WATUMIAJI WA INTANET NCHINI WAFIKIA MILIONI 54
Chini ya Rais Samia, watumiaji wa intaneti wameongezeka kutoka milioni 29.8 mwaka 2021 hadi milioni 54.1 mwaka 2025, ongezeko la asilimia 81.6.
Hali hii imechochea maendeleo ya uchumi wa kidijitali (digital economy), kuongeza fursa za elimu ya mtandaoni (online learning), biashara mtandao (e-commerce) na uvumbuzi katika sekta ya teknolojia.
Kwa kulinganisha, Kenya ina watumiaji wa intaneti milioni 22.7 na Uganda milioni 14.2, jambo linaloonyesha Tanzania imepiga hatua kubwa zaidi katika upanuzi na matumizi ya intaneti ukilinganisha na nchi jirani.

Comments
Post a Comment