Skip to main content

WAZIRI MCHENGERWA ASHIRIKI KONGAMANO LA UCHUMI JIJINI ARUSHA



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa ni miongoni mwa viongozi waliohudhuria jukwaa la uchumi Arusha linalofanyika katika Ukumbi wa IACC Arusha.


Kongamano hili limejumuisha zaidi ya wadau 1000 kutoka maeneo mbalimbali duniani na kushirikisha mawaziri kadhaa wa sekta za tofauti.


Mwanamajumui wa Afrika Profesa Patrick Lumumba pia amealikwa kuwa miongoni mwa watoa mada.


Jukwaa hilo limeandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda ili kutoa fursa kwa wafanyabiashara wa Mkoa huo kupata ujuzi wa namna ya kutumia fursa za uchumi zilizopo mkoani Arusha.

Comments

Popular posts from this blog

SEKTA YA NISHATI IWE KICHOCHEO CHA KUIUNGANISHA AFRIKA KUJENGA UCHUMI