WAZIRI SILAA AWANUNULIA VITI 100 TAASISI YA TASACO

Mh.ametoa wito kwa Viongozi wa Jimbo la Ukonga kuwakimbilia wananchi pindi wapatapo Changamoto kwasababu Mwananchi akipata Changamoto haangalii kama una pesa ila Imani Yako na kujitoa kwako wakati wa matatizo.

Aidha Mh.Silaa amewaasa Wanachama wa TaSaCo kutumia njia nzuri wa utunzaji wa Fedha ili kujihakikishia usalama wake huku akitolea Mfano kuwa mwanadamu Kila siku anachangamoto na wakati wowote anaweza akajikopesha Fedha za Taasisi na baadae akashindwa kuzirudisha.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa TaSaCo hiyo Paul Chegere amesema kuwa wao kama Taasisi wanaamini kuwa maisha yao yameunganishwa na umoja ili kujiwekea akiba na kukopeshana hatimaye kuleta maendeleo binafsi,kwa jamii na Taifa kwa ujumla.

Ameongeza kuwa tumqini lao limejikita kwenye fursa na uwezeashaji ili kizifikia fursa hizo kwa kujikwamua kiuchumi huku hatma yao ukiwa imefungamana na uwepo wa Taasisi mbalimbali zenye kutoa huduma rafikiza binafsi na Serikali kama vile Benki ,Bima za afya na nyinginezo.

Kadhalika amesema lengo na natamanio yao ni kwamba wajasiriamali ambao hawako kwenye mifumo rasmi ya ajira ni kujiunga na bima za afya na kupata Matibabu kwa gharama nafuu.

TaSaCo ni Taasisi inayojumishwa na vikundi vya ujasiriamali vya kuweka na kukopa(vicoba) ambayo idadi yake inafikia 57,huku kukiwa na Wanachama 510 ambao wengi wamenufaika,wamefanikisha kuendesha maisha yao pamoja na kuinuka kiuchumi.















Comments

Popular posts from this blog

SEKTA YA NISHATI IWE KICHOCHEO CHA KUIUNGANISHA AFRIKA KUJENGA UCHUMI