UZALISHAJI WA MAZAO YA CHAKULA WAFIKIA TANI MIL. 1.3 MKOANI SHINYANGA
Chini ya uongozi wa Rais Samia serikali imefanya mabadiliko makubwa kwenye sekta ya kilimo mkoani Shinyanga ikiwemo kuongeza matumizi ya mbolea kwa ajili ya shughuli za kilimo kutoka tani 5443 mwaka 2020
hadi tani 9,909 mwaka 2025.
Imeimarisha huduma za ugani kwa kununua
vitendea kazi ikiwemo pikipiki 214, vipima udongo 5 na vishikwambi 193 kwa ajili ya maafisa ugani na katika kuhakikisha kuwa kilimo kinafanyika katika misimu yote ya mwaka imeongeza skimu 13 za umwagiliaji kutoka
2 mwaka 2020 hadi 15 mwaka 2025 zilizojengwa katika 8 Halmashauri za wilaya za Shinyanga, Shinyanga Mjini, Manispaa ya Kahama, Msalala na Kishapu.
Hii imepelekea kuongezeka kwa mavuno ya mazao kutoka tani 684,200 mwaka 2020 hadi tani 884,116 mwaka 2025 pia kuongezeka kwa
uzalishaji wa mazao ya chakula kutoka tani 797,000 mwaka 2020 hadi tani 1,313,073 mwaka 2025 na mazao ya biashara kutoka tani 99,250 mwaka 2020 hadi tani 170,673 mwaka 2024.

Comments
Post a Comment