WAANDISHI WA HABARI WAKUMBUSHWA KUZINGATIA MAADILI YA KAZI KATIKA KIPINDI HIKI CHA UCHAGUZI.
Koch, amesema vyombo vya habari ni nguzo muhimu katika kulinda Demokrasia,vikihusisha wananchi na viongozi,hivyo waandishi wanapaswa kuepuka upendeleo,kutoa habari sahihi,kuheshimu faragha na kuepuka lugha ya chuki.
Aidha amesisitiza umuhimu wa mafunzo ya namna bora ya kuripoti habari zinazokuza uwajibikaji na ushiriki wa wananchi katika uchaguzi nyakati za uchaguzi.
Hata hivyo Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Media Brains,Jesse Kwayu,amesema Waandishi wa habari wanapaswa kutumia kalamu zao kuwaelimisha wananchi juu ya umuhimu wa kushiriki uchaguzi na kuchagua viongozi bora.
Ameongeza kuwa Demokrasia hudhoofika pale uandishi unapokuwa wa uchochezi au wa upande mmoja, na kusisitiza kutoa nafasi sawa kwa wagombea wanawake na wanaume.
Nae Mkurugenzi Mwenza wa Media Brains, Absalom Kibanda, amewataka waandishi kufuata Maadili, miiko na sheria za uchaguzi, kuepuka ushabiki wa kisiasa, na kuzingatia usalama wao wanaporipoti masuala ya kisiasa ili kuepuka kuligawa Taifa.


Comments
Post a Comment