RAIS SAMIA AMEJENGA SHULE MPYA ZA SEKONDARI 1000
Chini ya Rais Samia, Sekta ya Elimu imekua, ambapo ruzuku ya Elimu bila Ada imeongezeka kutoka shilingi bilioni 249.66 mwaka 2020|21 hadi shilingi bilioni 484.27 mwaka 2024|25, sawa na ongezeko la shilingi bilioni 234.61 asilimia 93.97).
Vilevile, vyumba vya madarasa vimeongezeka kwa 62,685 (kutoka 191,708 hadi 254,393), shule za sekondari zimeongezeka kwa 1,031 (kutoka 3,863 hadi 4,894) na mabweni kwa 1,000 (kutoka 2,245 hadi 3,245).
Mabadiliko haya yametokana na maamuzi ya Serikali kuongeza uwekezaji
kwenye elimu ili kupunguza msongamano wa wanafunzi, kuboresha
mazingira ya kujifunza na kutoa fursa sawa kwa watoto wote nchini.
3

Comments
Post a Comment