KWALA INDUSTRIAL PARK(KIP)ITATOA AJIRA 600,000
Chini ya Rais Samia, zaidi ya ajira 600,000 (ajira 100,000 za moja kwa moja na 500,000 zisizo za moja kwa moja) zinatarajiwa kupatikana kupitia Kwala Industrial Park, huku zaidi ya watu milioni 1 wakinufaika moja kwa moja na sekta mbalimbali zinazohusiana na mradi huu.
Vilevile, serikali inatarajia kukusanya mapato makubwa ya kodi na ushuru yanayokadiriwa kuwa zaidi ya shilingi trilioni 2 kwa mwaka, ambapo kati yake shilingi trilioni 1.2 ni mapato ya kodi pekee.

Comments
Post a Comment