Skip to main content

TAWA YAMNASA SIMBA MLA MIFUGO KONDOA





-Jitahada zaendelea  kuwasaka simba wengine

Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA imefanikiwa kumkamata simba jike akiwa hai baada ya mfululizo wa mashambulizi ya wanyama hao kuua zaidi ya mifugo 20 katika Wilaya ya Kondoa, mkoani Dodoma.



Simba huyo aliingia kwenye rada za askari wa TAWA majira ya saa 4 usiku, Septemba 6, 2025, katika kijiji cha Chemchem, kufuatia msako mkali uliodumu kwa siku tatu ambapo mnyama huyo alijikuta tayari  amenasa katika mtego  maalum uliowekwa na Askari hao.


Imeripotiwa kuwa wanyama simba wamekuwa wakifanya mashambulizi ya mifugo katika vijiji vya Chemchem na Iyoli, Kata ya Kingale ambapo katika nyakati tofauti waliua ng’ombe wawili na punda mmoja na  baadae  kuua ng’ombe 18 katika gereza la king'ang'a. Aidha, waliripotiwa pia kuua mbuzi wawili katika kijiji cha Iyoli.



Comments

Popular posts from this blog

SEKTA YA NISHATI IWE KICHOCHEO CHA KUIUNGANISHA AFRIKA KUJENGA UCHUMI