WAZIRI BASHUNGWA AWASILI BUNGENI KUWASILISHA BAJETI YA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCH


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent L. Bashungwa (Mb) akiwasili katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma, ambapo atawasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26, leo tarehe 26 Mei 2025.



Dodoma – Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Innocent L. Bashungwa (Mb.), leo asubuhi amewasili katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma kwa ajili ya kuwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026.

Mhe. Bashungwa anatarajiwa kueleza mbele ya Bunge mipango, vipaumbele, na mikakati ya wizara hiyo kwa mwaka ujao wa fedha, ikiwa ni pamoja na maboresho katika sekta za ulinzi wa raia, usimamizi wa sheria, huduma za dharura na masuala ya uhamiaji.
Bajeti hii ni sehemu ya utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa na Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala, ikilenga kuboresha huduma kwa wananchi na kuimarisha usalama wa ndani ya nchi.

Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inatoa wito kwa wananchi kufuatilia uwasilishaji wa bajeti hiyo kupitia vyombo rasmi vya habari na mitandao ya kijamii ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Daniel Sillo (Mb), akiwasili katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma kwa ajili ya kushiriki katika uwasilishaji wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Mwaka wa Fedha 2025/26, leo Mei 26, 2025.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw. Ally Gugu, akiwasili katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma kushuhudia uwasilishaji wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2025/26, leo Mei 26, 2025.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Dkt. Maduhu Kazi, akiwasili katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma kushiriki katika uwasilishaji wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2025/26, leo tarehe 26 Mei 2025.


Wakuu wa Vyombo vya Usalama vilivyo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wakiwasili katika Viwanja vya Bunge jijini Dodoma kwa ajili ya kushiriki katika uwasilishaji wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2025/26, leo Mei 26, 2025

Comments

Popular posts from this blog

SEKTA YA NISHATI IWE KICHOCHEO CHA KUIUNGANISHA AFRIKA KUJENGA UCHUMI