Chilya amesema tukio hilo la kusikitisha limetokea mnamo tarehe 15 Mei 2025, majira ya saa 9:45 mchana. Uchunguzi wa awali unaonesha kuwa chanzo cha tukio hilo ni wivu wa mapenzi baada ya wazazi wa marehemu kumkataa Eric kuwa mchumba wa binti yao, na badala yake kumpendelea mwanaume mwingine. Hali hiyo ilimsababisha mtuhumiwa kupata wivu mkali uliosababisha kuchukua maamuzi hayo ya kikatili.


Katika tukio jingine, lililotokea tarehe 8 Mei 2025, majira ya saa 6:30 usiku, kwenye mgodi wa Gold Field Company uliopo kijiji cha Lukalasi, wilaya ya Mbinga, mkoa wa Ruvuma, maji yaliingia ndani ya mgodi huo na kusababisha kifusi kutitia. Katika ajali hiyo ya mgodi, wachimbaji watatu waliokuwa kazini walifukiwa na kifusi hicho na kupoteza maisha.

Comments

Popular posts from this blog

SEKTA YA NISHATI IWE KICHOCHEO CHA KUIUNGANISHA AFRIKA KUJENGA UCHUMI