ENG.NGULANGWA ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA UBUNGE KILWA KASKAZINI


Eng. Mohamed Ngulangwa akirejesha Fomu kwa Katibu wa Wilaya ya Kilwa, Mhe. Masendera.

KILWA, Juni 29 - Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma wa CUF–Chama Cha Wananchi, Eng. Mohamed Mshamu Ngulangwa, leo Jumapili amechukua na kurejesha rasmi fomu ya uteuzi ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Kilwa Kaskazini kupitia chama hicho.

Hatua hiyo imekuja kufuatia wito wa wazee na vijana wa Jimbo la Kilwa Kaskazini pamoja na Wilaya ya Kilwa waliomhimiza mjukuu na ndugu yao huyo kugombea nafasi hiyo ya uongozi, wakionesha imani kubwa juu ya uwezo na uadilifu wake.

Eng. Ngulangwa, ambaye ni mzaliwa wa Kilwa na mmatumbi halisi, anabeba sifa za kipekee kielimu na kitaaluma. Ana Shahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Ujenzi (Master in Engineering Management - MEM), Shahada ya Uzamili katika Usimamizi wa Biashara (MBA), pamoja na Shahada ya Uhandisi wa Ujenzi (BSc in Civil Engineering). Aidha, ana elimu ya dini ya Kiislamu katika kiwango cha Thanawi.

Jimbo la Kilwa Kaskazini ni mojawapo ya majimbo yaliyokuwa chini ya uongozi wa CUF kufuatia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, kabla ya sintofahamu za kisiasa kuvuruga mchakato wa uchaguzi mwaka 2020.

Comments

Popular posts from this blog

SEKTA YA NISHATI IWE KICHOCHEO CHA KUIUNGANISHA AFRIKA KUJENGA UCHUMI