RAIS SAMIA AMETOA CHANJO YA BURE KWA WATOTO 1,600,000
Chini ya uongozi wa Rais Samia, huduma za chanjo kwa watoto chini ya miaka mitano katika Halmashauri 184 zimetolewa kwa kiwango kikubwa, ambapo watoto 1,610,303 kati ya 1,556,556 sawa na asilimia 103 walikamilisha dozi ya tatu ya chanjo ya Pentavalent (Penta3) inayokinga magonjwa matano hatari (dondakoo, kifaduro, pepopunda, homa ya ini aina ya B na Hib),
Huku watoto 1,526,884 sawa na asilimia 98 wakipata dozi ya pili ya chanjo ya Surua, inayolinda dhidi ya ugonjwa wa surua unaoweza kusababisha homa kali, nimonia na hata kifo.

Comments
Post a Comment