WAHARIRI WAASWA KUZINGATIA MAADILI YA UHARIRI KIPINDI CHA UCHAGUZI


Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) Mhe. Jaji wa Mahakama ya Rufani Jacobs Mwambegele akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kikao cha Tume na Wahariri wa Habari kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Kikao hicho cha siku moja kilifanyika jijini Dar es Salaam leo Agosti 01, 2025.
Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Ndg Kailima Ramadhani akiwasilisha mada katika Kikao cha Tume na wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusu uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025. Kikao hicho cha siku moja kilifanyika jijini Dar es Salaam leo Agost 01, 2025.
Wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari walioshiriki mkutano wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Wahariri wa Vyombo vya Habari kuhusu Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 uliofanyika jijini Dar es Salaam mapema leo Agosti 01, 2025.


Dar es Salaam – Wahariri wa vyombo vya habari nchini wamehimizwa kufuata kwa umakini kanuni na maadili ya uchaguzi kwa lengo la kuhakikisha taarifa zinazotolewa hazimpendelei chama, mgombea au taasisi yoyote ya kisiasa, kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Wito huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), Mheshimiwa Jaji Jacobs Mwambegele, wakati wa kikao kazi kati ya Tume hiyo na wahariri wa vyombo vya habari.

“Vyombo vya habari vina nafasi ya kipekee katika kuleta uchaguzi wa amani, haki na uhuru. Tunawaomba wahariri kusimamia ukweli, uwajibikaji na kutotoa nafasi kwa habari zenye mwelekeo wa kichochezi au upendeleo,” amesema Jaji Mwambegele.

Ameeleza kuwa uchaguzi ni mchakato shirikishi unaohitaji ushirikiano wa karibu kati ya Serikali, vyombo vya habari, asasi za kiraia na wananchi ili kufanikisha uchaguzi wa kidemokrasia.

“Tukisimama pamoja, tukiheshimu sheria na maadili, tutashuhudia uchaguzi bora zaidi katika historia ya taifa letu,” amesema kwa kusisitiza Jaji Mwambegele.

Kikao hicho kinalenga kuimarisha ushirikiano kati ya Tume na vyombo vya habari ili kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi na zisizopotosha wakati wa kipindi cha uchaguzi.

Comments

Popular posts from this blog

SEKTA YA NISHATI IWE KICHOCHEO CHA KUIUNGANISHA AFRIKA KUJENGA UCHUMI