MIGOGORO YA NDOA INAHARIBU MAADILI YA WATOTO
Wazazi na walezi wameaswa kupunguza Migogoro kwenye ndoa kwani ni moja kati ya vyanzo vya kuporomoka kwa maadili ya watoto,hivyo ni vyema kutengeneza mahusiano mazuri kwa wanandoa ili kuepuka Migogoro hiyo na kuishi kwa amani na upendo.
Rai hiyo imetolewa Leo Juni 18,2025 na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Machimbo kata ya Kipunguni, Wilayani Ilala Jijini Dar es salaam Yohana Isaya kwenye maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyoandaliwa na Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi(UWT) wa Tawi la Kitinye.
"Kuna baadhi ya Wanandoa wanagombanana kupigana mbele ya Watoto,baba anampiga mama na kumtukana huku watoto wakishuhudia Jambo ambalo linatoa funzo baya kwa watoto na kupelekea kutokuwa na maadili mwema"Amesema Isaya
Ameongeza kuwa iwapo wazazi au Walezi wakiwalea watoto wao kwenye maadili mema itasaidia kuwa na watoto wenye maadili ambao ni msaada kwa wazazi,jamii na Taifa hapo baadae.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi(UWT) Tawi la Kitinye Kata ya Kipunguni Jovina Bankobeza amesema kuwa Katika kuadhimisha sikuya Mtoto wa Afrika ni muhimu Serikali na wadau kuandaa mipango thabiti ya kuendeleza watoto ,kukuza ufahamubwa wazazi,walezi na jamii kuhusu utatuzi wa changamoto zinazowakabili watoto na kuzitafutia ufumbuzi.
Amesema kuwa UWT kama wazazi na walezi wa Jamii tuna Kila sababu ya kukumbusha wajibuwetu ili kuokoa kizazi cheti na kujenga mshikamano wa Pamoja Katika ujenzi wa Taifa.
Amesema ni wajibu wa kila mmoja kihimiza maadili na malezi ya kiimani, kuhamasisha kukemea na kupinga matumizi ya dawa za kulevya Katika jamii yetu, kufanya kazi kwa bidii na kujenga upendo na mshikamano .
Naye Afisa Ustawi wa Jamii Kata ya Kipunguni Tumaini Urio amesema kuwa suala la ukatili na unyanyasaji kwa watoto limeshika KASI sio Nchini tu ni Duniani kwa ujumla ,hivyo amewataka wazazi kufuatilia mienendo na kuwa karibu na watoto wao.
amesema iko haja kama jamii za kiafrika kuungana kwa pamoja kuwatetea kwa kutoa Elimu ili ukatili na unyanyasaji dhidi ya watoto uweze kupungua au kutokomea kabisa ili tuwe na jamii Bora itakayokuwa na maadili mazuri ambayo yatasaidia Katika ukuaji wa uchumi na maendeleo kwa ujumla.








Comments
Post a Comment